Singii
Member
- Jul 6, 2017
- 56
- 120
Nilipo kuwa chuo niliachwa kwa sms, nakumbuka ilikua mida ya saa12 jioni, Mara sms ikaingia, kusoma naona risala ndefu yakuachwa bila sababu yoyote, mwishoni anaandika eti usichukue maamuzi mabaya. Nilicheka moyonj nikasema huyu hanijui Mimi. Basi sikuwaambia hata room mates wangu, nilichofanya nilibeba madesa yangu nakuelekea seminar rooms kusoma, nikasema nikienda library naweza kuonana nae. Room mates walienda library, akawafata nakuwauliza , mbona mmemwa cha mwenzenu peke yake je ! akifanya jambo baya la kujidhuru?, wakamuuliza kwani kafanya nini? akajibu nimemwacha. Wakabaki wanashangaa , wakamwabia mbona hayupo room ameenda kusoma, alivyo sikia vile hakuamini ilibidi anitafute , ahakikishe, alinikuta napiga kitabu na niko norm. Akabaki anashangaa, tukapiga story mbili tatu, wala sikumgusia kuhusu kiniacha. Yaani nilikua na hasira moyoni, na hasira yangu iliishia kwenye kitabu, nahivi tulikua tunajiandaa na UE. Matokeo yalipo toka nilipiga balaa kuliko mitihani yote, yeye akapata sup 3, wale wenzangu nao wakawa na sup za kutosha. Alipoona matokeo yangu hakuamini, akanipigia na kusema hakufikiria kama nitafaulu vile alijua nitadisco .Tukabakia marafiki tu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app