Kama unataka kuondoka kwenye umasikini, waepuke masikini kama ukoma

Kama unataka kuondoka kwenye umasikini, waepuke masikini kama ukoma

Mtu anapewa fursa itakayompa kesho yake halafu anakuwa mbishi then anaenda kuwauliza walioshindwa ili wampe ushauri ,unafikiri mtu aliyeshindwa atakushauri nin?mim nilikuwa maskin sana nalala njaa na familia yangu lakin baada ya kufanya maamuz angalau nimetoboa naweza kuingiza dola 6000 kwa wiki
shida ni kua kitabu kinaandikwa ulaya kinatafasiliwa bongo ambao mifumo ya nchi haimruhusu kabisa mtu kufanya hayo
 
Rafiki yangu mpendwa,

Hivi unajua ya kwamba umasikini huwa unaambukizwa kama magonjwa yanayoambukizwa?

Ndiyo, hiyo ni kweli kabisa, pale unapokaa na masikini, wanakusababisha uendelee kubaki kwenye umasikini.

Huenda kwa kusoma sentensi hizo chache umejisikia vibaya, umenichukulia mbaguzi na mwenye dharau.

Sitakushangaa kwa hilo, kwani hata mimi wakati najifunza hili kwa mara ya kwanza sikulielewa haraka.
Ni mpaka pale niliposoma tafiti baada ya tafiti kwenye nguvu ya wale wanaotuzunguka na jinsi tabia inavyoweza kuambukizwa.

Kuhusu nguvu ya wanaokuzunguka, Jim Rhon alikuwa akinukuliwa mara kwa mara akisema vile ulivyo ni wastani wa watu watano unaotumia nao muda wako mwingi.

Hili unaweza kulithibitisha wewe mwenyewe, bila hata ya kutumia nguvu sana.
Yaangalie maisha yako, kisha angalia maisha ya marafiki zako wa karibu.
Angalia wana watoto wangapi, wana magari ya aiba gani, wana nyumba au wanakaa maeneo gani, kazi na/au biashara wanazofanya.

Utashangaa jinsi ambavyo mna ufanano mkubwa.
Je unadhani hilo limetokea tu kama ajali?

Hapana, kuna nguvu kubwa sana inayofanya kazi, nguvu inayohakikisha hutofautiani sana na wale unaotumia nao muda wako mwingi.

Kwa kujua hili basi, unakuwa umepata silaha ya kwanza muhimu ya kuondoka kwenye umasikini, ambayo ni kuhakikisha hutumii muda wako mwingi na masikini.

Hakikisha wale watu wa karibu kabisa kwako siyo masikini, hata kama bado hawajawa matajiri, basi wasiwe watu wanaovumilia umasikini, wawe watu wanaopambana kweli kweli kuondoka kwenye umasikini.


richvspoor6.jpg


Kwa upande wa tabia kuambikizwa, tafiti zinaonyesha tabia za watu wetu wa karibu huwa zinatuathiri moja kwa moja, hata kama watu hao wapo mbali.

Utafiti mkubwa kabisa uliowahi kufanywa wa kufuatilia maisha ya watu kwa muda mrefu (The Framingham study) umeonyesha kwamba unywaji, uvutaji na hata unene ni vitu vinavyoambukizwa.

Hiyo ina maana kwamba kama una rafiki ambaye ni mlevi, anavuta sigara au ni mnene unakuwa kwenye hatari ya wewe kuwa kama yeye.
Hata kama hukuwa na tabia hizo kabisa, kitendo cha kuwa na urafiki na mwenye tabia hizo, kinakuweka kwenye hatari kubwa ya kujenga tabia za aina hiyo pia.

Na hili siyo jipya kwenye maisha yako.
Unakumbuka ulipokuwa mtoto wakati wazazi wako wanakukataza usicheze au kuongozana na watoto wenye tabia mbaya?
Hawakuwa wanaona unafaidi sana, walijua, kupitia uzoefu kwamba haitachukua muda na wewe utakuwa na tabia kama zao.

Hivyo pia ndivyo ilivyo kwenye umasikini, ukiwa na rafiki masikini, unakuwa kwenye hatari kubwa ya wewe kuwa masikini pia.

Ni kwa sababu hiyo ndiyo maana nakushauri kama unataka kuondoka kwenye umasikini, hatua ya kwanza kwako kuchukua ni kuwaepuka masikini kama ukoma.

Rafiki, niweke hili wazi kwamba adui yetu mkubwa ni umasikini, na hivyo kuwaepuka masikini haimaanishi wao ni watu wabaya, ila tunajikinga wasituambukize umasikini wao.

