Kama unataka kuondoka kwenye umasikini, waepuke masikini kama ukoma

Usijikite na vitabu vya utajiri tu,jikite na viitabu vya saikolojia pia.

Una tatizo la kisaikolojia la kumskasirikia kila anayeenda against na wewe,hiyo ni tatizo waone wanasaikolojia.
πŸ˜‚πŸ˜‚
Ghafla umekuwa mwanasaikolojia wa kunidiagnose na kunishauri?
Watanzania mnapenda sana kukimbilia mambo yaliyo kabisa nje ya uwezo wenu.
Anyway, get money, #NothingElseMatters
 
Bernie Sanders ni socialist, anajipambanua hilo wazi kabisa.
Mfumo wa kisoshalisti ulishafeli, hauwezi kuleta matokeo yoyote mazuri.
Democrats ndiyo kabisa wanapumulia mashine na hizo itikadi zao za kishoshalisti, 2024 hawatoboi.
 
Mkuu,
Nashukuru kwa kuwa msomaji wangu kwa muda mrefu.
Kuhusu urahisi hilo sina shaka nalo, nitakuwa raisi wa Tanzania.
Na kuhusu mfumo bora wenye kuleta maendeleo japo una changamoto zake, siyo ujamaa wala ukomunisti, bali ubepari unaosimamiwa vizuri.
Mimi siyo msomaji wa vitabu vya motivations tu, nasona vitabu vya historia, uchumi, biashara, siasa n.k.
Kama unaweza, soma kitabu kinachoitwa Seeing like a state uone jinsi mwandishi amechambua Nyerere alivyoshindwa kwenye vijiji vya ujamaa kwa kuadopt ideology ambayo haikuwa sahihi kwa stage yetu ya maendeleo.
 
Mkuu,
Ulivyokuwa unapambanua hoja hapa ulikuwa unanifurahisha, nikaona napata challenge ya kweli ili tufikiri zaidi.
Ila haya maswali yako hapa yamenishtua, yaani hujui vitu basic hivyo?
1. China ndiyo ya pili kwa kuwa na mabilionea wengi duniani.
2. Kwani mtu akafanya kazi kwa juhudi kubwa, akatoa thamani kubwa kwa watu, akaajiri wengi na akawa bilionea, kuna tatizo gani hapo?
Yaani kwako kufanya kazi kwa juhudi sawa, ila kuwa bilionea siyo sawa?
Hapo unanishangaza.


 
Mkuu,
Ulaya itoe kwenye equation yako kabisa,
Wale walishastaarabika zamani sana.
Wale wapo mbele mno, wameshafikia level ya kuweza kutoa Universal Basic Income kwa wananchi wake, yaani unalipwa hata kama hufanyi kazi.
Sisi huko bado, role model wetu tuanze na Singapore, kisha Korea kusini, kisha China.
Hao ndiyo wa kuiga kwao yale mazuri.

Kuhusu kukufafanulia kwa sababu ni mvivu kusoma vitabu, tusingepaswa hata kuwa na hii discussion hapa kama siyo msomaji wa vitabu.
Kama unakusanya kusanya vitu mtandaoni huko na kuja kujenga navyo hoja hapa tunaishia tu kupotezeana muda.

Nikuombe usome vitabu hivi viwili ambavyo nitaambatanisha hapa, kisha ukimaliza tuje tufanye mjadala wa kina hapa, wenye manufaa kwa taifa letu.

1. Seeing like a state.

2. From Third World to First: The Singapore Story
 

Attachments

πŸ˜‚πŸ˜‚
Ghafla umekuwa mwanasaikolojia wa kunidiagnose na kunishauri?
Watanzania mnapenda sana kukimbilia mambo yaliyo kabisa nje ya uwezo wenu.
Anyway, get money, #NothingElseMatters
Tena sio differential diagnosis,hiyo ni provisional diagnosis.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚
Ghafla umekuwa mwanasaikolojia wa kunidiagnose na kunishauri?
Watanzania mnapenda sana kukimbilia mambo yaliyo kabisa nje ya uwezo wenu.
Anyway, get money, #NothingElseMatters
Tena sio differential diagnosis,hiyo ni provisional diagnosis.
 
Ambacho hujajua,
Matajiri mitaji wote wakubwa, mitaji yao Ni watu maskini.

Kuanzia wafanyakazi, bidhaa zao Hadi Bei wanazouza sokoni Ni kwa ajili ya watu maskini
So hapa ni ishu kwako kuchagua Upande.
Mtoa mada kaelezea vizuri.
 
Matajiri wengi wazinzi tu ..hamna lolote hapo. Hiyo ni biashara ya kitabu unafanya. Utajiri ni Neema ya Mungu tu. Kuna wenye juhudi nyingi za kuupata lakini wameambulia hasara tu.
Whatever, binafsi nauchukia sana Umaskini
 
Mkuu,
Nashukuru kwa kunielimisha. Mimi siyo mtaalamu wa uchumi na wala sifahamu kila kitu. Ndio maana niliomba taarifa kwako. Machache niliyoyaeleza ni kutokana na ufahamu wangu mdogo wa kujifunza kwa kuunga unga tu mitandaoni.

Kwakuwa wewe ni msomaji, bila shaka utakubaliana nami kuwa mtu huelezea kitu kutokana na ukomo wa ufahamu wake. Kwahiyo mambo yaliyo juu ya ufahamu wangu siwezi kuyaelezea kwa usahihi wake.

