Kama wewe ni smart na una akili, kwanini hujafanikiwa kuwa Tajiri? Inageukia kwamba wewe ni mjinga

Duniani hakuna bahati.
 
Humu jf tajiri niko pekeangu naona wengi wananiongelea mimi tu

Ni hivi uthubutu na nidham ya pesa ndio kila kitu kwenye tasnia ya utajiri akili uwe nazo tu za kung'amua yaani usiwe kichaa tu basi umemaliza
 
Ni ujinga huwezi Lima kwa kutegemea mvua.
Na endapo utapata Basi itakuwa kwa bahati.
 
Unafanyaje pesa ikutafute?
Yes, pesa ipo kila mahali na kila unayemwona Ni pesa hiyo hivyo Basi unatakiwa kuweka vipendwa vitakavyosababisha pesa ikutafute.

Mfano rahisi fundi uashi unapojenga kwa ufanisi wa hali ya juu kiasi Cha kuwa attract watu kukuulizia, Basi hapo jua inakuulizia pesa au pesa inakutafuta.
Lkn ukiwa jambazi maana yake unaitafuta pesa na hutoipata milele na hata Kama utaipata Basi itakutoroka ghafla, hii ndio sababu ya watu wanaoitafuta pesa kutumia nguvu nyingi yumkini hata kuua ili kuipata pesa na kuangukia kwenye majanga makubwa maishani.
 
Ujafanikiwa au hujafanikiwa?
 
Hivi unajua maana ya Utafiti? hiyo ndio result ya utafiti? sample iko wapi? idadi ya watu waliofanyiwa huo utafiti iko wapi? kwa location ipi? kumbe umecopy tu hapo ukaanzisha na uzi?
Utafiti ni mchakato wa kukusanya, kuchambua, na kutafsiri taarifa

Kwanza kabisa, utafiti huu unategemea simulation uliofanywa na Alessandro Pluchino na wenzake, unaochunguza jinsi bahati inavyoathiri wealth distribution

Kwa undani zaidi, utafiti huu unaonyesha kuwa watu wenye vipaji vya wastani mara nyingi wanaweza kufanikiwa sana ikiwa bahati inawasaidia.

Matokeo haya yametokana na mchakato wa kisayansi wa kuiga mifumo ya kijamii, na si tafiti za moja kwa moja kwa watu wa kweli, bali ni mbinu iliyothibitisha dhana za kitabia na kiuchumi.

Kwa maelezo yote unayoyahitaji, nimeambatanisha vyanzo vyote vya utafiti:

1 Utafiti wa msingi unapatikana kwenye jukwaa la kitaaluma la arXiv:
Soma Utafiti Kamili Hapa

https://arxiv.org/abs/1802.07068

2 Muhtasari wa kitaalamu wa MIT Technology Review ambao unatoa maelezo ya jinsi bahati inaweza kuwa kiini cha mafanikio:
Soma Makala ya MIT Technology Review Hapa

If you’re so smart, why aren’t you rich? Turns out it’s just chance.

3 Uchambuzi wa kina kutoka kwa Scientific American ambao unachambua nafasi ya bahati kwenye maisha:
Soma Makala ya Scientific American Hapa

The Role of Luck in Life Success Is Far Greater Than We Realized

Hivyo, maswali yako yote kuhusu idadi ya sampuli, maeneo, na njia za uchambuzi yamejibiwa ndani ya rasilimali hizi. Nakualika usome ili kupata uelewa wa kina. 😊
 

Attachments

Nadhani labda neno sahihi kwa muktadha wa hoja yangu ni "hujafanikiwa," na si "ujafanikiwa."
Naam.

Kwani kufanikiwa ni lazima kuwa tajiri?

Kama mtu kwao wana historia ya usomi, tangu mdogo ametaka kuwa mwalimu atakayeelimisha jamii, hilo ndilo lengo lake kubwa kuliko hata utajiri, akiweza kufundisha wagu wengi sana akaelimisha jamii bila ya kuwa tajiri, huyo kafanikiwa au hajafanikiwa?
 