Kama una ndugu yako ni mgonjwa wa ukimwi na ana kidonda, hutakigusa kwa mikono mitupu, lazima utavaa mipira ya kujikinga. Japo unampenda ndugu yako kweli, lakini kile alichonacho hukipendi, hivyo unajikinga nacho.

Na hilo ndiyo nataka ujifunze hapa, siyo uwadharau masikini, siyo uwabague na kuwanyanyapaa.

Badala yake uwaepuke, usitumie nao muda wako mwingi, usisikilize ushauri wao hasa kwenye mambo ya fedha.

Ni kwa njia hizo ndiyo unaweza kuepuka kuambukizwa umasikini ili mapambano unayoendesha dhidi ya umasikini yawe na tija.

Kitu kingine ambacho nimekuwa naksafani sana kwenye hii safari ya kuondoka kwenye umasikini ni hiki; njia bora ya kuwasaidia masikini ni kwa wewe kutokuwa masikini kama wao.

Kama ambavyo maelekezo ya kwenye ndege yanaeleza, inapotokea dharura, jipe kwanza hewa ya oksijeni ndiyo uweze kuwasaidia wengine hasa watoto.

Hivyo pia ndivyo ilivyo kwenye umasikini, huwezi kuwasaidia masikini huku na wewe ukiwa masikini.

Hivyo rafiki yangu, waepuke masikini ili utoke kwenye umasikini.
Na ukishatoka kwenye umasikini ndiyo utaweza kuwasaidia vizuri masikini hao.

Rafiki, kama bado hujaelewa namna bora ya kuwaepuka masikini, kuvunja tabia za kimasikini ulizojijengea na kujenga tabia mpya za kitajiri, nina habari njema kwako.

Habari njema ni kwamba kitabu cha TABIA ZA KITAJIRI, kitabu ambacho kinakupa mwongozo wa kuvunja tabia za kimasilini na kujenga tabia za kitajiri kipo tayari.

Hiki ni kitabu muhimu sana cha kusomwa na kila ambaye ameshachoshwa na laana ya umasikini na hataki tena kuendelea hivyo.

Kitabu hiki ni silaha imara ya kumshinda adui mkuu wa maisha yetu ambaye ni UMASIKINI.

Karibu sana usome kitabu hiki cha TABIA ZA KITAJIRI, ujifunze kwa kina na kuondoka na silaha muhimu ya kwenda kuivunja laana ya umasikini ambayo imekuandama maisha yako yote.


huwezi-kuwaridhisha313.png


JINSI YA KUPATA KITABU.
Kitabu cha TABIA ZA KITAJIRI kinapatikana kwa nakala ngumu (hardcopy) na nakala tete (softcopy).
Kama upo Dar es salaam utaletewa kitabu popote ulipo kwa hardcopy au kama utanunua softcopy utatumiwa kwa email.

Na kama upo nje ya Dar es salaam utatumiwa kitabu kule ulipo.
Kujipatia nakala yako ya kitabu cha TABIA ZA KITAJIRI, wasiliana na namba 0752 977 170 au 0678 977 007.


20220430_075702.jpg


Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.
Yaani dah watu wengine sijui wakoje eti anatuuzia kitabu cha jinsi mbinu ya kuwa tajiri lakini yeye sio tajiri
 
Matajiri wengi wazinzi tu ..hamna lolote hapo. Hiyo ni biashara ya kitabu unafanya. Utajiri ni Neema ya Mungu tu. Kuna wenye juhudi nyingi za kuupata lakini wameambulia hasara tu.
Kama ni Neema ya mungu na wewe muombe mungu uwe billionea.

Tafuta helA upunguze stress
 
Nachojua ktk Ulimwengu wa Roho. Wachawi wa mtaa au kijiji usiku Saa sita kamili wachawi baada ya kupigwa filimbi ya kichawi ukitana kijiweni kwao then kabla awajanza kuwanga huwa wanazunguka njia au barabara zote za kijiji au mtaa huku wakitamka na kuwanenea laana ya umasikini, magonjwa,na dhiki za KILA aina wakaazi wote wa mtaa au kijiji husika, wakimaliza ndipo uruka kuwanga na wakirudi ufanya hivyo hivyo kupiga laana kwa watu waliolala then ndipo utawanyika. So mtu yeyeto kuanzia aflajiri atakaekanyaga au tumia barabara hizo zile laaana zitamvaa kama hana nguvu nyingine ya ziada au usaidizi mwingine, thus unakuta mtaa au kijiji wote level moja ya maisha ya dhiki kama umasikini ni wote, nyumba chakavu wote, Hakuna anaefaulu iwe elimu, maisha wote level sawa, unakuta mtaa mzima hakuna hata mwenye kumudu kuweka taa nje.
Ukiona ufanikiwi mtaa fulani au eneo fulani kama huna nguvu ya ziada au usaidizi, ushauri hama. Laana ndio uleta tabia na tabia ndio uzaa umasikini. Na umasikini ndio chanzo cha mambo yote maovu.
Noma sana!
 
