Kama unataka kuondoka kwenye umasikini, waepuke masikini kama ukoma

Kama unataka kuondoka kwenye umasikini, waepuke masikini kama ukoma

Mkuu samahani sana kwa sababu nadhani kwamba kitabu chako kinaelezea tabia za kitajiri ambazo ndio issue kubwa inayofanya kitabu hiko kiwe sokoni.

Na wala kitabu hiko chenye page 200 zote sidhani kama page hizo zinazungumzia nini maana ya utajiri,bali ninatumai kwamba maana ya neno utajiri hasa kwako haina ulazima wa kununua kitabu ndipo utuelekeze.

Kwa sababu maelezo yako katika uzi huu yakikadiriwa yanafika page hata moja.

So kama umeweza kuandika maelezo anayochukua page moja vipi ishindikane kuelezea maana ya utajiri ambayo huwenda isifike hata nusu page ikiwa utaamua kufupisha maana ?
Nikiwaambia muache kuuliza maswali ya kijinga mnakimbilia kupaniki.
Nimekupa maelekezo hapo, bado unalazimisha kile unataka wewe.
Ndiyo maana nasema pata pesa na maswali ya kijinga kama haya hutasumbua nayo watu.
Kila la kheri.
 
Sawa mkuu asante.
 
Rafiki yangu mpendwa,

Hivi unajua ya kwamba umasikini huwa unaambukizwa kama magonjwa yanayoambukizwa?

Ndiyo, hiyo ni kweli kabisa, pale unapokaa na masikini, wanakusababisha uendelee kubaki kwenye umasikini.

Huenda kwa kusoma sentensi hizo chache umejisikia vibaya, umenichukulia mbaguzi na mwenye dharau.

Sitakushangaa kwa hilo, kwani hata mimi wakati najifunza hili kwa mara ya kwanza sikulielewa haraka.
Ni mpaka pale niliposoma tafiti baada ya tafiti kwenye nguvu ya wale wanaotuzunguka na jinsi tabia inavyoweza kuambukizwa.

Kuhusu nguvu ya wanaokuzunguka, Jim Rhon alikuwa akinukuliwa mara kwa mara akisema vile ulivyo ni wastani wa watu watano unaotumia nao muda wako mwingi.

Hili unaweza kulithibitisha wewe mwenyewe, bila hata ya kutumia nguvu sana.
Yaangalie maisha yako, kisha angalia maisha ya marafiki zako wa karibu.
Angalia wana watoto wangapi, wana magari ya aiba gani, wana nyumba au wanakaa maeneo gani, kazi na/au biashara wanazofanya.

Utashangaa jinsi ambavyo mna ufanano mkubwa.
Je unadhani hilo limetokea tu kama ajali?

Hapana, kuna nguvu kubwa sana inayofanya kazi, nguvu inayohakikisha hutofautiani sana na wale unaotumia nao muda wako mwingi.

Kwa kujua hili basi, unakuwa umepata silaha ya kwanza muhimu ya kuondoka kwenye umasikini, ambayo ni kuhakikisha hutumii muda wako mwingi na masikini.

Hakikisha wale watu wa karibu kabisa kwako siyo masikini, hata kama bado hawajawa matajiri, basi wasiwe watu wanaovumilia umasikini, wawe watu wanaopambana kweli kweli kuondoka kwenye umasikini.

richvspoor6.jpg

Kwa upande wa tabia kuambikizwa, tafiti zinaonyesha tabia za watu wetu wa karibu huwa zinatuathiri moja kwa moja, hata kama watu hao wapo mbali.

Utafiti mkubwa kabisa uliowahi kufanywa wa kufuatilia maisha ya watu kwa muda mrefu (The Framingham study) umeonyesha kwamba unywaji, uvutaji na hata unene ni vitu vinavyoambukizwa.

Hiyo ina maana kwamba kama una rafiki ambaye ni mlevi, anavuta sigara au ni mnene unakuwa kwenye hatari ya wewe kuwa kama yeye.
Hata kama hukuwa na tabia hizo kabisa, kitendo cha kuwa na urafiki na mwenye tabia hizo, kinakuweka kwenye hatari kubwa ya kujenga tabia za aina hiyo pia.

