Mkuu,
Nashukuru kwa kunielimisha. Mimi siyo mtaalamu wa uchumi na wala sifahamu kila kitu. Ndio maana niliomba taarifa kwako. Machache niliyoyaeleza ni kutokana na ufahamu wangu mdogo wa kujifunza kwa kuunga unga tu mitandaoni.
Kwakuwa wewe ni msomaji, bila shaka utakubaliana nami kuwa mtu huelezea kitu kutokana na ukomo wa ufahamu wake. Kwahiyo mambo yaliyo juu ya ufahamu wangu siwezi kuyaelezea kwa usahihi wake.
Kama mfumo wa kibepari wa Marekani ndio unaona ni sahihi zaidi kuliko mfumo wa kiuchumi wa nchi za Ulaya ambao ni 'hybrid economic system (half capitalisms, half socialism) basi naomba niendelee kujifunza zaidi huenda nikawa na ufahamu mzuri kama ulivyo wewe na nikabadilika huko mbeleni.
Hata hivyo, kwa ufahamu wangu wa sasa, nitaendelea kuamini kuwa mfumo huu wa Ulaya ndio mzuri zaidi maana unaondoa social inequalities kwenye jamii. Ya kwamba, pesa zimilikiwe na watu wengi kuliko kumilikiwa na watu wachache kwenye jamii. Ikitokea wamekuwepo mabilionea basi iwe ni natural na siyo kwamba ndio iwe focus ya jamii nzima. Ikumbukwe, kuondoa social inequalities ni agenda mojawapo ya kudumu ya Umoja wa Mataifa. Kwa maoni yangu, na kwa ufahamu wangu mdogo nilionao, ubepari kamili unachangia kwa kiasi kikubwa social inequalities. Nifahamike kuwa simanishi turejee kwenye sera za ujamaa za Mwl Nyerere. Tuwe nusu ubebari, na nusu ujamaa kama ilivyo nchi nyingi za Ulaya.
Ila ngoja niendelee kujifunza na huenda nikabadilika na mie nikaanza kufata principles za kuutafuta utajiri kama unavyotuhimiza. Japokuwa inahitajika nguvu kubwa zaidi kubadilika maana mie sio muumini mzuri wa ubinafsi. Kidogo nachopata nagawana na wachache wenye shida zaidi ili kwenda nao sawa. Kitu ambacho ni kinyume na principlkes za kutafuta utajiri maana kwenye kutafuta utajiri inabidi uwe mbinafsi zaidi, na uwanyonye watu wengine ili wewe uendelee kuinuka juu. Mfano: Kama umeajiri watu uhakikishe unawabana kisawasawa ikibidi uwalipe mishahara ya kinyonyaji ili upunguze operational cosst na ku-maximize profit ili uwe bilionea. Hizi ni sifa mojawapo za kuelekea kwenye ubilionea. Huenda nikawa sipo sahihi pia kwa haya nayosema. Nipo tayari kuendelea kujifunza. Ahsante sana.
Mkuu,
Tuendelee kujifunza, hakuna awezaye kujua kila kitu.
Na kwa mijadala ya aina hii inatufungua tufikiri zaidi.
Tukirudi kwenye hii mifumo ya kiuchumi, hakuna mfumo mmoja ambao ni bora kabisa na usio na mapungufu.
Lakini sasa ukilinganisha mifumo yote ambayo imewahi kujaribiwa hapa duniani, angalau ubepari una nafuu ukilinganisha na hiyo mingine.
Siyo kwamba ni perfect, lakini angalau unafanya mambo yaende.
Na siyo ubepari wa ubeberu, bali ubepari ambao unadhibitiwa kwa misingi sahihi.
Tukirudi kwa hoja ya ulaya, kikubwa nachokiona kwao ni ustaarabu.
Wenzetu wamestaarabika sana kiasi kwamba mtu anajua wajibu wake na kutekeleza na anajali maslahi ya wengine.
Ndiyo maana hybrid inafanya kazi kwao, social services ziko accessible kwa wote.
Na hayo ni matokeo ya uwekezaji ambao tayari ulishafanyika miaka mingi iliyopita.
Kwa sisi kwa kiwango cha ustaarabu tulichonacho, inabidi tukimbizane kwanza.
Ona hata demokrasia tu inavyotusumbua, tatizo ni moja, hatujafikia ustaarabu wa kutosha kuamini katika demokrasia.
Tenga muda usome vitabu viwili nilivyoshirikisha hapa kisha tutaendelea kujadiliana hili kwa kina zaidi.