Ukikaa na watu masikini utavutwa kwenye umasikini hivyo hivyo ukikaa na matajiri. Umasikini ni roho ya laana za ukoo ambazo Kazi yake kuu ni kufunga akili.
 
Ufukara ni moja ya Adui aliyezishinda Serikali karibu zote za Kiafrika.

Sijui kama tutamuweza Adui huyu
Wanashindwa kwa interest zao za kisiasa.
Wanawafanya wengi wawe masikini Ili wawatawale. Pia ni nature kwa maana hakuna mwafrika anaeweza mletea maendeleo mwafrika mwenzake. Pia waafrika hawana uwezo wa kuongoza Jamii ikastawi.
 
Urope ime
Habari za sijui kuutafuta utajiri utazisikia sanasana kwenye nchi maskini kama Bongo. Ila nchi zilizoendelea ukiachana na Marekani (Nasemea hasa hasa nchi za Ulaya), huwezi kusikia hizi swagga za kutafuta utajiri maana system ya nchi yenyewe ipo katika hali ya kuwafanya watu wote waishi maisha karibia sawa. Kitakachomtofautisha mwenye pesa nyingi sana na mtu mwingine ni kuhusu tu makazi. Kwamba mtu mwenye pesa nyingi ataishi kwenye nyumba inayojitegemea na mtu wa kawaida anaishi kwenye apartments. Ila mambo mengine wapo sawa tu maana hakuna gap kubwa kati ya maskini na tajiri.

Unakuta wote wanapata mahitaji yao kwenye supermarket moja. Siyo kama Bongo wanaonunua mahitaji Mliman city ni wenye pesa zaidi. Unakuta pia Ulaya huduma za afya ni sawa kwa watu wote siyo kama Bongo mwenye pesa anapata matibabu Agakhan na makabwela wanaenda Mwananyamala. Elimu nchi nyingi za Ulaya ni bure na baadhi unalipia pesa kidogo kwa chuo kikuu. Siyo kama Bongo mwenye pesa anapeleka watoto wake Internanational school makabwela wanapeleka watoto wao Shule ya msingi Buza. Mahakama zinatenda haki kwa watu wote, siyo kama Bongo mwenye pesa anaweza kununua haki na kabwela akafungwa hata kwa ushahidi wa uongo.

Unakuta pia hata anayefanya kazi ya usafi analipwa mshahara unaomtosha kulipa bills zote kwa mwezi na kubakisha chenchi. Yaani mfanya usafi anaweza kusafiri hata kwa ndege siyyo kama bongo ili usafiri kwa ndege mpaka uwe tajiri. Sasa nchi kama hizi mtu anatafuta utajiri wa kazi gani? Hizi stori zipo tu nchi maskini.

Kwa kuhitimisha, mie huwa naona watu wanaohimiza sana watu kuwa matajiri wanataka tuendelee kuwa na mfumo wa kutengeneza nchi ya wenye nacho na wasio nacho hivyo kuendelea kumkandamiza mtu maskini. Any way... Ngoja niishie hapa kwanza kwa sasa..
Urope imelala,
Urope ipo stagnant,
Wale zama zao zilishapita.
Ndiyo maana innovations zote sasa zinatokea US.
Hatuwezi kujilinganisha na Europe.
Sisi bado tupo kwenye hustling stage.
 
Tuhimizane;
1) Kufanya kazi kwa bidii na kuacha uvivu maana ka-nchi ketu bado kana shida nyingi za huduma za kijamii
2) Tuwahimize viongozi kuweka sera za usawa kwa watu wote katika nyanja za kijamii, kisiasa na kiuchumi
3) Watu wenye vipaji wavitumie vipaji vyao ili kuifanya dunia (nchi) yetu kuwa sehemu nzuri ya kuishi muda huu mfupi tuliokopeshwa kuishi hapa Duniani (miaka yenyewe michache tu 60-80 years).

