Kama Wakenya wameweza, sisi tunashindwa kwenda kujifunza kwao?

Kama Wakenya wameweza, sisi tunashindwa kwenda kujifunza kwao?

Inasemekana, kuna wakati Wakenya walikuwa wanakuja Tanzania, nafikiri Gairo, kununua viazi mviringo na kwenda kuvifsafisha, kuvigrade, na kuvifanyia packaging kisha kuvisafirisha kwenda sokoni Dubai.

Inasemekana, Wakenya hua wanavifuata vitunguu Tanzania, si kwa ajili ya kuviuza Kenya, bali nchi za nje hasa Dubai.

Inasemekana, hata Wachimbaji wadogo wa madini ya Tanzanite, kwa miaka ya nyuma, walikuwa wanapendelea zaidi kuuza madini yao Kenya kuliko nchini. Inaonekana kulikuwa na cha ziada walichokuwa wanakipata huko, vinginevyo, wasingejihatarisha kiasi hicho kutorosha madini mpaka Kenya.

Inasemekana, miaka ya nyuma , Kenya ilikuwa ikisafirisha Tanzanite nyingi zaidi kuliko Tanzania, nchi pekee duniani Tanzanite inakopatikana.

Inasemekana, miaka ya nyuma, Wakenya walikuwa wakifuata parachichi nchini Tanzania. Kipindi hicho, parachichi zilikuwa na bei nzuri, lakini walipoacha kufanya hivyo, wakulima wa Tanzania wakaambulia maumivu. Na hayo maparachichi, Wakenya walikuwa wakienda kuyasafirisha kwenda "ng'ambo".

Inavyoonekana, Wakenya wako vizuri zaidi kwenye biashara za "Kimataifa" kuwazidi Watanzania.

Wakenya ni "ndugu" zetu, kama wao wameweza, kwa nini sisi tushindwe?

Haitakuwa jambo jema endapo tutaamua kwenda kujifunza kwao?

Binafsi ninafikiria nimtafute Mkenya aliye vizuri kwenye hilo eneo ili nimfanye "mentor" wangu.

Tanzania tuna fursa nyingi sana. Tunachohitaji ni IDEA EXPLOSION!
Serikali ipunguzee urasimu
 
Nasafirisha Parachichi za Burundi kwenda Uholanzi kama vile zinatokea Tanzania biashara sio kulia lia bali ujanja
Hongera sana mkuu. Ikikupendeza, tumegee Elimu japo kidogo kuhusiana na hiyo biashara.
 
Mkuu, naomba uuondoe huo msamiati wa "hatuwezi", tunataka na sisi tuweze kama wao, na zaidi.

Tufanyeje ili tuwe bora kuwazidi?
Hii inawezekana kama Serikali yetu ikiwa na dhamira ya dhati. Vizuizi Tanzania ni vingi sana na pia roho ya wivu ni kubwa sana. Nchi yetu ni ngumu kufanya bihashara ndiyo maana hata wawekezaji huku kwetu inakuwa ngumu.
 
🙏
 
Halafu kuna kitu kingine, wakenya wanakopeshwa sana hela nyingi na mabenki yao sanasana Equity Bank Kenya inawapa sana mikopo. Yule Ceo wa Equity Bank Kenya ni mjanja na mbunifu kufinance wafanyabiashara Kenya.
Hao sasa ndiyo mabankers waliosoma na kuelimika. SJ kama "wale" wengine ambao hata kama una vigezo vya kupewa, bado wanaweza wakakuomba rushwa ili wakupitishie mkopo wako.
 
2021 22 Julai

Natengeneza Millioni Ishirini kwa Mwezi - Kyando

View: https://m.youtube.com/watch?v=ABgMyvX3FxE

Kutana na Ezron Satoki Kyando Mkulima na mwanachama wa TAHA kutoka Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani nchini Tanzania ambaye ameanza kuona matunda ya kilimo cha horticulture. Kyando ameweza kubadilisha maisha yake huku akikiri kuwa hata mshahara wake haujawahi kufikia faida anayopata hivi sasa kupitia kilimo cha horticulture.
Source : TAHA ONLINE TV

🙏🙏🙏
 
Halafu maendeleo hayataki kabisa demokrasia. Huko China ukileta ujinga kama vile ufisadi adhabu ni kifo. Hawakufika hapo kienyeji kwa kupiga porojo. Watu wasijilinganishe kabisa
Sidhani kama ni sahihi mkuu. Kama ndivyo, MAREKANI, Canada, Uingereza, Ujerumani, n.k. zisingekuwa kwenye G20.
 
Sidhani kama ni sahihi mkuu. Kama ndivyo, MAREKANI, Canada, Uingereza, Ujerumani, n.k. zisingekuwa kwenye G20.
Marekani ina demokrasia gani? Hillary Clinton alishinda kura za wananchi akaja kushindwa kwenye kura za watu 240 tu wanaojiita electoral college.
 
Nchi zilizo pata kurupushani za bunduki, kufany mabadiliko ................................................................................
 
Benjamin Fernandes wa NALA ulishawahi kujiuliza kwanini hakuamua HQ za kampuni yake ziwepo bongo badala yake amezipeleka Nairobi?

Utajifunza kitu kuhusu issue ya Starlink walichofanyiwa hiyo ni mifano miwili tu muhimu.

Hapo Nairobi Google wanazo ofisi.

Hapo Nairobi Microsoft wanazo ofisi.

Viongozi wa Tanzania wako busy kuhakikisha moto unakimbizwa kila mkoa eti kuzindua miradi kwa mabilioni ya pesa.

Huku kwenye mitandao wakina Mwashambwa wanapewa $3 kusifia kwa kila post na wao wanaona sawa na siku inapita wakijiita ni wazalendo.

Jione tofauti.
 
Aisee
 
Inasemekana, kuna wakati Wakenya walikuwa wanakuja Tanzania, nafikiri Gairo, kununua viazi mviringo na kwenda kuvifsafisha, kuvigrade, na kuvifanyia packaging kisha kuvisafirisha kwenda sokoni Dubai.

Inasemekana, Wakenya hua wanavifuata vitunguu Tanzania, si kwa ajili ya kuviuza Kenya, bali nchi za nje hasa Dubai.

Inasemekana, hata Wachimbaji wadogo wa madini ya Tanzanite, kwa miaka ya nyuma, walikuwa wanapendelea zaidi kuuza madini yao Kenya kuliko nchini. Inaonekana kulikuwa na cha ziada walichokuwa wanakipata huko, vinginevyo, wasingejihatarisha kiasi hicho kutorosha madini mpaka Kenya.

Inasemekana, miaka ya nyuma , Kenya ilikuwa ikisafirisha Tanzanite nyingi zaidi kuliko Tanzania, nchi pekee duniani Tanzanite inakopatikana.

Inasemekana, miaka ya nyuma, Wakenya walikuwa wakifuata parachichi nchini Tanzania. Kipindi hicho, parachichi zilikuwa na bei nzuri, lakini walipoacha kufanya hivyo, wakulima wa Tanzania wakaambulia maumivu. Na hayo maparachichi, Wakenya walikuwa wakienda kuyasafirisha kwenda "ng'ambo".

Inavyoonekana, Wakenya wako vizuri zaidi kwenye biashara za "Kimataifa" kuwazidi Watanzania.

Wakenya ni "ndugu" zetu, kama wao wameweza, kwa nini sisi tushindwe?

Haitakuwa jambo jema endapo tutaamua kwenda kujifunza kwao?

Binafsi ninafikiria nimtafute Mkenya aliye vizuri kwenye hilo eneo ili nimfanye "mentor" wangu.

Tanzania tuna fursa nyingi sana. Tunachohitaji ni IDEA EXPLOSION!
Yote haya ilaumu serikali ya CCM kudumaza akili za Watanzania kwa miaka yote hii toka uhuru. CCM inawaelekeza watu waendelee kuwa watulivu na kuomba Mungu na kutaka wananchi wake waendelee kuabudu Waarab na Wayahudi huku wakitumia viongozi wa hizo dini za hao watu. CCM is a parasite kwa kweli.
 
Tuliwacheka walipowakumbatia wazungu baada ya Uhuru, na sisi tukawafukuza kama paka mwizi na kuwaambia imetosha na uhuru mmetupa kwaherini kana kwamba tutaweza

Wenzetu mpaka leo kuna wazungu wenye mashamba huko na wao (wazungu) ndio waliowafundisha kila kitu kuanzia ukulima wa faida mpaka packaging na usafirishaji

Wao wamefanikiwa hata kwenye mashamba ya chai na ndio mpaka Ulaya tunakunywa chai yao na makampuni makubwa kama Unilever ni kubwa sana na ndio wanunuzi wao wakubwa wanatengeneza PG tips
Ukija kwenye soko la mboga na matunda kwa mfano Western International Market ya West London utakuta bidhaa nyingi zinatoka Kenya
Ila Tz hutaona hata nyanya moja lakini za Uganda pia zipo bidhaa nyingi tu na mimi ni mnunuzi mkubwa hapo

Wenzetu wametuzidi sana kwa sababu ya elimu na pia vibali kupata ni balaa kwa Tz ila bidhaa zetu nyingi zinaenda Kenya na mpaka South Africa ila zinaandikwa zimetoka huko
Sisi wakulima ni dhalili sana wakati wao mkulima ana nguvu haswa
Kumbe suluhisho la tatizo lipo ...yupo huyu mwenzetu ana A B C kwa nini tusianze na kupata elimu kutoka kwake mtanzania mwenzetu kwa hicho kidogo anachojua halafu kuhusu changamoto za vibali viongozi wetu ni wasikivu jamani tusiwe watu wa kujikatisha tamaa kwa maneno yetu wenyewe maana usemacho ndicho utakachopata hata dini zetu zinatuinya.Watz tuna uelewa mkubwa tunakosea sehemu kidogo mfano upendo na uaminifu kati yetu lakini kichwani tuko vizuri sana kuliko hao majirani zetu ndio maana wao wanakuja kutumia fursa zetu ...Tuamke sasa tuache kulaumu tupambane
 
Tuwe wakweli jmn pia wengi wetu hatuna elimu ya biashara ndio maana mabenki mengi utakuta wameweka masharti mengi kwetu kwa sababu tukikopa hatuna utamaduni wa kulipa kwa wakati...yaani ukiwauliza banks mbalimbali watakuonyesha orodha ndefu wa watz walioshindwa kukipa madeni ya mikopo ya biashara kwa wakati,hivyo basi kabla ya kukopa tupate elimu ya biashara,elimu ya jinsi vyombo,taasisi za serikali zinavyo fanya kazi hadi kupata vibali halal bila vikwazo
 
Kumbe suluhisho la tatizo lipo ...yupo huyu mwenzetu ana A B C kwa nini tusianze na kupata elimu kutoka kwake mtanzania mwenzetu kwa hicho kidogo anachojua halafu kuhusu changamoto za vibali viongozi wetu ni wasikivu jamani tusiwe watu wa kujikatisha tamaa kwa maneno yetu wenyewe maana usemacho ndicho utakachopata hata dini zetu zinatuinya.Watz tuna uelewa mkubwa tunakosea sehemu kidogo mfano upendo na uaminifu kati yetu lakini kichwani tuko vizuri sana kuliko hao majirani zetu ndio maana wao wanakuja kutumia fursa zetu ...Tuamke sasa tuache kulaumu tupambane
Hatulaumu Mkuu bali tunajaribu kupambana sana ila kuna watu wanaweka ngumu mpaka utoe kitu ingawa hawajui umehangaika kiasi gani kufika hapo

Wenzetu wazungu leo wamefika sehemu wala huonani na binadamu uso kwa uso ni mitandao tu unamaliza kila kitu
Mtandao hauombi rushwa ingawa hawana rushwa wala tamaa wenzetu ila wamerahisisha sana mambo

