Kama wewe ni smart na una akili, kwanini hujafanikiwa kuwa Tajiri? Inageukia kwamba wewe ni mjinga

Kama wewe ni smart na una akili, kwanini hujafanikiwa kuwa Tajiri? Inageukia kwamba wewe ni mjinga

Bahati haina nafasi, kila kitu hutokea kwa sababu maalum, mfano ukiokota hela sio bahati ila unastahili kwasababu ulipita njiani na ukaangaza macho ukaiona

hao wakina BIll gate ndyo usiwatolee mifano kabisa, utajiri au pesa zao hazijaja kwa bahati mbaya bali juhudi na mipango yao binafsi.
Duniani hakuna bahati.
 
Humu jf tajiri niko pekeangu naona wengi wananiongelea mimi tu

Ni hivi uthubutu na nidham ya pesa ndio kila kitu kwenye tasnia ya utajiri akili uwe nazo tu za kung'amua yaani usiwe kichaa tu basi umemaliza
 
Chukulia umelima mahindi huo mwaka ukapata mazao mengi halafu wenzio wakapigwa na ukame bei ikpaa juu ukapiga hela.
Umelima mahindi, huo mwaka mvua zakanyesha mazao yakanawiri kila kona, bei ikashuka ukauza kwa hasara.Je hayo matukio yana ashiria bahati au akuli ?
Ni ujinga huwezi Lima kwa kutegemea mvua.
Na endapo utapata Basi itakuwa kwa bahati.
 
Unafanyaje pesa ikutafute?
Yes, pesa ipo kila mahali na kila unayemwona Ni pesa hiyo hivyo Basi unatakiwa kuweka vipendwa vitakavyosababisha pesa ikutafute.

Mfano rahisi fundi uashi unapojenga kwa ufanisi wa hali ya juu kiasi Cha kuwa attract watu kukuulizia, Basi hapo jua inakuulizia pesa au pesa inakutafuta.
Lkn ukiwa jambazi maana yake unaitafuta pesa na hutoipata milele na hata Kama utaipata Basi itakutoroka ghafla, hii ndio sababu ya watu wanaoitafuta pesa kutumia nguvu nyingi yumkini hata kuua ili kuipata pesa na kuangukia kwenye majanga makubwa maishani.
 
Hii inamaanisha kuwa mafanikio hayategemei tu akili au maarifa, bali pia ni matokeo ya jinsi tunavyoweza kuchangia au kuhusika katika mazingira yanayotoa fursa.

Hivyo, iko wazi kuwa mafanikio ya kifedha mara nyingi ni matokeo ya mchanganyiko wa talanta, juhudi, lakini pia ni matokeo ya fursa, wakati, na hata mazingira ya kijamii.

Kama unajiuliza kwanini haujafanikiwa kuwa tajiri licha ya kuwa na akili, inaweza kuwa kwamba hujapata nafasi nzuri au umekosa sehemu muhimu ya bahati inayohitajika kufanikiwa.

Je, unakubaliana kuwa bahati na mazingira vina nafasi kubwa kwenye mafanikio?
Ujafanikiwa au hujafanikiwa?
 
Hivi unajua maana ya Utafiti? hiyo ndio result ya utafiti? sample iko wapi? idadi ya watu waliofanyiwa huo utafiti iko wapi? kwa location ipi? kumbe umecopy tu hapo ukaanzisha na uzi?
Utafiti ni mchakato wa kukusanya, kuchambua, na kutafsiri taarifa

Kwanza kabisa, utafiti huu unategemea simulation uliofanywa na Alessandro Pluchino na wenzake, unaochunguza jinsi bahati inavyoathiri wealth distribution

Kwa undani zaidi, utafiti huu unaonyesha kuwa watu wenye vipaji vya wastani mara nyingi wanaweza kufanikiwa sana ikiwa bahati inawasaidia.

Matokeo haya yametokana na mchakato wa kisayansi wa kuiga mifumo ya kijamii, na si tafiti za moja kwa moja kwa watu wa kweli, bali ni mbinu iliyothibitisha dhana za kitabia na kiuchumi.