Haya mambo ya kulishana upepo wa kupeana hamasa za kuutafuta utajiri hapa Duniani ni kulishana upepo ambao hauna manufaa yoyote. Tunawajengea watu nadharia vichwani kwamba kuutafuta utajiri ndio mambo yote kwenye maisha hali inayopelekea vijana kutafuta utajiri kwa njia ambazo pengine hazina mchango mkubwa kwenye uchumi wa nchi mfano betting na mambo mengine yanayofanana na hayo.

Kingine ni kuwa, hizi hamasa za kuwafanya watu wapate hisia za kuutafuta utajiri kunawafanya watu wapate stress na depression kwenye maisha pale wanapoona hawawezi kutimiza hizo hisia za kuwa tajiri.

Focus isiwe kuwafanya watu waone utajiri wa mapesa mengi ndio ufahari wa maisha. Tuzingatie point 3 hapo juu kama nilivyoandika.

NB: Mtoa mada; unaweza kuniambia kwa nchi zilizoendelea siku nyingi kama Sweden, Finland, Denamarak, Netherlands zina mabilionea wangapi ukilinganisha na idadi nyingine ya watu? Mana tulitegemea kwakuwa wao wameanza kusoma vitabu tangia zamani na wamefanikiwa tangia zamani basi kungekuwa na Mabilionea wengi zaidi kuliko watu wengine wa kawaida kama hiki mnachotueleza kwenye hivyo vitabu vya motivation vya wafanyabiashara wa vitabu wa huko Marekani ni kweli.

Naomba ulete takwimu za Mabilionea wa hizo nchi nilizozitaja tuone graph ikoje. Angalau onesha kuanzia miaka 50 huko nyuma tuone trend ilivyo.
Msiweke nchi yoyote ya Europe kwenye hizi comparisons zenu.
Watu tunaweza kujipima nao ni Asia, kama China, Korea na wengine.
Ambao tulianzia pamoja miaka siyo mingi.
Unajilinganisha na nchi ambazo wakati babu zetu wanavaa ngozi wao tayari walikuwa na viwanda vya nguo?
Hamuwezi kuwa serious.
Angalieni hatua ambazo China inapiga, pamoja na mapungufu yake mengi, bado inapiga hatua kubwa.
Ndiyo tunapaswa kukaa huko.
 
Mkuu kwanza mtoa mada hataki kuelezea nini maana ya utajiri kwa mujibu wake na kitabu..

Pengine utajiri anaokusudia yeye ni kuwa na uwezo wa kufikiri na wewe unagusia utajiri wa mapesa.

Pengine utajiri anaogusia mtoa mada ni uwezo wa kutongoza mademu wengi lakini wewe unagusia utajiri wa pesa nyingi.

Pengine utajiri anaokusudia mtoa mada ni kuwa na vitabu vingi vya kiswahili vilivyoandikwa na makirita amani kumbe wewe unakusudia utajiri wa mapesa mengi.
Mkuu, mbona una mawazo mgando sana.
Unashindwa kuelewa mambo madogo hivi huo utajiri utauweza kweli?
Tumeshajadiliana na kumaliza lako, lakini bado una nyongo tu.
Get a life mkuu, utakufa siku siyo zako.
And by the way, Get Money, #NothingElseMatters
 
shida ni kua kitabu kinaandikwa ulaya kinatafasiliwa bongo ambao mifumo ya nchi haimruhusu kabisa mtu kufanya hayo
Mbona suti inavaliwa ulaya na bongo mnavaa.
Mbona burger zinaliwa Marekani na hapa bongo mnakula?
Mengine yote ya wezekane ila kwenye fedha ndiyo ishindikane?
Huu ndiyo ujinga unawafanya wengi kubaki kwenye umasikini.
Soma kitabu uvue huu ujinga.
 
Yaani dah watu wengine sijui wakoje eti anatuuzia kitabu cha jinsi mbinu ya kuwa tajiri lakini yeye sio tajiri
Kama padri anavyofundisha na kufungisha ndoa wakati yeye hana ndoa.
Unaionaje hiyo?
 
Mkuu, mbona una mawazo mgando sana.
Unashindwa kuelewa mambo madogo hivi huo utajiri utauweza kweli?
Tumeshajadiliana na kumaliza lako, lakini bado una nyongo tu.
Get a life mkuu, utakufa siku siyo zako.
And by the way, Get Money, #NothingElseMatters
Mkuu mimi na wewe tumeshamalizana.

Huonekani kama mtu mstaarabu wa kupokea mawazo tofauti badala yake unakuwa mtu wa misimamo ya hasira na kuamini kila anayekuhoji analengo la kukukwamisha,
hizo ni mindset za kimasikini sana ambazo unatuonesha hapa.

