Kama wewe ni smart na una akili, kwanini hujafanikiwa kuwa Tajiri? Inageukia kwamba wewe ni mjinga

Kama wewe ni smart na una akili, kwanini hujafanikiwa kuwa Tajiri? Inageukia kwamba wewe ni mjinga

kweli kabisa, kuna vigezo vingi kwahiyo unaweza ukawa na akili na usitajirike

na bahati ina mchango mkubwa sana, huwa naandika humu

sema sasa watu wengi hawaelewi maana ya bahati

bahati ni zile nafasi unazopata bila juhudi/ujuzi wako binafsi
Kama hujatajirika maana yake huna akili dada/kaka, bahati hata ikitokea kama huna akili unaitumiaje/unaijuaje? Kujua tu fursa ni akili, tusijitoe ufahamu
 
Nashukuru kwa maoni yako. Mafanikio ni dhana pana na inaweza kuwa na maana tofauti kwa kila mtu.
Kama unavyosema, mafanikio yanaweza kutimiza malengo na matakwa yako binafsi, hata kama hayo hayahusiani na utajiri wa kifedha.

mafanikio ni kile kinachokuleta furaha na kuridhika, iwe ni kwa kuwa na afya nzuri, kujenga familia, au kufikia ndoto zako binafsi, bila kujali utajiri wa kifedha.
Hapa inaongelewa mafanikio au utajiri? Mafanikio kila ntu ana tafsiri yake, wengine wanaweza kusema kuoa tu ni mafanikio, wkt kwa mwingine kuokoka au kufaulu test moja
 
bahati hata haihitaji akili, inakukumbatia tu
Wapo wengi waliokota dhahabu na hawakujua so tunaitaje hii kiongozi? Mtu akitumia maarifa na yakamtoa ndio tunasema alipata bahati period! Kama hakutumia chance tunasema hana bahati, lakini maarifa ya kutumia chances ndio akili ambayo baadaye tutasema alikuwa na bahati!
 
kila mtu ni bora katika sector fulani...tatizo linakuja kwenye kujua ubora wako,..... duniani hakuna BAHATI.... mafanikio ya kiuchumi yanahitaji zaidi ya akili pia maamuzi magumu...
 
Yaani mimi nipambane kuforce connection za michongo ya shamba.

Nipate japo kibishi, Nifanye kazi kwa taabu mvua yangu, jua langu 24/7.

Nikusanye kakiasi nianzishe biashara Inakufa, Narudi tena shamba naanzisha tena biashara inaenda vizuri, mara naanguka tena.

Sikati tamaa narudi tena farm round hii ka-bussiness kanajipa, Kanakua, nidhamu ya kutosha, ubahili wa kuzidi mpaka inakua kitu cha kueleweka.

Lei hii aje mtu kirahisii rahisi tu anasema Mafanikio ni bahati, Sijui mpango wa Mungu, Are you serious..?

Haijalishi una akili au Huna, kama Huna hamu ya mafanikio na kama Hauendi speed kutafuta fursa, yaani unaamini bado una muda utafanya kesho, Endelea kusubiria bahati....😆😆

NB: Mjinga aliye focus hufanikiwa zaidi kuliko Mwenye akili aliyeridhika tu na kupoa akiamini "one day Yes".

Ni kweli kabisa kwamba mafanikio yanahitaji juhudi na nidhamu kubwa.

tafiti zinazohusiana na utajiri na mafanikio, kama ilivyoelezwa katika utafiti wa MIT Technology Review kuhusu mchango wa bahati katika mafanikio, zinaonyesha kuwa si lazima mtu mwenye kipaji kikubwa ndiye atakayefaidi zaidi, bali ni wale waliokuwa na "bahati" ya kushika fursa zinazoletwa na mazingira yao.

Hata hivyo, badala ya kuangalia mafanikio kama suala la bahati tu, mifano ya watu kama Bill Gates inadhihirisha kuwa mazingira, wakati, na juhudi binafsi huleta matokeo bora zaidi.

Kwa hiyo, kama unavyosema, hakuna mafanikio yanayokuja bila juhudi na kufanya kazi kwa bidii.
 
Newton alikufa maskini naye alikua anaakili
19 kweusi kule?? Unajuaje kwamba level aliyokua nayo wakati ndio ilikua utajiri? Kuna facts zake za net-worth yake ya miaka hiyo na comparison ya matajiri wa wakati huo?

Isaac Newton's net worth was just over £30,000 shortly before the South Sea Bubble started and was around the same when he died in 1727. However, he did lose a significant amount of money during the bubble. Paund hizo miaka hiyo unaona alikuwa maskini? Leo hii tu bado amount hiyo ni significant sembuse miaka 300 iliyopita? You are jokingi braza!

Mtoto wa Bakhressa aliweka juhudi gani mpaka azaliwe na billionaire?

Bakhressa anaweza zaa kilaza/mbumbumbu ambaye hata jina lake kusoma na kuandika atashindwa wala kuhesabu atashindwa kujua lakini straight on ni billionaire, bila juhudi.

