Bora mkuu uko huko! Hutafuti kufikiri "nje" ya boksi, bali unaishi nje ya boksi.
Tushauri tuliopo huku nyumbani, tunawezaje na sisi kufikisha huko mboga na matunda tunayolima?
Bora mkuu uko huko! Hutafuti kufikiri "nje" ya boksi, bali unaishi nje ya boksi.
Tushauri tuliopo huku nyumbani, tunawezaje na sisi kufikisha huko mboga na matunda tunayolima?
Kuna wakati Kikwete aliishia kutuma vijana wakajifunze namna ya kufanya packaging ya bidhaa zetu
Ila tatizo la mswahili huwa hamalizi alichoanza hata siku moja kiufupi huwa wanaangalia nini wananchi wanaongelea halafu wanalianzisha linaishia katikati maana hawqjui kuendeleza
Kweli ukiangalia hata mizigo inayopelekwa mikoani kupitia malori tu au train jinsi walivyo pack utalia ni vurugu
Yaani unaagiza mzigo wa nguo unaweza kukuta spana ya gari imo ndani kisa mzigo wa mwingine wa spea umefumuka
Tunaweza ila je tuna matunda na mboga mboga za kila msimu?
Huku wanataka mzigo anakupa wiki Tatu in advance na uwe haujaharibika na unaweza kukaa kwa siku hata tano bila kuharibika kwa sababu ya masoko
Tunahitaji umwagiliaji sana bila kutegemea mvua kama tuna nia ya kuuza nje
Huku hawanunui kwa msimu wanaletewa kila siku kwa ndege
Ndio maana unaona jirani wanakuja kununua kwetu wakiwa kwao msimu tofauti
Hata SA wananunua sana parachichi kutoka kwetu na kuyauza ulaya kwa sababu lazima wakidhi mahitaji ya kila siku ya ulaya
Kuna tende fulani zinaitwa Majhul zilianzia Morocco na sasa wanazalisha mpaka USA na Saudia na Israel
Yaani ni tende kubwa sana na ni tamu pia
Sasa SA kajiongeza zipo sokoni hapa na nimetoa order yangu kwenda kuuza hapa hapa
Nafikiri na wao wameanza kuzalisha huko
Dunia ya leo kila mmoja anapata faida kubwa kwa chakula na sisi ardhi tunayo
Leo kuna shamba la ndani ya sehemu kubwa Los Angeles ambapo wamepanda kila kitu na hawahitaji ardhi bali ndani ya jengo kubwa wanapanda kila kitu
Sisi tunajivuta kwa mambo mengi sana yaani akili yetu especially tz naona inakuwa taratibu sana au viongozi hawataki maendeleo