Wewe mwenyewe unaonekana una uchungu na hasira ya pesa ndio maana hutaki kuhojiwa kuhusu kitabu.

Na wewe endelea kutafuta pesa utaacha kuwasumbua watu kuhusu kununua kitabu.

Matajiri akina modewji hawalazimishi watu kununua bidhaa zao kama unavyofanya wewe hapa.
 
Urope ime

Urope imelala,
Urope ipo stagnant,
Wale zama zao zilishapita.
Ndiyo maana innovations zote sasa zinatokea US.
Hatuwezi kujilinganisha na Europe.
Sisi bado tupo kwenye hustling stage.
Wewe kwakuwa ni msomaji najua utakuwa ni mfuatiliaji pia wa mambo mengi ya kidunia. Unamfahamu Senator mmoja wa US anaitwa Bernie Sanders? Unafahamu itikadi za siasa zake za US? Jaribu kumfuatilia vizuri siasa zake na maandishi yake juu ya Siasa za US na maono yake anavyolinganisha mfumo wa uchumi wa US na ule wa nchi za Ulaya.

Fuatilia pia comments kwenye pages zake kwenye social media uone maoni ya watu wa kawaida wa Marekani tofauti na Matajiri wachache wanaomiliki uchumi wa Marekani. Uwe unatembelea pia mtandao wa Quora kujifunza watu wengine Duaniani wana maono yapi kuhusu uchumi wa nchi za Ulaya na ule wa Marekani. Mwisho kabisa fuatilia mwenendo wa SIASA za chama cha Democrat uone maono yao juu ya uchumi wa Marekani.
 
Urope ime

Urope imelala,
Urope ipo stagnant,
Wale zama zao zilishapita.
Ndiyo maana innovations zote sasa zinatokea US.
Hatuwezi kujilinganisha na Europe. Sisi bado tupo kwenye hustling stage

Nimewahi kusoma andiko lako huko nyuma unasema una maono ya kuwa Rais wa nchi yetu siku moja. Kama haya ndio maono yako kuhusu uchumi wa nchi yetu basi tuna changamoto kubwa kama Taifa. Mie nakuomba uendelee kujifunza zaidi hasa katika nchi za wenzetu waliotangulia. Uone walianza vipi, wako wapi sasa na wanamaono ya kufika wapi hapo baadae. Ujifunze changamoto wanazopitia na u-digest hizo changamoto kwa kuonesha namna gani sisi tunaweza kuepuka hizo changamoto katika safari yetu. Usiwe mbaguzi wa kujifunza , usiegemee kusoma vitabu vya motivation speakers wa Marekani peke yake. Soma na makala nyingine ikiwemo mtandao kama Quora uone maoni ya watu wengine walio wasomi na wananchi wa kawaida Duniani.
 
Hakika, tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...

Masikini nae mtu hata kama hana kitu...
 
Msiweke nchi yoyote ya Europe kwenye hizi comparisons zenu.
Watu tunaweza kujipima nao ni Asia, kama China, Korea na wengine.
Ambao tulianzia pamoja miaka siyo mingi.
Unajilinganisha na nchi ambazo wakati babu zetu wanavaa ngozi wao tayari walikuwa na viwanda vya nguo?
Hamuwezi kuwa serious.
Angalieni hatua ambazo China inapiga, pamoja na mapungufu yake mengi, bado inapiga hatua kubwa.
Ndiyo tunapaswa kukaa huko.
CHINA inapiga hatua kwa kuhamasisha watu wake wawe Mabilionea kama unavyotaka kutushawishi na sisi ?

Wewe kama msomaji wa vitabu uliyebobea, Je, unadhani focus ya sasa ya nchi yetu iwe kuwahamasisha watu kutafuta utajiri au watu wafanye kazi kwa bidii na kulipa kodi kisha Serikali kutumia vizuri hizo kodi kuboresha huduma za kijamii?

Je, kwenye huko kusoma kwako, umewahi kujiuliza kwanini nchi nyingi zinazoongoza kwa watu wake kuwa na furaha duniani ni nchi za Ulaya na siyo Marekani?

Kwa misingi hiyo, Je, ungependa nchi zipi ziwe role model wetu?

Nakuomba ufafanue na sisi wavivu wa kusoma vitabu tujifunze kupitia hapa JF.
 
Utajiri unapatikana kwa kununua vitabu vya Makirita Amani
Nunueni vitabu kwa wingi ili mumsaidie Makirita Amani kua tajiri zaidi na apate kutunanga zaidi sisi masikini [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom