Kama waziri kuonana na Rais ni changamoto hivi, kuna shida mahali

Kama waziri kuonana na Rais ni changamoto hivi, kuna shida mahali

Kwenye vikao vya Baraza la mawaziri hawaonani huko?
Nashangaa

Raisi Samia hapendi umbeya
Email ya ikulu anayo,simu anayo,bosi wake waziri mkuu yupo

Hicho anataka kupeleka umbeya kwa raisi kitu gani?

Huyu Mkenda pia ana shida nakumbuka aliongeq bungeni akiponda kuwa bodi ya mikopo ya Elimu ya juu hawampi ushirikiano
Alipobanwa baadaye akakana kuwa hakusema

Afanye kazi zake kwa kuzingatia taratibu
Ofisi ya Raisi sio banda la chips kuwa waweza tu kwenda kutaka kuonana na raisi
 
huyo anawaamini akina zuchu na mwijaku, ila watu muhimu hana la kuzungumza nao...tuna shida sana kama taifa
 
Nashangaa

Raisi Samia hapendi umbeya
Email ya ikulu anayo,simu anayo,bosi wake waziri mkuu yupo

Hicho anataka kupeleka umbeya kwa raisi kitu gani?

Huyu Mkenda pia ana shida nakumbuka aliongeq bungeni akiponda kuwa bodi ya mikopo ya Elimu ya juu hawampi ushirikiano
Alipobanwa baadaye akakana kuwa hakusema

Afanye kazi zake kwa kuzingatia taratibu
Ofisi ya Raisi sio banda la chips kuwa waweza tu kwenda kutaka kuonana na raisi
Kuna vitu Raisi anatakiwa kuelezwa kabla ya Kikao cha Baraza la mawaziri. Na akisharidhika ndio inaingia kama Agenda kwenye kikao cha Baraza la mawaziri.
 
Mifumo ya Tanzania ni ya kijinga sn, Stive Nyerere ni rahisi kumuona Rais kuliko Waziri/KM/RC/RAS/DC/Mbunge n.k, chawa wana thamani kubwa sn
Ndugu wala sio mifumo, ndio uhalisia wa tulipofikishwa na CCM.

CCM wanaamini (na ndivyo ilivyo) katika wizi wa kura ili wawepo madarakani, na si kwa utendaji uliotukuka.

Steve Nyenyere anaweza "kuhalalisha" ushindi wa kishindo wa CCM kwa kujaza watu kwenye mikutano ya kampeni tofauti na Prof. Mkenda ambaye (hata yeye binafsi anafahamu) hawezi kuihalalishia ushindi CCM kikampeni.

Kwa CCM na viongozi wao, mtu yeyote mwenye ushawishi wa wajinga wengi (mfano Mwamposa, Diamond, Ally Kiba na wengineo) kwao ni assets kwani wanaweza kuhalalisha ushindi wao kwa kuwakusanya hao wajinga kwa maelfu.
 
Rais anatakiwa awe na wasaidizi binafsi kama Katibu Binafsi ambao ni vichwa hasa wenye uelewa wa mambo mengi na ambao ni wazalendo kweli kweli.

Nina uzoefu na makatibu wa wabunge 11( mawaziri 4), ni vituko tu hao wasaidizi wao.

Natamani kama kwenye katiba au kanuni za bunge tuweke kipengele cha kumpatia kila kiongozi msaidizi kutoka TISS, Vyuo Vikuu au Taasisi ya Utafiti na Takwimu (Research Bureau) kama ipo.

Wabunge wengi pamoja na mawaziri na viongozi wengine wasaidizi wao wamekuwa ni "errand boys", kutumwa kwa michepuko tuu,kichwani weupeee.
 
Waziri Salum asiye na cheo chochote anaingia ikulu kama chooni na anaongea na rais kama vile mpenzi wake
Screenshot_20250125-133202.png

Lkn waziri wa masuala ya elimu anazinguliwa kuonana na rais. Shubamiti!!
 
Back
Top Bottom