Uchaguzi 2020 Kama wewe sio dhaifu kwanini utafute kupendelewa?

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
MTU DHAIFU HUTAFUTA UPENDELEO; JE LISU ANAPAMBANA NA MTU DHAIFU?

Na, Robert Heriel

Kikawaida watu dhaifu hutafuta kupendelewa, hutafuta dezo kwa watu. Pia kikawaida watu dhaifu ndio hupewa upendeleo na huukubali huo upendeleo kwa kuwa wanajua hawastahili.

Hii ni tofauti na mtu hodari. Mtu hodari hapendi kupendelewa, hapendi dezo, na wala hatafuti upendeleo kwani anajiamini kuwa yeye ni hodari, anauwezo, na ni mahiri katika jambo fulani hivyo anastahili.

Tulipokuwa wadogo ndani ya familia, hasa yenye watoto kuanzia wawili wanaokaribiana. Ni kawaida kuona yule mdogo(dhaifu) akiwa mchokozi, na hata ikitokea wakipigana mdogo anajua wazi kabisa wazazi(hasa Mama) atamtetea yeye. Hata kwenye chakula au zawaid ni kawaida mdogo(dhaifu) kupewa upendeleo maalumu na wazazi. Hiii ni kumfanya mtoto aliyemdogo kujisikia vyema.

Mfano wa pili;
Wale tuliosoma tutakubaliana kuwa, wanafunzi wengi wanaotafuta kuvujishiwa mitihani na waalimu ni wale wanafunzi dhaifu. Hata mwalimu anapovujisha mtihani hufanya hivyo kwa kujua wazi kuwa wanafunzi wake ni vilaza, dhaifu, hawajajiandaa vyakutoha. Hivyo huwapa upendeleo wa kuwaonyesha mtihani kabla ya muda wa mtihani kufika.

Kwa asilimia 90% Upendeleo huvunja haki. Watu wote waliopendelewa walivunja haki za wengine. Kupendelewa ni matokeo ya kutokujiamini, kudharauliwa, kutokustahili.

Hata Makazini wale wote wanaotafuta upendeleo wengi wao hawastahili, sio mahiri, hawajiamini, na wengi ni wapenda Rushwa. Hii huwafanya kujipendekeza kwa Boss ili kupewa upendeleo maalumu.

Watu hodari na mahiri huwa hawatafuti kupendelewa. Wanajua yakuwa wao ni bora. Wanajua kuwa wao wanajua kupambana katika mazingira yoyote yale bila kujali. Hawana muda wa kutumia uhalifu, uovu, hila au njama kujitangaza au kuhitaji kukubalika.

Kwenye michezo, hasa mpira, ni kawaida timu dhaifu kuomba upendeleo kwa Refa. Hii husababisha kumnunua Refa na wale Kamisaa. Timu inayojiamini,bora na mahiri haiwezi kutafuta upendeleo kwa refa.

Mtu bora hujisikia aibu pale anapopendelewa. Mtu hodari hujisikia kaabishwa pale anapohisi anapendelewa yaani hashindi kihalali, yaani hana uwezo wa kushinda kulingana na sheria za mchezo, bali hila, njama, figisu figisu ndizo zitamfanya ashinde.

Lakini Mtu dhaifu huchekelea pale anapopendelewa, anaona ni kawaida kufanya hila au njama, au figisu figisu ili kutimiza ushindi bandia.

Mtu dhaifu baada ya kupendelewa ni lazima aanze maisha ya Uongo, ulaghai na utapeli. Watu wote waliopendelewa huwa ndio mwanzo wa kutapeli na kulaghai watu ili kuwafanya waone ni kweli anastahili ushindi.

Tundu Lisu ni Hodari, hahitaji upendeleo(Hila, njama, Figisu Figisu) Ili ashinde. Watu kama Tundu Lisu nilishasemaga ni heavy Weight katika mapambano. Ni shujaa kama Goliath, anauzoefu wa vita, sio kama Daudi ambaye alipewa upendeleo na Mungu kwenye pambano lake na Goliath.