Zama hizi kuonana na mtu ana kwa ana Ulaya ni nadra sana kwenye biashara au ofisi za umma
Sisi nyumbani kila kitu lazima uende ofisini na huko unakuta mafisi yanasubiri
 
Hatulaumu Mkuu bali tunajaribu kupambana sana ila kuna watu wanaweka ngumu mpaka utoe kitu ingawa hawajui umehangaika kiasi gani kufika hapo

Wenzetu wazungu leo wamefika sehemu wala huonani na binadamu uso kwa uso ni mitandao tu unamaliza kila kitu
Mtandao hauombi rushwa ingawa hawana rushwa wala tamaa wenzetu ila wamerahisisha sana mambo

Zama hizi kuonana na mtu ana kwa ana Ulaya ni nadra sana kwenye biashara au ofisi za umma
Sisi nyumbani kila kitu lazima uende ofisini na huko unakuta mafisi yanasubi
Tushaanza mkuu siku hizi lesseni unaomba kwenye mtandao,kufungua kampuni unaomba kwenye mtandao ...sawa zipo changamoto mblmbl ndogondogo tena za mtu mmoja mmoja hazikosekani ndio maana ya vyombo vya sheria au viongozi wetu wapo......niseme ukweli Uongozi uliopo umepania kweli watanzania tutoke kimaisha ila hatuwezi kutoka kwa kukaa kulia lia tu hakuna pesa rahisi ingekuwa hivyo kila mtu angekuwa Bhakresa ( nimetoa mfano) ...pence changamoto wajasiriamali tukae tujadili...labda nikuulize wewe ni mwanachama wa chama cha wafanyabiashara hapo ulipo? yaani TCIA? huko watakupa A B C ya haya maswali yako.Raisi wetu SSH anasema kila nchi ina utamaduni na historia yake hatuwezi kutumia utamaduni wa wenzetu kufanikisha ya kwetu hilo la msingi sana ...utamaduni wa kutomuabudu mzungu bali kumheshimu kama binadamu mwenzetu na ndio maana kwao kuna ukabila kwetu hakuna ...hivyo nasi tuna mazuri mengi tu ....tupambane tuache lugha za kukatishana tamaa maisha hayajawahi kuwa mepesi ...na kila leo ni mpya hivyo kujifunza ni muhimu
 
Hatulaumu Mkuu bali tunajaribu kupambana sana ila kuna watu wanaweka ngumu mpaka utoe kitu ingawa hawajui

Yote haya ilaumu serikali ya CCM kudumaza akili za Watanzania kwa miaka yote hii toka uhuru. CCM inawaelekeza watu waendelee kuwa watulivu na kuomba Mungu na kutaka wananchi wake waendelee kuabudu Waarab na Wayahudi huku wakitumia viongozi wa hizo dini za hao watu. CCM is a parasite kwa kweli.
Hebu tuchukue kweli matatizo yetu A % yamesababishwa ba CCM kama unavyosema Au pia tuchukulie B % zingine ni matatizo waliyotaja wengine kama elimu,afya ,nk je ni watanzia wangapi leo hii wana uhakika wa kula,kusoma,malazi na kupata huduma ya afya? ...Je wote wanaji shughulisha na nini? Wamesomea? Wana vyeti? Leseni? ....Ninachotaka kusema ni kwamba kumbe tunaweza kuishi hata kama kuna chama kibaya lakini muhimu watu wapate mambo ya msingi manne 1.Chakula 2.Afya 3.Malazi 4.Elimu ....halafu mtu ukaweka nguvu kwenye eneo lako ulilosomea iwe. Kilimo,biashara au ajira ukafuata taratibu zote za nchi fanya kwa bidiii tena ukiomba Mungu wako kila wakati na uhakika utafanikiwa ...tuache kulaumu kuongoza ni kazi jamani ...ni kipaji kwanza..Watanzania tunakosea padogo kusifia sana wenzetu ( hata kama hatujui changamoto zao) kama vile sisi ni mazuzu vile...jamani mimi nakataa nina akili nzuri tu naweza kufanya anachofanya mkenya,mzungu nikiamua.
 
Back
Top Bottom