Kwa upande mwingine. Mtoto wa muuza viazi anayekosa dawa ya kutibu ugonjwa wa macho yaka-develop upofu taratibu huku yeye na familia wakiona baadae akawa kipofu anakuwa hajaweka juhudi gani huyo mtoto?

kwa mjibu wa mifano hii, mafanikio si jambo linalojitokeza tu kwa juhudi binafsi, bali ni matokeo ya mchanganyiko wa vipengele vingi ikiwa ni pamoja na fursa, mazingira, na bahati.
 
Kubadikisha akili kuwa mali ni kazi kubwa mno chief - na ndiyo maana unashangaa kukuta Prof ni chawa.
 
Utajiri ni siri na kudhamiria unawezakuwa unaakili ila huna siri,ninaposema siri ni wenye siri ndo watanielewa

Ndio, hili ni ukweli kwamba utajiri sio tu suala la kuwa na akili bahati au juhudi, bali pia inahusisha 'siri' au maarifa ya ndani kuhusu jinsi ya kutumia fursa zilizopo. '

'Siri'
(CLASSIFIED) inaweza kumaanisha kwamba kuna mambo yasiyo wazi au yaliyo na ugumu kwa wengine, lakini watu waliopata mafanikio wanajua na kuyaendeleza kwa busara.
 
Ni kweli kabisa kwamba mafanikio yanahitaji juhudi na nidhamu kubwa.

tafiti zinazohusiana na utajiri na mafanikio, kama ilivyoelezwa katika utafiti wa MIT Technology Review kuhusu mchango wa bahati katika mafanikio, zinaonyesha kuwa si lazima mtu mwenye kipaji kikubwa ndiye atakayefaidi zaidi, bali ni wale waliokuwa na "bahati" ya kushika fursa zinazoletwa na mazingira yao.

Hata hivyo, badala ya kuangalia mafanikio kama suala la bahati tu, mifano ya watu kama Bill Gates inadhihirisha kuwa mazingira, wakati, na juhudi binafsi huleta matokeo bora zaidi.

Kwa hiyo, kama unavyosema, hakuna mafanikio yanayokuja bila juhudi na kufanya kazi kwa bidii.
Mkuu kwenye bidii 👍🏾, Ila bado siwezi kukuunga mkono hapo kwenye upande wa bahati.

Bahati iko in-term of spiritual being wakati huo Mafanikio ni mchakato halisi - Physic, Logic and Mantic.

Mkuu usiwe unapenda kuconclude mambo/jambo kwa watu wengi based on maoni ya watu wachache.

Wanaofanikiwa kupitia hiyo bahati "kamseleleko" kiukweli wapo ila sio moja kwa moja, bado kuna jitihada waliitumia mfano Mtu alieshinda mkeka - alitake risk mara kadhaa 😆😆

Lakini ni wachache mno hawatoshi kuthibitisha kwamba Mafanikio ni "Bahati,".
 
kwa mjibu wa mifano hii, mafanikio si jambo linalojitokeza tu kwa juhudi binafsi, bali ni matokeo ya mchanganyiko wa vipengele vingi ikiwa ni pamoja na fursa, mazingira, na bahati.
Exactly. Mtu yeyote anayetaja mafanikio akakosa kuitaja bahati hajui maisha huyo.

Kagame hakutakiwa kuwa Rais wa Rwanda, aliyependwa na kuongoza vizuri zaidi alikuwa kamanda Fred Rwigyema ila bahati ilikuwa ya Kagame baada ya Rwigyema kufa. Samia hakugombea na sasa ni Rais, hajatolea jasho Urais hata kidogo hata yeye aliwahi sema ni "kudra za mwenyezi Mungu".
 
Kufanikiwa siyo kuwa tajiri.kufanikiwa ni neno pana sana linalojumuisha kutokuwa na makandokando kwenye jamii Yako ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto ambaazo zinaisumbua jamii.mfano aliyegundua gari na aliyegundua dawa kama vile za ukimwi,malaria n.k hao ndiyo walifanikiwa.unaweza ukawa tajiri lakini ukawa kero Kwa jamii.
 
Ni ujinga ndio... Wengi wanatafuta pesa badala yakufanya pesa iwatafute.
Ukitafuta pesa utaiba, utakuwa jambazi, utafisadi, utakaba, utakufa pia.
 
Nimefanikiwa kuwa Tajiri wa afya, Tajiri wa amani ya moyo, Tajiri wa mapendo, Tajiri wa kutenda mema, Tajiri wa kusaidia jamii yangu kupitia elimu yangu ili kutatua changamoto mbalimbali katika society, Tajiri wa kuonyesha mfano wa tabia Njema ya kuigwa kwa wakubwa na wadogo katika jamii yangu,Tajiri wa Hekima, akili na busara, Tajiri wa Uongozi wenye kuacha tija na alama katika Jamii yangu,..............nk.

Mimi ni smart na nina akili, Hayo mafanikio mengine unayoyazungumzia ni yapi?
 
Thamani ya vitu unavyomiliki ikiwa Ni pamoja na pesa ndio utajiri na sio kuwa na afya, tabia njema nk.
 
Back
Top Bottom