Na hili siyo jipya kwenye maisha yako.
Unakumbuka ulipokuwa mtoto wakati wazazi wako wanakukataza usicheze au kuongozana na watoto wenye tabia mbaya?
Hawakuwa wanaona unafaidi sana, walijua, kupitia uzoefu kwamba haitachukua muda na wewe utakuwa na tabia kama zao.

Hivyo pia ndivyo ilivyo kwenye umasikini, ukiwa na rafiki masikini, unakuwa kwenye hatari kubwa ya wewe kuwa masikini pia.

Ni kwa sababu hiyo ndiyo maana nakushauri kama unataka kuondoka kwenye umasikini, hatua ya kwanza kwako kuchukua ni kuwaepuka masikini kama ukoma.

Rafiki, niweke hili wazi kwamba adui yetu mkubwa ni umasikini, na hivyo kuwaepuka masikini haimaanishi wao ni watu wabaya, ila tunajikinga wasituambukize umasikini wao.

Kama una ndugu yako ni mgonjwa wa ukimwi na ana kidonda, hutakigusa kwa mikono mitupu, lazima utavaa mipira ya kujikinga. Japo unampenda ndugu yako kweli, lakini kile alichonacho hukipendi, hivyo unajikinga nacho.

Na hilo ndiyo nataka ujifunze hapa, siyo uwadharau masikini, siyo uwabague na kuwanyanyapaa.

Badala yake uwaepuke, usitumie nao muda wako mwingi, usisikilize ushauri wao hasa kwenye mambo ya fedha.

Ni kwa njia hizo ndiyo unaweza kuepuka kuambukizwa umasikini ili mapambano unayoendesha dhidi ya umasikini yawe na tija.

Kitu kingine ambacho nimekuwa naksafani sana kwenye hii safari ya kuondoka kwenye umasikini ni hiki; njia bora ya kuwasaidia masikini ni kwa wewe kutokuwa masikini kama wao.

Kama ambavyo maelekezo ya kwenye ndege yanaeleza, inapotokea dharura, jipe kwanza hewa ya oksijeni ndiyo uweze kuwasaidia wengine hasa watoto.

Hivyo pia ndivyo ilivyo kwenye umasikini, huwezi kuwasaidia masikini huku na wewe ukiwa masikini.

Hivyo rafiki yangu, waepuke masikini ili utoke kwenye umasikini.
Na ukishatoka kwenye umasikini ndiyo utaweza kuwasaidia vizuri masikini hao.

Rafiki, kama bado hujaelewa namna bora ya kuwaepuka masikini, kuvunja tabia za kimasikini ulizojijengea na kujenga tabia mpya za kitajiri, nina habari njema kwako.

Habari njema ni kwamba kitabu cha TABIA ZA KITAJIRI, kitabu ambacho kinakupa mwongozo wa kuvunja tabia za kimasilini na kujenga tabia za kitajiri kipo tayari.

Hiki ni kitabu muhimu sana cha kusomwa na kila ambaye ameshachoshwa na laana ya umasikini na hataki tena kuendelea hivyo.

Kitabu hiki ni silaha imara ya kumshinda adui mkuu wa maisha yetu ambaye ni UMASIKINI.

Karibu sana usome kitabu hiki cha TABIA ZA KITAJIRI, ujifunze kwa kina na kuondoka na silaha muhimu ya kwenda kuivunja laana ya umasikini ambayo imekuandama maisha yako yote.

huwezi-kuwaridhisha313.png

JINSI YA KUPATA KITABU.
Kitabu cha TABIA ZA KITAJIRI kinapatikana kwa nakala ngumu (hardcopy) na nakala tete (softcopy).
Kama upo Dar es salaam utaletewa kitabu popote ulipo kwa hardcopy au kama utanunua softcopy utatumiwa kwa email.

Na kama upo nje ya Dar es salaam utatumiwa kitabu kule ulipo.
Kujipatia nakala yako ya kitabu cha TABIA ZA KITAJIRI, wasiliana na namba 0752 977 170 au 0678 977 007.

20220430_075702.jpg

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.
Mnataka kuwa matajiri, kwani hamkuambiwa ni vigumu tajiri kuuona ufalme wa mbinguni mithili ya ngamia kupenya kwenye tundu la sindano? 😂😂 Natania.
 