Watu hodari, mashujaa ndio hufanyiwa hila, njama, figisu Figisu ili washindwe. Huwezi mfanyia Figisu Figisu mtu dhaifu wakati unajua hana uwezo wa kukushinda. Na huwezi mpendelea mtu ambaye unauhakika kabisa anauwezo wa kushinda.

Washindi hawapewagi upendeleo, bali huwekewa hila, njama, Figisu Figisu ili wasishinde.

Sisemi kuwa Lisu hana madhaifu mengine, Hasha! Lisu ni mwanadamu kama wanadamu wengine. Lakini itoshe kusema kuwa anapambana na Mtu dhaifu wakati yeye ni shujaa.

Kama wangekuwa wanalingana uzani. Basi mmoja asingependelewa. Na kama mpambanaji anayepambana na Lisu angekuwa anajiamini angesema kwa ushujaa kabisa hivi: , nataka nipigane naye kavu kavu, huyu hanishindi kwa vyovyote. Lakini udhaifu ndio hupelekea mtu kutumia silaha.

Hujawahi ona hata kwenye vita wanapokutana wababe, basi utaona wote wanatupa silaha, wanasema tupigana kavu kavu kama unajiamini. Na kweli wote wanatupa silaha na ngumi zinaanza kuchapwa. Mpaka kidume apatikane.

Hivi ni kweli Tundu Lisu ni hodari kiasi hiki mpaka apatiwe nafasi ya kuonyesha uwezo wake na ushujaa wake?
Unajua Lisu anapambana Kavu Kavu na mtu anayetumia silaha(Hila, njama, Figisu Figisu) ambapo ni kinyume na mchezo wa mapambano.

Ni sawa na shuleni, mwanafunzi kipanga ambaye hajavujishiwa mtihani afanye mtihani na mwanafunzi aliyevujishiwa mtihani. Hata kama mwanafunzi aliyevujishiwa mtihani atafaulu lakini bado atakuwa ni kilaza tuu na yeye mwenyewe anajua hivyo.

Watu Dhaifu hutafuta kupendelewa. Lakini wanajijua wazi kabisa uwezo ni mdogo bila hila, njama na figisu figisu.

Makala hii inaweza kutumika katika nyanja zote za maisha. Nafahamu hata hapo ulipo huenda unapambana na mtu unayemuweza kabisa lakini anapendelewa, iwe ni ofisini, kwenye biashara, shuleni, chuoni, mpirani, masumbwi n.k

KUMBUKA: Tundu Lisu ametumika kama kiwakilishi cha watu majasiri, hodari, shujaa na mahiri. Huenda ni wewe au mtu mwingine.

Mtu dhaifu ametumika kama kiwakilishi cha watu wote mnaopenda kupendelewa kutokana na udhaifu wenu wa kuwa na uwezo mdogo.

Swali Muhimu:
Kama wewe sio dhaifu kwani utafute kupendelewa?

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
 
Hongera Robert huwa unaandika vizuri sana makala zako.

Mgombea Urais CCM aliwaambia wakurugenzi ambao ndio wasimamizi wa Uchaguzi.

Mimi nakupa kazi.
Nakupa mshahara.
Nakupa gari zuri.
Nakupa posho.
Nakupa nyumba
Alafu bado unakwenda kumtangaza mpinzani???????

Huyu mtu ni DHAIFU haamini katika ushindani,Uchaguzi, demokrasia na utu
Huwa anajiita Kichaa Au Jiwe.
 
Mtu jasili na hodari umemutaja kwa jina ila hujatutajia jina la mutu Zaifu,, tufanye makasiriko?
 
Umeandika vizuri sana ila CHADEMA sio majasiri ata kidogo, ni majasiri kwa wapumbavu na wasiojielewa, huwezi kupinga kitu ulichokitaka kisa kimetekelezwa na mwingine, mi sio mwanasiasa ila mtu mwenye akili timamu aliwaona hawa ni wasanii tangu 2015
 
Hongera Robert huwa unaandika vizuri sana makala zako.

