miaka kama mitano iliyopita nilikuwa na mahusiano na dada mmoja wa jirani na mahali ninapoishi, mimi nilimsumbua sana kuingia kwenye mahusiano name ila akawa hataki, siku moja nilibahatika kupata kazi dar nikahama nilikokuwa mwanzo, nikiwa kule dar nikaja kujua kwamba naye amechaguliwa chuo cha sehemu ile ile nikaendeleza kumuomba tuwe na mahusiano (hapo tunchat kwa simu)
miezi imeenda akawa anasafiri kwenda bukoba nakumbuka niliamka asubuhi sana nimuwahi ubungo pale, nikamuwahi nikampa na zawadi mbili tatu, baadaye akaja kunikubalia.
Nikiwa likizo kazini nikarudi nyumbani kwetu nje ya dar, usiku mmoja nikapokea simu kwa namba ngeni kuuliza nani naongea naye nikajibiwa kuwa “mpenzi wako” mnhh nikiwaza ninao kama watatu na sikumbuki sauti zao vyema kwa sababu alibadili sauti, nikamwambia wewe ni anna (daah nikataja demu mwingine) bais akaniuliza uko wapi maana nimerudi kwetu huku, nikamjibu nipo hapa hapa likizo, akasema unafanya nini name kiutani nikamjibu kuwa nakunywa pombe, daah akaniacha pale pale hata sikuamini, mzigo sijala, mahusiano yamedumu kwa miezi kadhaa tu, looh, nikamuomba sana msamaha wapiii!!!
mwaka jana ameshuhudia tu pciha za ndoa yangu na mke wangu mzuri, akaishia kukomenti hongera best, ila najua pengine anaumia sababu aliniacha kwa kosa la kijinga ambalo lililkuwa linazungumzika, namshukuru akanifanya nikutane na huyu mama kija wangu mpenzi!
Wakati mwingine ukiachwa kubali tu huenda unapelekwa kwa mtu sahihi zaidi!