Mkuu usiwaone wakenya wanakuja wale hawaji na lakisaba [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]. Wale wamejipanga ohoo! Ngoja nikuelezee. Kuna jamaa yangu alikuwa kwenye hizo ishu alinipaga ufafanuzi wakina. Ngoja nieleze kwa urefu, samahani kama nitakosea (spellings natype fastafasta).
1. Kwanza ili uweze kuexport vitu kwenda soko la Ulaya, Marekani, Uarabuni, UAE, Dubai, Saudi Arabia. Lazima uwe na vibali ambavyo vinalipiwa pesa, uwe na vibali vya ubora kama ISO standards,EU standards, Halal standards. Hapo pesa inahitajika
2. Uwe na mtaji wa kununua mazao na kusafirisha mazao mpaka sehemu husika. Hapo pesa inahitajika
3. Uwe na eneo ambalo linakidhi ubora wa kimataifa kwa ajili ya packing, wafanyakazi, mitambo ya packaging. Maana yake ama ujenge kiwanda au ukodi jengo lenye vigezo ndio uanze uzalishaji. Na ili upate certificate ya kimataifa inabidi jengo liwe lako sasa piga hesabu ya kununua kiwanja cha Light industry au heavy industry mpaka unapata hati ya kiwanja ushatoa rushwa mpaka umechoka [emoji1787][emoji1787], kujenga jengo kwa designs,michoro na ubora wa kimataifa EU,USA, ISO standards ni pesa [emoji1787], kuvuta umeme hapo ni kuwapa rushwa tanesco mpaka wakuletee umeme umeshachoka [emoji1787][emoji1787], kuweka mitambo hapo kutafuta mitambo inayotoa bidhaa yenye ubora wa kimataifa na mpaka uitoe mitambo bandarini ushatoa rushwa ya kutosha [emoji1787][emoji1787], kulipa wafanyakazi ambao wana ujuzi wa kuzalisha bidhaa yenye ubora wa kimataifa sio kulipualipua[emoji1787] , mpaka kufikisha ubora wa kimataifa umechoka[emoji1787][emoji1787][emoji1787]. Hapo ni pesa tu inahitajika
4. Uwe na uwezo wakutafuta container special la kusafirisha mazao na kulipakiaa ama kwenye meli au ndege. Hapo ni pesa inahitajika
5. Uwe na connection ya upande wa pili wa unakopeleka na hao unakoexport lazima uwalipe. Na mzigo kufika mpaka kwa mteja lazima ulipe. Hapo pesa inahitajika
6. Uwe na pesa ya marketing ya bidhaa unayozalisha, na kuhudhuria international exhibition mara kwa mara ili kupata wateja wakubwa. Hapo hela inahitajika.
7. Bado kuna kulipa kodi na usafiri wa pande zote mbili, nchi unayotoa mzigo na unakopeleka, hapo kwa Tanzania mpaka uzungushwe na kusumbuliwa kweli kweli [emoji1787]. Na Hapo hela inahitajika.
Baada ya harakati zote hizo ndio sasa unaanza kuingiza hela.
Huo mchakato wa kuzalisha bidhaa za kuexport unataka hela na ubora wa kimataifa. Ukifanya kosa moja TU umekula hasara. Mzigo kama hauna ubora wa kimataifa unatupwa. Huko wenzetu wako very serious, sio huku ukitoa rushwa mzigo feki unavuka [emoji1787]
Ndio maana matajiri wa kibongo hawapo kwenye viwanda vya kuexport vitu kwenda soko la kimataifa. Wao wapo kwenye biashara za kuagiza vitu dubai,china, uturuki. Weka kwenye stoo na madukani unauza unapata hela bila usumbufu. Au wanajenga mahoteli na mabar mkalewe humo na kuzagamuana humo wao waingize hela. Au wanajenga sheli, mkaweke mafuta waingize hela fasta. Au wanajenga shule, mlipie ada watoto wao waingize hela. Au wananunua malori na macontena na mafuta, yapige safari za Congo, Zambia, Rwanda, Burundi, waingize hela. Au wanaweka viwanda vya unga wa ngano, juisi, energy drinks, pombe, mnunue mnywe/mle waingize hela. Au wananunua mabasi ya mkoani, weka nauli pandeni safirini, wao wanaigiza hela.
Sekta ya kuexport vitu sio rahisi kama unavyofikiria. Hao wakenya wamejipanga na ni wazoefu. Msiwachukulie poa.