Mgombea Urais CCM aliwaambia wakurugenzi ambao ndio wasimamizi wa Uchaguzi.

Mimi nakupa kazi.
Nakupa mshahara.
Nakupa gari zuri.
Nakupa posho.
Nakupa nyumba
Alafu bado unakwenda kumtangaza mpinzani???????

Huyu mtu ni DHAIFU haamini katika ushindani,Uchaguzi, demokrasia na utu
Huwa anajiita Kichaa Au Jiwe.
Pia yafaa Kama taifa ,Kama shida no Sheria zetu,tuiboreshe Sheria ya kupambana na rushwa,kwani hiyo no rushes dhahiri kabisa.Ndio maana Kariba mpya wanaipinga kwa nguvu zote.
 
MTU DHAIFU HUTAFUTA UPENDELEO; JE LISU ANAPAMBANA NA MTU DHAIFU?

Na, Robert Heriel

Kikawaida watu dhaifu hutafuta kupendelewa, hutafuta dezo kwa watu. Pia kikawaida watu dhaifu ndio hupewa upendeleo na huukubali huo upendeleo kwa kuwa wanajua hawastahili.

Hii ni tofauti na mtu hodari. Mtu hodari hapendi kupendelewa, hapendi dezo, na wala hatafuti upendeleo kwani anajiamini kuwa yeye ni hodari, anauwezo, na ni mahiri katika jambo fulani hivyo anastahili.

Tulipokuwa wadogo ndani ya familia, hasa yenye watoto kuanzia wawili wanaokaribiana. Ni kawaida kuona yule mdogo(dhaifu) akiwa mchokozi, na hata ikitokea wakipigana mdogo anajua wazi kabisa wazazi(hasa Mama) atamtetea yeye. Hata kwenye chakula au zawaid ni kawaida mdogo(dhaifu) kupewa upendeleo maalumu na wazazi. Hiii ni kumfanya mtoto aliyemdogo kujisikia vyema.

Mfano wa pili;
Wale tuliosoma tutakubaliana kuwa, wanafunzi wengi wanaotafuta kuvujishiwa mitihani na waalimu ni wale wanafunzi dhaifu. Hata mwalimu anapovujisha mtihani hufanya hivyo kwa kujua wazi kuwa wanafunzi wake ni vilaza, dhaifu, hawajajiandaa vyakutoha. Hivyo huwapa upendeleo wa kuwaonyesha mtihani kabla ya muda wa mtihani kufika.

Kwa asilimia 90% Upendeleo huvunja haki. Watu wote waliopendelewa walivunja haki za wengine. Kupendelewa ni matokeo ya kutokujiamini, kudharauliwa, kutokustahili.

Hata Makazini wale wote wanaotafuta upendeleo wengi wao hawastahili, sio mahiri, hawajiamini, na wengi ni wapenda Rushwa. Hii huwafanya kujipendekeza kwa Boss ili kupewa upendeleo maalumu.

Watu hodari na mahiri huwa hawatafuti kupendelewa. Wanajua yakuwa wao ni bora. Wanajua kuwa wao wanajua kupambana katika mazingira yoyote yale bila kujali. Hawana muda wa kutumia uhalifu, uovu, hila au njama kujitangaza au kuhitaji kukubalika.

Kwenye michezo, hasa mpira, ni kawaida timu dhaifu kuomba upendeleo kwa Refa. Hii husababisha kumnunua Refa na wale Kamisaa. Timu inayojiamini,bora na mahiri haiwezi kutafuta upendeleo kwa refa.

Mtu bora hujisikia aibu pale anapopendelewa. Mtu hodari hujisikia kaabishwa pale anapohisi anapendelewa yaani hashindi kihalali, yaani hana uwezo wa kushinda kulingana na sheria za mchezo, bali hila, njama, figisu figisu ndizo zitamfanya ashinde.

Lakini Mtu dhaifu huchekelea pale anapopendelewa, anaona ni kawaida kufanya hila au njama, au figisu figisu ili kutimiza ushindi bandia.