Mafanikio hayana maana objective. Bali ni highly subjective na kila mtu ana maana yake. Na inategemea unaongelea akili za aina gani sababu watu hutofautiana orientation na matumizi. Wengine huwekeza kwenye utafutaji wa mali/utajiri, wengine huwekeza kwenye academic endeavors na wengine wapate tu kuishi maisha peaceful. Hiyo list ni infinity.

From their point of view wote wamefanikiwa.
 
Kwani kufanikiwa ni lazima kuwa tajiri?
Hapana, mafanikio siyo lazima kuwa tajiri wa kifedha. Ingawa utajiri unaweza kuwa kipimo cha mafanikio kwa wengi, kila mtu ana mtazamo wake kuhusu mafanikio.
Mafanikio yanaweza kumaanisha kutimiza malengo yako, na sio lazima malengo hayo yawe ya kifedha.

Kama mtu kwao wana historia ya usomi, tangu mdogo ametaka kuwa mwalimu atakayeelimisha jamii, hilo ndilo lengo lake kubwa kuliko hata utajiri, akiweza kufundisha wagu wengi sana akaelimisha jamii bila ya kuwa tajiri, huyo kafanikiwa au hajafanikiwa?
Mfano, umesema kama mtu ambaye alikusudia kuwa mwalimu na alitimiza lengo lake la kuelimisha jamii, hata kama hajapata utajiri, amefanikiwa kwa kutimiza malengo yake na kuwa na athari chanya kwa wengine.

kama vile watu maarufu kama Einstein au Tesla walivyofanikiwa kwa kutimiza malengo yao na kuwa na athari kubwa kwa dunia, hata kama hawakuwa tajiri kwa kiwango cha kifedha.

hoja yangu mimi Mafanikio na Bahati

Mafanikio ya kifedha mara nyingi yanategemea zaidi bahati na fursa. Hata watu wenye kipaji na juhudi wanahitaji nafasi nzuri au matukio ya bahati ili kufanikiwa. Kwa hiyo, bahati na fursa zina mchango mkubwa katika mafanikio hayo.

"If you’re so smart, why aren’t you rich? Turns out it’s just chance."
 
Kuzaliwa kwenyewe ni bahati, hakuna mtu anayezaliwa kwa kupanga.

Na bila kuzaliwa huwezi kuwa tajiri.

Wazazi watakaokuzaa ni bahati, hakuna mtu anayepanga azaliwe na wazazi gani.

Na ukichunguza wazazi wanaokuzaa wana mchango mkubwa wa kutufanya uwe tajiri ama la.

Nchi uliyozaliwa ni bahati, hakuna mtu anayepanga atazaliwa nchi gani. Na kuna nchi ukizaliwa una nafasi ndogo ya kuwa tajiri, wakati nchi nyingine ulizaliwa huko nafasi za kuwa tajiri ni kubwa.

Mwaka uliozaliwa ni bahati, hakuna mtu anayepanga mwaka atakaozaliwa. Na kuna miaka imepita huko umasikini ulikuwa mwingi sana, na kadiri tulivyojiongwza miaka ilivyiwndelea fursa zimeongezeka.

Sasa, ukiangalia mambo mengi haya yanayiendana na nahati, itakataaje sehemu ya bahati katika utajiri?

Nakibali hata wenye bahati pengine huifanyia kazi iki wajenge utajiri, lakini huwezi kuondoa kabisa sehemu ya bahati katika utajiri.
 
Na wewe umeamini hayo? Bahati ni imani tu.
 
Mleta mada hujawa SMART(Specific Measurable Attainable Realistic Time bounded ).Huyo genius ni smart katika eneo fulani na si nyanja zote.Hata ushirikina wapo watu smart..
 
Na hakuna Siri kwa tajiri yaan tajiri hana Siri, pigia mstari msipumbazwe na maneno ya kuokoteza matajiri hawana siri wana Wasiri na hao wasiri ndio wanaowatunzia Siri, tajiri hana Siri bali anao watu wanaomtunzia Siri
Kama anatunziwa siri na wengine hiyo siyo siri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…