Nakubaliana nawewe 100% Suala la Utajiri linategemea na Mungu alivyokupangia Maisha yako yaweje.
Kuna watu wanaHustle litaa eg. MACHIMBON miaka pilikichi lakin mwingine anaaanza leo anapata Jiwe ananyanyuka kiuchumi vivo hivyo kwa Wakulima.
Wanalima kila mwaka lakin wakulima wachache sana wanaotoboa maisha.

Ila nimeona mdau anatupanga tununuwe kitabu chake Anasahau Mungu ndio kila kitu katk maisha.
Teh teh teh teh
Dk Makirita bado una kazi kama mitazamo ya watu ndio kama hii mmmh kuna safari ndefu bado ya watu kupata ufahamu wa Elimu ya Maisha na Mafanikio!
 
Masikini waliowengi huwa wanashauriana mambo ya kwenda kunywa pombe kutafuta Madanga na kuosha rungu, kudiskasi mambo ya Diamondi na Simba na Yanga.

Siku imeisha hiyo siku ya pili ni kulalamika kuwa Raisi demu hafai.
Sure kabisa yani.
 
Dk Makirita bado una kazi kama mitazamo ya watu ndio kama hii mmmh kuna safari ndefu bado ya watu kupata ufahamu wa Elimu ya Maisha na Mafanikio!
Acha tu mkuu,
Yaani hii kitu bado ni ngumu mno kwa watu.
Sasa naelewa kwa nini hii nchi inashindwa kupiga hatua licha ya kuwa na rasilimali.
Mitazamo ambayo watu wanayo ni ya hovyo sana.
 
Habari za sijui kuutafuta utajiri utazisikia sanasana kwenye nchi maskini kama Bongo. Ila nchi zilizoendelea ukiachana na Marekani (Nasemea hasa hasa nchi za Ulaya), huwezi kusikia hizi swagga za kutafuta utajiri maana system ya nchi yenyewe ipo katika hali ya kuwafanya watu wote waishi maisha karibia sawa. Kitakachomtofautisha mwenye pesa nyingi sana na mtu mwingine ni kuhusu tu makazi. Kwamba mtu mwenye pesa nyingi ataishi kwenye nyumba inayojitegemea na mtu wa kawaida anaishi kwenye apartments. Ila mambo mengine wapo sawa tu maana hakuna gap kubwa kati ya maskini na tajiri.

Unakuta wote wanapata mahitaji yao kwenye supermarket moja. Siyo kama Bongo wanaonunua mahitaji Mliman city ni wenye pesa zaidi. Unakuta pia Ulaya huduma za afya ni sawa kwa watu wote siyo kama Bongo mwenye pesa anapata matibabu Agakhan na makabwela wanaenda Mwananyamala. Elimu nchi nyingi za Ulaya ni bure na baadhi unalipia pesa kidogo kwa chuo kikuu. Siyo kama Bongo mwenye pesa anapeleka watoto wake Internanational school makabwela wanapeleka watoto wao Shule ya msingi Buza. Mahakama zinatenda haki kwa watu wote, siyo kama Bongo mwenye pesa anaweza kununua haki na kabwela akafungwa hata kwa ushahidi wa uongo.

Unakuta pia hata anayefanya kazi ya usafi analipwa mshahara unaomtosha kulipa bills zote kwa mwezi na kubakisha chenchi. Yaani mfanya usafi anaweza kusafiri hata kwa ndege siyyo kama bongo ili usafiri kwa ndege mpaka uwe tajiri. Sasa nchi kama hizi mtu anatafuta utajiri wa kazi gani? Hizi stori zipo tu nchi maskini.

Kwa kuhitimisha, mie huwa naona watu wanaohimiza sana watu kuwa matajiri wanataka tuendelee kuwa na mfumo wa kutengeneza nchi ya wenye nacho na wasio nacho hivyo kuendelea kumkandamiza mtu maskini. Any way... Ngoja niishie hapa kwanza kwa sasa..
 
Kuna ukweli ila kuna mdau kagisia happ mtaji wa tajiri ni haohao maskini. Labda mfanye mtaji na si rafiki.
 