Mtu dhaifu baada ya kupendelewa ni lazima aanze maisha ya Uongo, ulaghai na utapeli. Watu wote waliopendelewa huwa ndio mwanzo wa kutapeli na kulaghai watu ili kuwafanya waone ni kweli anastahili ushindi.

Tundu Lisu ni Hodari, hahitaji upendeleo(Hila, njama, Figisu Figisu) Ili ashinde. Watu kama Tundu Lisu nilishasemaga ni heavy Weight katika mapambano. Ni shujaa kama Goliath, anauzoefu wa vita, sio kama Daudi ambaye alipewa upendeleo na Mungu kwenye pambano lake na Goliath.

Watu hodari, mashujaa ndio hufanyiwa hila, njama, figisu Figisu ili washindwe. Huwezi mfanyia Figisu Figisu mtu dhaifu wakati unajua hana uwezo wa kukushinda. Na huwezi mpendelea mtu ambaye unauhakika kabisa anauwezo wa kushinda.

Washindi hawapewagi upendeleo, bali huwekewa hila, njama, Figisu Figisu ili wasishinde.

Sisemi kuwa Lisu hana madhaifu mengine, Hasha! Lisu ni mwanadamu kama wanadamu wengine. Lakini itoshe kusema kuwa anapambana na Mtu dhaifu wakati yeye ni shujaa.

Kama wangekuwa wanalingana uzani. Basi mmoja asingependelewa. Na kama mpambanaji anayepambana na Lisu angekuwa anajiamini angesema kwa ushujaa kabisa hivi: , nataka nipigane naye kavu kavu, huyu hanishindi kwa vyovyote. Lakini udhaifu ndio hupelekea mtu kutumia silaha.

Hujawahi ona hata kwenye vita wanapokutana wababe, basi utaona wote wanatupa silaha, wanasema tupigana kavu kavu kama unajiamini. Na kweli wote wanatupa silaha na ngumi zinaanza kuchapwa. Mpaka kidume apatikane.

Hivi ni kweli Tundu Lisu ni hodari kiasi hiki mpaka apatiwe nafasi ya kuonyesha uwezo wake na ushujaa wake?
Unajua Lisu anapambana Kavu Kavu na mtu anayetumia silaha(Hila, njama, Figisu Figisu) ambapo ni kinyume na mchezo wa mapambano.

Ni sawa na shuleni, mwanafunzi kipanga ambaye hajavujishiwa mtihani afanye mtihani na mwanafunzi aliyevujishiwa mtihani. Hata kama mwanafunzi aliyevujishiwa mtihani atafaulu lakini bado atakuwa ni kilaza tuu na yeye mwenyewe anajua hivyo.

Watu Dhaifu hutafuta kupendelewa. Lakini wanajijua wazi kabisa uwezo ni mdogo bila hila, njama na figisu figisu.

Makala hii inaweza kutumika katika nyanja zote za maisha. Nafahamu hata hapo ulipo huenda unapambana na mtu unayemuweza kabisa lakini anapendelewa, iwe ni ofisini, kwenye biashara, shuleni, chuoni, mpirani, masumbwi n.k

KUMBUKA: Tundu Lisu ametumika kama kiwakilishi cha watu majasiri, hodari, shujaa na mahiri. Huenda ni wewe au mtu mwingine.

Mtu dhaifu ametumika kama kiwakilishi cha watu wote mnaopenda kupendelewa kutokana na udhaifu wenu wa kuwa na uwezo mdogo.

Swali Muhimu:
Kama wewe sio dhaifu kwani utafute kupendelewa?

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
TUNDU LISSU NI DHAIFU SANA HUONI ANAVYOLIALIA MAJUKWAANIN NA KUWATEGEMEA MATAIFA YA ULAYA KUHALALISHA HILA ZAKE ZA KUTAKA KUHARIBU AMANI YETU MTU HODARI JPM ANAPAMBANA BILA KULIALIA

USIJE MFANANISHA MAGUFULI NA MAMBO YA AJABU....
 
