Kama wewe ni smart na una akili, kwanini hujafanikiwa kuwa Tajiri? Inageukia kwamba wewe ni mjinga

Binafsi sidhani mafanikio ni kuwa tajiri, bali mafanikio ni kutimiza matamanio au matakwa yako binafsi. Wenda nisiwe mjinga kwa maana utajiri haupo kwenye matamanio yangu.
 
kweli kabisa, kuna vigezo vingi kwahiyo unaweza ukawa na akili na usitajirike

na bahati ina mchango mkubwa sana, huwa naandika humu

sema sasa watu wengi hawaelewi maana ya bahati

bahati ni zile nafasi unazopata bila juhudi/ujuzi wako binafsi
Mfano umezaliwa ukakuta tayari baba yako ni raisi wa nchi😅
 
Yaani mimi nipambane kuforce connection za michongo ya shamba.

Nipate japo kibishi, Nifanye kazi kwa taabu mvua yangu, jua langu 24/7.

Nikusanye kakiasi nianzishe biashara Inakufa, Narudi tena shamba naanzisha tena biashara inaenda vizuri, mara naanguka tena.

Sikati tamaa narudi tena farm round hii ka-bussiness kanajipa, Kanakua, nidhamu ya kutosha, ubahili wa kuzidi mpaka inakua kitu cha kueleweka.

Lei hii aje mtu kirahisii rahisi tu anasema Mafanikio ni bahati, Sijui mpango wa Mungu, Are you serious..?


Haijalishi una akili au Huna, kama Huna hamu ya mafanikio na kama Hauendi speed kutafuta fursa, yaani unaamini bado una muda utafanya kesho, Endelea kusubiria bahati....😆😆


NB: Mjinga aliye focus hufanikiwa zaidi kuliko Mwenye akili aliyeridhika tu na kupoa akiamini "one day Yes".
 
"Better to be born lucky than gifted"
 
MAFANIKIO = Akili X Busara X Nguvu za kiroho X nafasi (fursa).
Kimojawapo kikikosa Mafanikio ni 0 (sifuli). Kwahiyo ni wastani wa hivyo nilivyovitaja. Ukiwa na akili sana na busara na pia ukawa mwombaji au unatumia mashetani lakini ukakosa fursa (nafasi) ya kutumia hivyo vipawa utaishia umasikini
 
"Better to be born lucky than gifted"
 
Tazama Kiswahili kinavyopea:

1. Wealthiness = Utajiri
2. Richness = Utajiri

Hao watu smart na wenye akili , wengi wapo katika kundi la pili, na bila shaka wana mchango mkubwa katika kuwafanikisha watu wa kundi la kwanza.
Asili (nature) ndiyo inatutaka binadamu tuwe hivyo na kamwe hatuwezi wote kuwa matajiri wa mali au wote tukawa smart na wenye akili. Muhimu katika maisha ni kuwa na kuimarisha furaha zetu..!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…