Tuhimizane;
1) Kufanya kazi kwa bidii na kuacha uvivu maana ka-nchi ketu bado kana shida nyingi za huduma za kijamii
2) Tuwahimize viongozi kuweka sera za usawa kwa watu wote katika nyanja za kijamii, kisiasa na kiuchumi
3) Watu wenye vipaji wavitumie vipaji vyao ili kuifanya dunia (nchi) yetu kuwa sehemu nzuri ya kuishi muda huu mfupi tuliokopeshwa kuishi hapa Duniani (miaka yenyewe michache tu 60-80 years).

Haya mambo ya kulishana upepo wa kupeana hamasa za kuutafuta utajiri hapa Duniani ni kulishana upepo ambao hauna manufaa yoyote. Tunawajengea watu nadharia vichwani kwamba kuutafuta utajiri ndio mambo yote kwenye maisha hali inayopelekea vijana kutafuta utajiri kwa njia ambazo pengine hazina mchango mkubwa kwenye uchumi wa nchi mfano betting na mambo mengine yanayofanana na hayo.

Kingine ni kuwa, hizi hamasa za kuwafanya watu wapate hisia za kuutafuta utajiri kunawafanya watu wapate stress na depression kwenye maisha pale wanapoona hawawezi kutimiza hizo hisia za kuwa tajiri.

Focus isiwe kuwafanya watu waone utajiri wa mapesa mengi ndio ufahari wa maisha. Tuzingatie point 3 hapo juu kama nilivyoandika.

NB: Mtoa mada; unaweza kuniambia kwa nchi zilizoendelea siku nyingi kama Sweden, Finland, Denamarak, Netherlands zina mabilionea wangapi ukilinganisha na idadi nyingine ya watu? Mana tulitegemea kwakuwa wao wameanza kusoma vitabu tangia zamani na wamefanikiwa tangia zamani basi kungekuwa na Mabilionea wengi zaidi kuliko watu wengine wa kawaida kama hiki mnachotueleza kwenye hivyo vitabu vya motivation vya wafanyabiashara wa vitabu wa huko Marekani ni kweli.

Naomba ulete takwimu za Mabilionea wa hizo nchi nilizozitaja tuone graph ikoje. Angalau onesha kuanzia miaka 50 huko nyuma tuone trend ilivyo.
 
Nimesoma vizuri lakini nikaona mwenye biashara ya kitabu yeye mwenyew ajani shauri bado sana tajiri sio dalali
 
Mkuu kwanza mtoa mada hataki kuelezea nini maana ya utajiri kwa mujibu wake na kitabu..

Pengine utajiri anaokusudia yeye ni kuwa na uwezo wa kufikiri na wewe unagusia utajiri wa mapesa.

Pengine utajiri anaogusia mtoa mada ni uwezo wa kutongoza mademu wengi lakini wewe unagusia utajiri wa pesa nyingi.

Pengine utajiri anaokusudia mtoa mada ni kuwa na vitabu vingi vya kiswahili vilivyoandikwa na makirita amani kumbe wewe unakusudia utajiri wa mapesa mengi.
 
Matajiri wengi wazinzi tu ..hamna lolote hapo. Hiyo ni biashara ya kitabu unafanya. Utajiri ni Neema ya Mungu tu. Kuna wenye juhudi nyingi za kuupata lakini wameambulia hasara tu.
Ha ha haa. Kutafuta utajiri ni nadharia zilizowekwa vizuri kwenye maandishi ya wauza vitabu wa Marekani. Vitabu vingi vinavyoelezea mambo ya utajiri vimeandikwa huko Marekani.

Ila Ulaya hizi habari huwezi kuzisikia kiviiile. Watu wa Ulaya hawana makuu na purukushani nyingi za kutafuta hela. Wanaangalia ni jinsi gani wanaweza kumudu bills za mwezi basi.

Masuala sijui ya kuwa Bilionea utayasikia kwenye nchi maskini kama Bongo. Tupambane kuhimizana kufanya kazi kwa bidii kila mtu kwa nafasi yake ili Serikali ikusanye kodi na kuimarisha huduma za kijamii. Vilevile tupaze sauti Serikali iweke mazingira ya usawa katika huduma za kijamii, kiuchumi na kisiasa. Haya mambo ya kutafuta utajiri ni kulishana upepo tu.
 