Nafurahi sana nikisoma uzi kama hizi, zina chambua mambo kinagaubaga, Mkuu agiza balimi kumi hapo kwa mangi nakuja kulipa
 
Kaweka na namba kabisa utume bila nakasiriko [emoji851][emoji851][emoji851][emoji851][emoji851][emoji851]
 
Kwenye utawala wake hajaajiri watu wala kuongeza mishahara na madaraja ya watumishi, ajabu anatuomba tumwajiri Tena.

Ingawa siyo vizuri kuwalinganisha hao mahasimu wawili Kama Daudi na Goliath.

Kama Lisu angekuwa Goliath, angekufa kwa risasi (Jiwe) moja kwenye uwanja wa mapambano pale Dodoma.
Tafuta character aliyeibuka mshindi kwenye mapambano ndiye umfananishe na Lissu.
 
Ndo maan tunalia na tume ya kishamba kila siku...
mwenyekiti wa tume anaonesha mahaba yake wazi wazi....
 
Dr Bill subiri 28 October! Aliyemfungia mwenzake asifanye campaign wakati yeye kalala ni nani ????Lissu????? Ama mwenzake??
 
MTU DHAIFU HUTAFUTA UPENDELEO; JE LISU ANAPAMBANA NA MTU DHAIFU?

Na, Robert Heriel

Kikawaida watu dhaifu hutafuta kupendelewa, hutafuta dezo kwa watu. Pia kikawaida watu dhaifu ndio hupewa upendeleo na huukubali huo upendeleo kwa kuwa wanajua hawastahili.

Hii ni tofauti na mtu hodari. Mtu hodari hapendi kupendelewa, hapendi dezo, na wala hatafuti upendeleo kwani anajiamini kuwa yeye ni hodari, anauwezo, na ni mahiri katika jambo fulani hivyo anastahili.

Tulipokuwa wadogo ndani ya familia, hasa yenye watoto kuanzia wawili wanaokaribiana. Ni kawaida kuona yule mdogo(dhaifu) akiwa mchokozi, na hata ikitokea wakipigana mdogo anajua wazi kabisa wazazi(hasa Mama) atamtetea yeye. Hata kwenye chakula au zawaid ni kawaida mdogo(dhaifu) kupewa upendeleo maalumu na wazazi. Hiii ni kumfanya mtoto aliyemdogo kujisikia vyema.

Mfano wa pili;
Wale tuliosoma tutakubaliana kuwa, wanafunzi wengi wanaotafuta kuvujishiwa mitihani na waalimu ni wale wanafunzi dhaifu. Hata mwalimu anapovujisha mtihani hufanya hivyo kwa kujua wazi kuwa wanafunzi wake ni vilaza, dhaifu, hawajajiandaa vyakutoha. Hivyo huwapa upendeleo wa kuwaonyesha mtihani kabla ya muda wa mtihani kufika.

Kwa asilimia 90% Upendeleo huvunja haki. Watu wote waliopendelewa walivunja haki za wengine. Kupendelewa ni matokeo ya kutokujiamini, kudharauliwa, kutokustahili.

Hata Makazini wale wote wanaotafuta upendeleo wengi wao hawastahili, sio mahiri, hawajiamini, na wengi ni wapenda Rushwa. Hii huwafanya kujipendekeza kwa Boss ili kupewa upendeleo maalumu.

Watu hodari na mahiri huwa hawatafuti kupendelewa. Wanajua yakuwa wao ni bora. Wanajua kuwa wao wanajua kupambana katika mazingira yoyote yale bila kujali. Hawana muda wa kutumia uhalifu, uovu, hila au njama kujitangaza au kuhitaji kukubalika.

Kwenye michezo, hasa mpira, ni kawaida timu dhaifu kuomba upendeleo kwa Refa. Hii husababisha kumnunua Refa na wale Kamisaa. Timu inayojiamini,bora na mahiri haiwezi kutafuta upendeleo kwa refa.

Mtu bora hujisikia aibu pale anapopendelewa. Mtu hodari hujisikia kaabishwa pale anapohisi anapendelewa yaani hashindi kihalali, yaani hana uwezo wa kushinda kulingana na sheria za mchezo, bali hila, njama, figisu figisu ndizo zitamfanya ashinde.

