Kama unasafiri kuja Arusha ujipange hali ya hewa ni mbaya sana

Kama unasafiri kuja Arusha ujipange hali ya hewa ni mbaya sana

Mbeya nadhani imezidi nimepika maharage Leo Siku ya nne hayajachacha hata
Ni kweli ukiwa Mbeya,Iringa na Niombe Maharage yanachukua mda mrefu sana kuchacha. Huwa yanaenda siku 4 hadi 5 ndo yanachacha. Wakati mikoa ya joto ni siku moja tu.
 
Kitu kipo Makete ni hatari, unalala na pea tatu za soksi na mablanketi mawili. Ila nakumbuka Sumbawanga enzi hizooo, unaenda na baiskeli shuleni halafu huwezi kuchomoa ufunguo wala kuifunga, mikono imeganda!!
 
97 naingia iringa mjini nikitokea morogoro, nakumbuka ilikuaa saa 4usiku, niliingia ndani, nikaitiwa msosi nikagoma kutoka ndani,nikaachwa nilale, asubuhi naamshwa kuonga na kunywa chai namuangalia dada aliyenifata kwa umakin"unasemaa"mimi huyo nikaoge!!! Aaaa wee.
Nikajigubika na kulala tena, nilikuja kuweza kuamka saa nne.

Ule mkoa bana acha tu. Baridi na inapiga mruzi, yaani asubuhi mmeamka mnakwenda stand, kubeba begi au mfuko nia dhabu, maana unatamani mikono ushike kifua muda wote.
 
Jiwe Alituelekeza Kufyatua Watoto Nchi Ikue Kiuchumi Kama China Na India
 
97 naingia iringa mjini nikitokea morogoro, nakumbuka ilikuaa saa 4usiku, niliingia ndani, nikaitiwa msosi nikagoma kutoka ndani,nikaachwa nilale, asubuhi naamshwa kuonga na kunywa chai namuangalia dada aliyenifata kwa umakin"unasemaa"mimi huyo nikaoge!!! Aaaa wee.
Nikajigubika na kulala tena, nilikuja kuweza kuamka saa nne.

Ule mkoa bana acha tu. Baridi na inapiga mruzi, yaani asubuhi mmeamka mnakwenda stand, kubeba begi au mfuko nia dhabu, maana unatamani mikono ushike kifua muda wote.
Nq mimi mara ya kwanza kuingia Iringa ilikuwa juni 1997.siku ya kwanza nilivaa nguo zote zilizokuwa kwenye begi,soksi na viatu,mablanketi ya kutosha,nikalala,lakini baridi linapenya.baada ya miaka kadhaa nilizoea,nikawa navaa sweta moja tu.

Kuoga kwa wiki mara moja tu,na mwili hautoi jasho,harufu,na wala hujisikii uchovu.
 
Nimefika Arusha na hata Kilimanjaro kule maeneo ya Umbwe milimani na sehemu kadhaa Tanzania ila niseme tu Baridi ya Njombe na Mbeya ni another level
 
Mtoa mada ushawahi kufika japo hata cape town south África?usingesema Tanzania kuna baridi!!ushawahi kukutana na maximum nyuzi joto 5?
Mtu katoa taarifa za Arusha, wewe unaleta habari za south Africa, wabongo kwa kujifanya much know!
 
Unaogopa kwenda Arusha??
Arusha kawaida Sana Mkuu ukilinganisha na njombe
Kuna jamaa alitoka Arusha nilikutana nae Mbeya ndo akaniambia kule muda mwingi wanakuwa msimu wa baridi watu wapo na makoti mazito, mizura na gloves mikononi, so nkajua huku Mbeya au Njombe cha mtoto
 
Back
Top Bottom