Matajiri wengi wazinzi tu ..hamna lolote hapo. Hiyo ni biashara ya kitabu unafanya. Utajiri ni Neema ya Mungu tu. Kuna wenye juhudi nyingi za kuupata lakini wameambulia hasara tu.

Hao wanaoutafuta utajiri bila kuupata hawatumii njia sahihi,unatakiwa ufanye vitu vya tofauti(unique) na sisi wabongo kinachotuponza ni ubishi usio na maana,
 
Matajiri wengi wazinzi tu ..hamna lolote hapo. Hiyo ni biashara ya kitabu unafanya. Utajiri ni Neema ya Mungu tu. Kuna wenye juhudi nyingi za kuupata lakini wameambulia hasara tu.

Mtu anapewa fursa itakayompa kesho yake halafu anakuwa mbishi then anaenda kuwauliza walioshindwa ili wampe ushauri ,unafikiri mtu aliyeshindwa atakushauri nin?mim nilikuwa maskin sana nalala njaa na familia yangu lakin baada ya kufanya maamuz angalau nimetoboa naweza kuingiza dola 6000 kwa wiki
 
Na ndefu ndiyo inayodumu.
Mchicha unaota ndani ya siku 3, hauwezi kudumu hata mwaka.
Mbuyu unaota miaka 7, unadumu mpaka miaka 100.
Hivyo tuweke nguvu zetu kwenye vitu vitakavyodumu.

Kweli kabisa wabongo wengi wanapenda kitonga
 
Kitecho cha kwenda kwenye kijiwe cha pombe na kuwaambiwa wanywaji waache kabisa tabia ya kunywa pombe tena waepuke walevi sio watu wazuri......hakuna mlevi atakayekupenda.......

hapa jf wengi ni watu wa maisha ya chini ambao mtu yeyote ambae atafundisha somo la kuhusu ishu ya uchumi lazima wajue kuhusu level ya maisha yake!

ona comments zao[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Habari za sijui kuutafuta utajiri utazisikia sanasana kwenye nchi maskini kama Bongo. Ila nchi zilizoendelea ukiachana na Marekani (Nasemea hasa hasa nchi za Ulaya), huwezi kusikia hizi swagga za kutafuta utajiri maana system ya nchi yenyewe ipo katika hali ya kuwafanya watu wote waishi maisha karibia sawa. Kitakachomtofautisha mwenye pesa nyingi sana na mtu mwingine ni kuhusu tu makazi. Kwamba mtu mwenye pesa nyingi ataishi kwenye nyumba inayojitegemea na mtu wa kawaida anaishi kwenye apartments. Ila mambo mengine wapo sawa tu maana hakuna gap kubwa kati ya maskini na tajiri.

Unakuta wote wanapata mahitaji yao kwenye supermarket moja. Siyo kama Bongo wanaonunua mahitaji Mliman city ni wenye pesa zaidi. Unakuta pia Ulaya huduma za afya ni sawa kwa watu wote siyo kama Bongo mwenye pesa anapata matibabu Agakhan na makabwela wanaenda Mwananyamala. Elimu nchi nyingi za Ulaya ni bure na baadhi unalipia pesa kidogo kwa chuo kikuu. Siyo kama Bongo mwenye pesa anapeleka watoto wake Internanational school makabwela wanapeleka watoto wao Shule ya msingi Buza. Mahakama zinatenda haki kwa watu wote, siyo kama Bongo mwenye pesa anaweza kununua haki na kabwela akafungwa hata kwa ushahidi wa uongo.

Unakuta pia hata anayefanya kazi ya usafi analipwa mshahara unaomtosha kulipa bills zote kwa mwezi na kubakisha chenchi. Yaani mfanya usafi anaweza kusafiri hata kwa ndege siyyo kama bongo ili usafiri kwa ndege mpaka uwe tajiri. Sasa nchi kama hizi mtu anatafuta utajiri wa kazi gani? Hizi stori zipo tu nchi maskini.

Kwa kuhitimisha, mie huwa naona watu wanaohimiza sana watu kuwa matajiri wanataka tuendelee kuwa na mfumo wa kutengeneza nchi ya wenye nacho na wasio nacho hivyo kuendelea kumkandamiza mtu maskini. Any way... Ngoja niishie hapa kwanza kwa sasa..
una akili sana bro
 
Back
Top Bottom