Lakini Mtu dhaifu huchekelea pale anapopendelewa, anaona ni kawaida kufanya hila au njama, au figisu figisu ili kutimiza ushindi bandia.

Mtu dhaifu baada ya kupendelewa ni lazima aanze maisha ya Uongo, ulaghai na utapeli. Watu wote waliopendelewa huwa ndio mwanzo wa kutapeli na kulaghai watu ili kuwafanya waone ni kweli anastahili ushindi.

Tundu Lisu ni Hodari, hahitaji upendeleo(Hila, njama, Figisu Figisu) Ili ashinde. Watu kama Tundu Lisu nilishasemaga ni heavy Weight katika mapambano. Ni shujaa kama Goliath, anauzoefu wa vita, sio kama Daudi ambaye alipewa upendeleo na Mungu kwenye pambano lake na Goliath.

Watu hodari, mashujaa ndio hufanyiwa hila, njama, figisu Figisu ili washindwe. Huwezi mfanyia Figisu Figisu mtu dhaifu wakati unajua hana uwezo wa kukushinda. Na huwezi mpendelea mtu ambaye unauhakika kabisa anauwezo wa kushinda.

Washindi hawapewagi upendeleo, bali huwekewa hila, njama, Figisu Figisu ili wasishinde.

Sisemi kuwa Lisu hana madhaifu mengine, Hasha! Lisu ni mwanadamu kama wanadamu wengine. Lakini itoshe kusema kuwa anapambana na Mtu dhaifu wakati yeye ni shujaa.

Kama wangekuwa wanalingana uzani. Basi mmoja asingependelewa. Na kama mpambanaji anayepambana na Lisu angekuwa anajiamini angesema kwa ushujaa kabisa hivi: , nataka nipigane naye kavu kavu, huyu hanishindi kwa vyovyote. Lakini udhaifu ndio hupelekea mtu kutumia silaha.

Hujawahi ona hata kwenye vita wanapokutana wababe, basi utaona wote wanatupa silaha, wanasema tupigana kavu kavu kama unajiamini. Na kweli wote wanatupa silaha na ngumi zinaanza kuchapwa. Mpaka kidume apatikane.

Hivi ni kweli Tundu Lisu ni hodari kiasi hiki mpaka apatiwe nafasi ya kuonyesha uwezo wake na ushujaa wake?
Unajua Lisu anapambana Kavu Kavu na mtu anayetumia silaha(Hila, njama, Figisu Figisu) ambapo ni kinyume na mchezo wa mapambano.

Ni sawa na shuleni, mwanafunzi kipanga ambaye hajavujishiwa mtihani afanye mtihani na mwanafunzi aliyevujishiwa mtihani. Hata kama mwanafunzi aliyevujishiwa mtihani atafaulu lakini bado atakuwa ni kilaza tuu na yeye mwenyewe anajua hivyo.

Watu Dhaifu hutafuta kupendelewa. Lakini wanajijua wazi kabisa uwezo ni mdogo bila hila, njama na figisu figisu.

Makala hii inaweza kutumika katika nyanja zote za maisha. Nafahamu hata hapo ulipo huenda unapambana na mtu unayemuweza kabisa lakini anapendelewa, iwe ni ofisini, kwenye biashara, shuleni, chuoni, mpirani, masumbwi n.k

KUMBUKA: Tundu Lisu ametumika kama kiwakilishi cha watu majasiri, hodari, shujaa na mahiri. Huenda ni wewe au mtu mwingine.

Mtu dhaifu ametumika kama kiwakilishi cha watu wote mnaopenda kupendelewa kutokana na udhaifu wenu wa kuwa na uwezo mdogo.

Swali Muhimu:
Kama wewe sio dhaifu kwani utafute kupendelewa?

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300

Cc: Paskali Mayalla, kipande, mwengeso, igunduge, yehodaya, kipande, crimea, barbarosa, nyani ngabu,
 
[emoji125][emoji125][emoji125] dhaifu
 
Back
Top Bottom