Kama mfumo wa kibepari wa Marekani ndio unaona ni sahihi zaidi kuliko mfumo wa kiuchumi wa nchi za Ulaya ambao ni 'hybrid economic system (half capitalisms, half socialism) basi naomba niendelee kujifunza zaidi huenda nikawa na ufahamu mzuri kama ulivyo wewe na nikabadilika huko mbeleni.

Hata hivyo, kwa ufahamu wangu wa sasa, nitaendelea kuamini kuwa mfumo huu wa Ulaya ndio mzuri zaidi maana unaondoa social inequalities kwenye jamii. Ya kwamba, pesa zimilikiwe na watu wengi kuliko kumilikiwa na watu wachache kwenye jamii. Ikitokea wamekuwepo mabilionea basi iwe ni natural na siyo kwamba ndio iwe focus ya jamii nzima. Ikumbukwe, kuondoa social inequalities ni agenda mojawapo ya kudumu ya Umoja wa Mataifa. Kwa maoni yangu, na kwa ufahamu wangu mdogo nilionao, ubepari kamili unachangia kwa kiasi kikubwa social inequalities. Nifahamike kuwa simanishi turejee kwenye sera za ujamaa za Mwl Nyerere. Tuwe nusu ubebari, na nusu ujamaa kama ilivyo nchi nyingi za Ulaya.

Ila ngoja niendelee kujifunza na huenda nikabadilika na mie nikaanza kufata principles za kuutafuta utajiri kama unavyotuhimiza. Japokuwa inahitajika nguvu kubwa zaidi kubadilika maana mie sio muumini mzuri wa ubinafsi. Kidogo nachopata nagawana na wachache wenye shida zaidi ili kwenda nao sawa. Kitu ambacho ni kinyume na principlkes za kutafuta utajiri maana kwenye kutafuta utajiri inabidi uwe mbinafsi zaidi, na uwanyonye watu wengine ili wewe uendelee kuinuka juu. Mfano: Kama umeajiri watu uhakikishe unawabana kisawasawa ikibidi uwalipe mishahara ya kinyonyaji ili upunguze operational cosst na ku-maximize profit ili uwe bilionea. Hizi ni sifa mojawapo za kuelekea kwenye ubilionea. Huenda nikawa sipo sahihi pia kwa haya nayosema. Nipo tayari kuendelea kujifunza. Ahsante sana.
 
Aisee Mkuu haya Maisha ni namna utakavyofight na kumshirikisha Mungu unachotaka.

Ninaamini sana katika juhudi, Mungu unayemtaja ameweka nguvu kubwa ndani yetu! Inayofanya kazi kwa kadri tutakavyoitumia. Soma (Waefeso 3:20)

Tumia hiyo mistari kubadilisha maisha yako.

Unaweza kuwa jinsi unataka.
 
Mkuu wewe umejuaje au ni miongoni mwao?
 
Mkuu,
Tuendelee kujifunza, hakuna awezaye kujua kila kitu.
Na kwa mijadala ya aina hii inatufungua tufikiri zaidi.
Tukirudi kwenye hii mifumo ya kiuchumi, hakuna mfumo mmoja ambao ni bora kabisa na usio na mapungufu.
Lakini sasa ukilinganisha mifumo yote ambayo imewahi kujaribiwa hapa duniani, angalau ubepari una nafuu ukilinganisha na hiyo mingine.
Siyo kwamba ni perfect, lakini angalau unafanya mambo yaende.
Na siyo ubepari wa ubeberu, bali ubepari ambao unadhibitiwa kwa misingi sahihi.

Tukirudi kwa hoja ya ulaya, kikubwa nachokiona kwao ni ustaarabu.
Wenzetu wamestaarabika sana kiasi kwamba mtu anajua wajibu wake na kutekeleza na anajali maslahi ya wengine.
Ndiyo maana hybrid inafanya kazi kwao, social services ziko accessible kwa wote.
Na hayo ni matokeo ya uwekezaji ambao tayari ulishafanyika miaka mingi iliyopita.

Kwa sisi kwa kiwango cha ustaarabu tulichonacho, inabidi tukimbizane kwanza.
Ona hata demokrasia tu inavyotusumbua, tatizo ni moja, hatujafikia ustaarabu wa kutosha kuamini katika demokrasia.

Tenga muda usome vitabu viwili nilivyoshirikisha hapa kisha tutaendelea kujadiliana hili kwa kina zaidi.
 
Mada ya masikini na tajiri ni pana sana. Mtu anakua masikini au tajiri katika nyanja ipi kwa mtazamo wako? Kwa sababu unaweza kuwa tajiri wa pesa ila ukawa ni masikini wa viungo vya mwili, n.k n.k
 
Mada ya masikini na tajiri ni pana sana. Mtu anakua masikini au tajiri katika nyanja ipi kwa mtazamo wako? Kwa sababu unaweza kuwa tajiri wa pesa ila ukawa ni masikini wa viungo vya mwili, n.k n.k
Mkuu,
Utajiri na umasikini unapimwa kwa fedha na mali.
Hayo mengine ni njia za masikini kujifariji tu.
 
Masikini ni wateja wazuri wa matajiri
Kwenye hii dunia, kila mtu ni mteja kwa mwenzake.
Ndivyo uchumi unavyoenda.
Hivyo point ya msingi ni mtu uwe na pesa ili uweze kupata yale unayotaka kutoka kwa wengine ambao hawawezi kukupa mpaka uwape pesa.
 
Utajiri Ni Afya so Mtu mwenye Afya njema Ni tajiri maana Pesa Kupata hazina ugumu Sana
Nonsense,
Wangapi wana afya tele na hawana pesa, tena wamezama kwenye madeni?
Jamani, tutafute pesa, tuache kujifariji na mambo ya kijinga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…