Kwa maelezo yote unayoyahitaji, nimeambatanisha vyanzo vyote vya utafiti:

1 Utafiti wa msingi unapatikana kwenye jukwaa la kitaaluma la arXiv:
Soma Utafiti Kamili Hapa
1733168973510.png

https://arxiv.org/abs/1802.07068

2 Muhtasari wa kitaalamu wa MIT Technology Review ambao unatoa maelezo ya jinsi bahati inaweza kuwa kiini cha mafanikio:
Soma Makala ya MIT Technology Review Hapa
1733170423931.png

If you’re so smart, why aren’t you rich? Turns out it’s just chance.

3 Uchambuzi wa kina kutoka kwa Scientific American ambao unachambua nafasi ya bahati kwenye maisha:
Soma Makala ya Scientific American Hapa
1733170497574.png

The Role of Luck in Life Success Is Far Greater Than We Realized

Hivyo, maswali yako yote kuhusu idadi ya sampuli, maeneo, na njia za uchambuzi yamejibiwa ndani ya rasilimali hizi. Nakualika usome ili kupata uelewa wa kina. 😊
 
Attachments

Nadhani labda neno sahihi kwa muktadha wa hoja yangu ni "hujafanikiwa," na si "ujafanikiwa."
Naam.

Kwani kufanikiwa ni lazima kuwa tajiri?

Kama mtu kwao wana historia ya usomi, tangu mdogo ametaka kuwa mwalimu atakayeelimisha jamii, hilo ndilo lengo lake kubwa kuliko hata utajiri, akiweza kufundisha wagu wengi sana akaelimisha jamii bila ya kuwa tajiri, huyo kafanikiwa au hajafanikiwa?
 
Mafanikio hayana maana objective. Bali ni highly subjective na kila mtu ana maana yake. Na inategemea unaongelea akili za aina gani sababu watu hutofautiana orientation na matumizi. Wengine huwekeza kwenye utafutaji wa mali/utajiri, wengine huwekeza kwenye academic endeavors na wengine wapate tu kuishi maisha peaceful. Hiyo list ni infinity.

From their point of view wote wamefanikiwa.
 
Kwani kufanikiwa ni lazima kuwa tajiri?
Hapana, mafanikio siyo lazima kuwa tajiri wa kifedha. Ingawa utajiri unaweza kuwa kipimo cha mafanikio kwa wengi, kila mtu ana mtazamo wake kuhusu mafanikio.
Mafanikio yanaweza kumaanisha kutimiza malengo yako, na sio lazima malengo hayo yawe ya kifedha.

Kama mtu kwao wana historia ya usomi, tangu mdogo ametaka kuwa mwalimu atakayeelimisha jamii, hilo ndilo lengo lake kubwa kuliko hata utajiri, akiweza kufundisha wagu wengi sana akaelimisha jamii bila ya kuwa tajiri, huyo kafanikiwa au hajafanikiwa?
Mfano, umesema kama mtu ambaye alikusudia kuwa mwalimu na alitimiza lengo lake la kuelimisha jamii, hata kama hajapata utajiri, amefanikiwa kwa kutimiza malengo yake na kuwa na athari chanya kwa wengine.

kama vile watu maarufu kama Einstein au Tesla walivyofanikiwa kwa kutimiza malengo yao na kuwa na athari kubwa kwa dunia, hata kama hawakuwa tajiri kwa kiwango cha kifedha.

hoja yangu mimi Mafanikio na Bahati

Mafanikio ya kifedha mara nyingi yanategemea zaidi bahati na fursa. Hata watu wenye kipaji na juhudi wanahitaji nafasi nzuri au matukio ya bahati ili kufanikiwa. Kwa hiyo, bahati na fursa zina mchango mkubwa katika mafanikio hayo.

"If you’re so smart, why aren’t you rich? Turns out it’s just chance."
 
Hapana, mafanikio siyo lazima kuwa tajiri wa kifedha. Ingawa utajiri unaweza kuwa kipimo cha mafanikio kwa wengi, kila mtu ana mtazamo wake kuhusu mafanikio.
Mafanikio yanaweza kumaanisha kutimiza malengo yako, na sio lazima malengo hayo yawe ya kifedha.

