Kama Wizara ya Maliasili na Serikali hawana mkakati wa kutokomeza kunguru weusi, tuwape tenda wachina

Hata mimi hawaniogopi, naweza nikawa nje nimekaa wakawa pembeni yangu ila akitokea mtu mwingine wanaondoka,

Napenda sana Ndege na Wanyama.
 
Nilikuwa napiga stor na jamaa zangu wa arusha nikawaambia jinsi hawa kunguru wanavofungua koki ya maji na kuyaacha yamwagike, kila mtu aliniona ni muongo...
Vitambaa vya kuchujia maji vikianikwa inje kunguru wanapenda kuvikanyaga na kuvinyea ....na watu wengi hawajashitukia hilo wanakwenda chujia maji pasipo kujua
 
Nime wafuatilia ni waharibifu sana hawana Faida hata 1. Wana kula maua/kiini cha miti inayo toa maua kuchavusha.
 
Tutapewa bajeti ya billion kumi kuwateketeza na tenda itaenda kwa wanamtandao
 
Next time wachanganyie na diazepam
 
Nime wafuatilia ni waharibifu sana hawana Faida hata 1. Wana kula maua/kiini cha miti inayo toa maua kuchavusha.
Heeh isije kuwa ndo maana hata matunda asilia yamekuwa adimu
 
Kama nchi ningeshauri tujifunze kushughulika na kero hata kama hazina madhara ya moja kwa moja!
Huko ulaya wenzetu huwa wanafanya oparesheni ya kuondoa paka, mbwa na ndege wasio natija...
duuh hapo kwenye b7.5!!!!, duuh, hebu kaangalie upya takwimu hizo labda umekosea ni mn
 
Bilioni saba duh mbona hayo mabilioni yangetumika na program nyinginezo mji wa dar ungekuwa safi na wa kupendeza mnooo
Sijajua kama ni kwel bil 7.ila hela hizo zingefanya uboreshaj wa dampo la lingato kwa kigamboni na pugu kwa kuweka magari ya uchakataji na usindikaj wa taka ngumu ajira tupu
 
Hata vifaranga vya kuku wanabeba hao.
 
Kwa kweli wanakera sana alaf cha kushangaza wamejaa sana kwenye nchi za kimaskini sijui wananasaba gani na umaskini awa kunguru?!!! Nchi kama Bangladesh, Sri lanka, Nepal and etc. Aliyetoa wazo la kuleta awa kunguru katuletea majanga kweli yan. Kwa kweli awa ndege wanachuki sana na binadam washawai nifukuzaga nilipokuwa shule ya msingi tena for the no reason 😀😀 Hawana faida yoyote kwenye mazingira yetu ata urembo wa kupendezesha mazingira yetu hawana kama ilivyo kwa ndege wetu wa asili.
 
Siku wakifua mboga yako hapo uani wakachukua vipande vya nyama na wakanyea nguo ulizoanika utaacha hii huruma
Sipikii nje sababu sina jiko la nje, hawaingii ndani na nafua kila siku hawajawahi kunyea nguo zangu na hata ikitokea wamenyea so what? Mavi ya Kunguru yana madhara gani hadi inifanye niwachukie?
 
Sipikii nje sababu sina jiko la nje, hawaingii ndani na nafua kila siku hawajawahi kunyea nguo zangu na hata ikitokea wamenyea so what? Mavi ya Kunguru yana madhara gani hadi inifanye niwachukie?
Hao viumbe siwezi kuwasahau nilikuwa niko barazani nakunywa niko na chupa za bia zangu chupa tatu naingia ndani kupokea simu ilikuwa kwenye chaji inaita nakuta wameziangusha zimevunjika pombe zimemwagika walidhani ni maji


Wakapeperuka mbele kuna nyaya za nguzo walikuwa wanalia huko wananiangalia

Nilijua kabisa wananizomea baada ya kufanya kile kitendo
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] eti wananizomea lakini ulishajua nia yao haikua kumwaga pombe yako bali ilikua kupata maji, ndio maana nikasema hawa kinachowasumbua sana ni kiu cha maji ndio maana wanakua na vurugu,

Wasamehe sababu wote ni viumbe wa Mungu na Rizki yao inatokana na sisi.
 
Wanafungua kwa midomo yao, mngekua mmewawekea chombo chao cha maji wangeacha,

Kiu ni kibaya sana unajua wao chakula wanapata kwa urahisi tu tatizo hua ni maji hasa kipindi hiki cha ukame.
Ilikuwa project ya watu kupiga hela wakaleta matatizo
 
Kunguru mama kunguru mamaa, hafugiki mama.
[emoji41]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…