Yaani mimi nipambane kuforce connection za michongo ya shamba.
Nipate japo kibishi, Nifanye kazi kwa taabu mvua yangu, jua langu 24/7.
Nikusanye kakiasi nianzishe biashara Inakufa, Narudi tena shamba naanzisha tena biashara inaenda vizuri, mara naanguka tena.
Sikati tamaa narudi tena farm round hii ka-bussiness kanajipa, Kanakua, nidhamu ya kutosha, ubahili wa kuzidi mpaka inakua kitu cha kueleweka.
Lei hii aje mtu kirahisii rahisi tu anasema Mafanikio ni bahati, Sijui mpango wa Mungu, Are you serious..?
Haijalishi una akili au Huna, kama Huna hamu ya mafanikio na kama Hauendi speed kutafuta fursa, yaani unaamini bado una muda utafanya kesho, Endelea kusubiria bahati....😆😆
NB: Mjinga aliye focus hufanikiwa zaidi kuliko Mwenye akili aliyeridhika tu na kupoa akiamini "one day Yes".