Mfano, umesema kama mtu ambaye alikusudia kuwa mwalimu na alitimiza lengo lake la kuelimisha jamii, hata kama hajapata utajiri, amefanikiwa kwa kutimiza malengo yake na kuwa na athari chanya kwa wengine.

kama vile watu maarufu kama Einstein au Tesla walivyofanikiwa kwa kutimiza malengo yao na kuwa na athari kubwa kwa dunia, hata kama hawakuwa tajiri kwa kiwango cha kifedha.

hoja yangu mimi Mafanikio na Bahati

Mafanikio ya kifedha mara nyingi yanategemea zaidi bahati na fursa. Hata watu wenye kipaji na juhudi wanahitaji nafasi nzuri au matukio ya bahati ili kufanikiwa. Kwa hiyo, bahati na fursa zina mchango mkubwa katika mafanikio hayo.

"If you’re so smart, why aren’t you rich? Turns out it’s just chance."
Kuzaliwa kwenyewe ni bahati, hakuna mtu anayezaliwa kwa kupanga.

Na bila kuzaliwa huwezi kuwa tajiri.

Wazazi watakaokuzaa ni bahati, hakuna mtu anayepanga azaliwe na wazazi gani.

Na ukichunguza wazazi wanaokuzaa wana mchango mkubwa wa kutufanya uwe tajiri ama la.

Nchi uliyozaliwa ni bahati, hakuna mtu anayepanga atazaliwa nchi gani. Na kuna nchi ukizaliwa una nafasi ndogo ya kuwa tajiri, wakati nchi nyingine ulizaliwa huko nafasi za kuwa tajiri ni kubwa.

Mwaka uliozaliwa ni bahati, hakuna mtu anayepanga mwaka atakaozaliwa. Na kuna miaka imepita huko umasikini ulikuwa mwingi sana, na kadiri tulivyojiongwza miaka ilivyiwndelea fursa zimeongezeka.

Sasa, ukiangalia mambo mengi haya yanayiendana na nahati, itakataaje sehemu ya bahati katika utajiri?

Nakibali hata wenye bahati pengine huifanyia kazi iki wajenge utajiri, lakini huwezi kuondoa kabisa sehemu ya bahati katika utajiri.
 
Utafiti ni mchakato wa kukusanya, kuchambua, na kutafsiri taarifa

Kwanza kabisa, utafiti huu unategemea simulation uliofanywa na Alessandro Pluchino na wenzake, unaochunguza jinsi bahati inavyoathiri wealth distribution

Kwa undani zaidi, utafiti huu unaonyesha kuwa watu wenye vipaji vya wastani mara nyingi wanaweza kufanikiwa sana ikiwa bahati inawasaidia.

Matokeo haya yametokana na mchakato wa kisayansi wa kuiga mifumo ya kijamii, na si tafiti za moja kwa moja kwa watu wa kweli, bali ni mbinu iliyothibitisha dhana za kitabia na kiuchumi.

Kwa maelezo yote unayoyahitaji, nimeambatanisha vyanzo vyote vya utafiti:

1 Utafiti wa msingi unapatikana kwenye jukwaa la kitaaluma la arXiv:
Soma Utafiti Kamili Hapa
View attachment 3167614
[1802.07068] Talent vs Luck: the role of randomness in success and failure

2 Muhtasari wa kitaalamu wa MIT Technology Review ambao unatoa maelezo ya jinsi bahati inaweza kuwa kiini cha mafanikio:
Soma Makala ya MIT Technology Review Hapa
View attachment 3167640
If you’re so smart, why aren’t you rich? Turns out it’s just chance.

3 Uchambuzi wa kina kutoka kwa Scientific American ambao unachambua nafasi ya bahati kwenye maisha:
Soma Makala ya Scientific American Hapa
View attachment 3167642
The Role of Luck in Life Success Is Far Greater Than We Realized

Hivyo, maswali yako yote kuhusu idadi ya sampuli, maeneo, na njia za uchambuzi yamejibiwa ndani ya rasilimali hizi. Nakualika usome ili kupata uelewa wa kina. 😊
Na wewe umeamini hayo? Bahati ni imani tu.
 
Mleta mada hujawa SMART(Specific Measurable Attainable Realistic Time bounded ).Huyo genius ni smart katika eneo fulani na si nyanja zote.Hata ushirikina wapo watu smart..
 
Na hakuna Siri kwa tajiri yaan tajiri hana Siri, pigia mstari msipumbazwe na maneno ya kuokoteza matajiri hawana siri wana Wasiri na hao wasiri ndio wanaowatunzia Siri, tajiri hana Siri bali anao watu wanaomtunzia Siri
Kama anatunziwa siri na wengine hiyo siyo siri
 
Back
Top Bottom