Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hata mimi hawaniogopi, naweza nikawa nje nimekaa wakawa pembeni yangu ila akitokea mtu mwingine wanaondoka,Daah umefanya jambo ambalo jamaa mmoja aliwahi fanya kule Yombo dovya miaka ya nyuma sana mpaka wakawa wanamwita kwa Kunguru maana aliweka sehemu ya maji na chakula na alikua kama amewafundisha awazagai hovyo wala kwenda sehemu ingine na pia nilishangaa kuona hawaogopi watu kabisaa...
Vitambaa vya kuchujia maji vikianikwa inje kunguru wanapenda kuvikanyaga na kuvinyea ....na watu wengi hawajashitukia hilo wanakwenda chujia maji pasipo kujuaNilikuwa napiga stor na jamaa zangu wa arusha nikawaambia jinsi hawa kunguru wanavofungua koki ya maji na kuyaacha yamwagike, kila mtu aliniona ni muongo...
Tutapewa bajeti ya billion kumi kuwateketeza na tenda itaenda kwa wanamtandaoKama nchi ningeshauri tujifunze kushughulika na kero hata kama hazina madhara ya moja kwa moja!
Huko ulaya wenzetu huwa wanafanya oparesheni ya kuondoa paka, mbwa na ndege wasio natija!
Hata hapa kwetu sioni kama inashindikana kuwaondoa kitaalam hawa kunguru weusi!
Historia inasemekana wazo la kuleta mbegu ya hawa kunguru weusi lilifanyika katika utawala wa CCM chini ya waziri mkuu wa zamani EDWARD LOWASSA ambapo liligharimu bilion 7.5 Wakiwa na lengo kwamba Kunguru hawa weusi wangesaidia kula uchafu huko mahospitali!
Bahati mbaya maamuzi hayo yalifanyika pasipo utafiti wa kitaalam!
Kundi la kwanza lilimwagwa Zanzibar! Na baadae wakazaliana na wengine walisafili kuja Tanzania bara kwa kudandia meli na majahazi baharini!
Hivi sasa kunguru hawa ni kero kubwa sana kwa taifa na wananchi!
1. Wanapiga makelele baadhi ya makundi mahospitalini
2. Wanachafua mazingira ya miti na kujisaidia ovyo.
3. Wanaharibu miundombinu ya umeme na kusababisha ukosefu wa umeme kwa dharula (wanabeba vipande vya waya wanapotua kwenye nyaya za tanesco wanagonganisha waya transfoma zinazima-KERO)
4. Wanachafua nguo za wananchi zilizoanikwa juani!
5. Wanawasumbua sana walevi na wapenda nyama choma huko bar
6. Wana wanyea mav hasa wanapoona mtu kavaa vizuri hususan MTU akivaa nguo nyeupe au ya kung'aa
7. Wanapokonya chakula watoto wadogo
8. Wanaipua mboga jikoni na kula hata kama ilifunikwa
9. Wakifa Hawaozi haraka
10. Ni hatari kwenye baadhi ya injini hasa maeneo ya uwanja wa ndege
Kiufupi hawa kunguru weusi wana kero nyingi ambazo lazima serikali ifanye mpango mkakati kuwatokomeza kabla hawajaongezeka!
Kama serikali itashindwa basi tenda wapewe wachina watuondolee huu upuuzi unaozidi kuzaliana!
WATU WAZURI HUSHUGHULIKIA KERO ZA WATU ILI WAKUMBUKWE KWA MAZURI NA SI KWA MABAYA
Asili yao ni India na huko wameshindikanaWanakula mayai ya Ndege wa Asili na kupelekea kupotea kwa asilimia kubwa ya Ndege wa Asili.
Hili ni Janga kubwa.
Next time wachanganyie na diazepamNinapoishi kuna Minazi mingi ndio wamefanya makazi yao, nimewawekea maji kwenye chombo maalum baada ya hapo awali kua wanafungua bomba la nje wanakunywa maji na kuacha yanamwagika,
Mabaki ya chakula hua nawawekea sehemu maalum na wakishaniona naelekea hiyo sehemu wanakuja kwa kelele kali hua natafsiri wanafurahi na kuitana, wanabeba na kula kwenye nyumba zao,
Watu wengine wanaona kero makelele yao nikagundua kinachowasumbua ni kiu cha maji.
Heeh isije kuwa ndo maana hata matunda asilia yamekuwa adimuNime wafuatilia ni waharibifu sana hawana Faida hata 1. Wana kula maua/kiini cha miti inayo toa maua kuchavusha.
Hii ni kama ile sumu ya panya auNext time wachanganyie na diazepam
duuh hapo kwenye b7.5!!!!, duuh, hebu kaangalie upya takwimu hizo labda umekosea ni mnKama nchi ningeshauri tujifunze kushughulika na kero hata kama hazina madhara ya moja kwa moja!
Huko ulaya wenzetu huwa wanafanya oparesheni ya kuondoa paka, mbwa na ndege wasio natija...
Why would i do that jamaniNext time wachanganyie na diazepam
Sijajua kama ni kwel bil 7.ila hela hizo zingefanya uboreshaj wa dampo la lingato kwa kigamboni na pugu kwa kuweka magari ya uchakataji na usindikaj wa taka ngumu ajira tupuBilioni saba duh mbona hayo mabilioni yangetumika na program nyinginezo mji wa dar ungekuwa safi na wa kupendeza mnooo
Siku wakifunua mboga yako hapo uani wakachukua vipande vya nyama na wakanyea nguo ulizoanika utaacha hii hurumaWhy would i do that jamani
Sipikii nje sababu sina jiko la nje, hawaingii ndani na nafua kila siku hawajawahi kunyea nguo zangu na hata ikitokea wamenyea so what? Mavi ya Kunguru yana madhara gani hadi inifanye niwachukie?Siku wakifua mboga yako hapo uani wakachukua vipande vya nyama na wakanyea nguo ulizoanika utaacha hii huruma
Hao viumbe siwezi kuwasahau nilikuwa niko barazani nakunywa niko na chupa za bia zangu chupa tatu naingia ndani kupokea simu ilikuwa kwenye chaji inaita nakuta wameziangusha zimevunjika pombe zimemwagika walidhani ni majiSipikii nje sababu sina jiko la nje, hawaingii ndani na nafua kila siku hawajawahi kunyea nguo zangu na hata ikitokea wamenyea so what? Mavi ya Kunguru yana madhara gani hadi inifanye niwachukie?
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] eti wananizomea lakini ulishajua nia yao haikua kumwaga pombe yako bali ilikua kupata maji, ndio maana nikasema hawa kinachowasumbua sana ni kiu cha maji ndio maana wanakua na vurugu,Hao viumbe siwezi kuwasahau nilikuwa niko barazani nakunywa niko na chupa za bia zangu chupa tatu naingia ndani kupokea simu ilikuwa kwenye chaji inaita nakuta wameziangusha zimevunjika pombe zimemwagika walidhani ni maji
Wakapeperuka mbele kuna nyaya za nguzo walikuwa wanalia huko wananiangalia
Nilijua kabisa wananizomea baada ya kufanya kile kitendo
Ilikuwa project ya watu kupiga hela wakaleta matatizoWanafungua kwa midomo yao, mngekua mmewawekea chombo chao cha maji wangeacha,
Kiu ni kibaya sana unajua wao chakula wanapata kwa urahisi tu tatizo hua ni maji hasa kipindi hiki cha ukame.