Nipo hapa Arusha kikazi....leo siku ya nne naona hali ya hewa ya kawaida na ni nzuri sana....kwa sisi tuliotokea Dar kwenye joto huku naona burudani mpaka natamani ningehamishia makazi huku........Arusha kuzuri sana.....kila mtu yupo bize na shughuli zake....si kina mama, mabinti, mabibi na mababu mpaka vitoto kila mtu ni pirika pirika tu........baridi ikinizidia nakimbilia pale pembeni ya uwanja wa sheik Amri Abeid nakunywa tangawizi na karanga......napoza baridi.......kuanzia asubuhi nilivyooga mpaka muda huu sijatoka hata jasho........