Kama Yesu Kristo alikufa Msalabani ili tukombowele katika utumwa wa Dhambi mbona bado dhambi zinazidi kuongezeka?

Kama Yesu Kristo alikufa Msalabani ili tukombowele katika utumwa wa Dhambi mbona bado dhambi zinazidi kuongezeka?

kwa jinsi nilivyoielewa biblia inatuambia yeye ni kweli nauzima kila amwaminiye atapata uzima wa milele , ila utashangaa wahubili wanavyo watisha waumini kuhusu dhambi na bwawa liwakalo motto na kibiriti hii yote kuwafanya watu wawe watiifu nawanyenye kevu kupita uhalisia ili waweze kukusanya mapato kiurahisi
🤣🤣🤣🤣
 
Mkuu ni swali zuri, ila jiulize swali dogo, wewe kama mzazi unajitoa kufanya kazi ili familia na wewe uie, je ulishawahi kumaliza njaa?

kwa wote wenye mwili na roho, ukombozi unakuja kwa juhudi yako, kwa maana utahukumiwa kwa kadiri ya matendo yako.

Ukombozi hauji kwa kusali sana au kukesha makanisani wakati unafanya matendo mabaya. Matendo yako na si kitu kingine
Kwahiyo hata kama ni mpagani na una matendo mazuri ni peponi moja kwa moja?
 
Mkuu hiyo bi porojo tu kama porojo zengine
Nalog off
 
🤣 Watu mnafukuana Spenkon
Screenshot_20230109-164201.png

Shetani mwenyewe anapewa mambo 🤣
 
Na dhambi za siku hizi hadi shetani anashika kichwa.....
Asingetukomboa, adhabu ya kufanya dhambi isingekuwa ndogo kama hiyo, yaani kuchomsa kwenye tanuru lw moto milele,, 🤷‍♂️,
Sasa alikufa na akatukomboa,, sasa ukifanya dhambi, badala ya kutupwa kwenye mafuta ya moto yachemkayo, basi utatupwa jehanum kwenye zowa la moto😂🙆🏻‍♀️
 
Yesu hakufa kwaajili ya kuwakomboa, hata hivyo biblia inasema alikuja kwaajili ya kondoo waliopotea wa nyumba ya israel ama wana wa kabila zake waliopotea, hivyo uwepo wake dunian ilikuwa ni kwaajili ya watu wa asili yake na jamii yake tu, ninyi wengine hamuhusiki acheni shobo.

Hakukuwa na ulazima wa yeye kufa msalaban ili awakomboe[emoji16][emoji23] bali chuki za wale aliokuwa anawahubiria ndio zilisababisha afe kwa kupewa makosa hivyo kifo chake kisiwe sabbu ya kusema ni ukombozi.

Hata hivyo kama yeye kwel alikuja kwaajil ya kuikomboa dunia basi isingetumika nguvu kubwa kueneza neno lake, hususan Afrika ambako mamilion ya watu walikufa wakilazimishwa kuamin huo upuuzi wa kidini na kushika mafundisho ya ukristo, pia hakukua na ulazma wa imani kuenea kwa njia ya vita za msalaba zilizokuwa na malengo ya kueneza hiyo imani ya Yesu wenu.

Pia hakuna Ushahidi wa yesu kukomboa wala kusaidia jambo lolote zaid ya uzushi wa wafia dini.

Yesu hajawai kuwepo, aliundwa na wakatoric miaka ya 300A.D kwa kuchukua historia za miungu ya wamisri, wahindu, then kuleta jina jipya la Yesu kutoka kwa Yeshua ama Zeus/Azazel ama Osiris mungu mwana wa kiume wa kimisri..

Tafuta dunia nzima hautapata historia ya uwepo wa yesu wala hao mitume wake kuishi dunian, zaid ya uzushi huo utaupata ktk vtabu vya kidini vinavyolazimisha mtu aamini bila kutumia fikra kupambanua mambo.

Yesu angekuwepo kwel basi angesharudi kitambo sana maana hata ktk maneno yake alikuwa akiwashuhudia baadhi ya watu wake kuwa angerejea muda si mrefu na kwa dalili ilionesha ni kipindi chake[emoji23][emoji23] yuko wapi sasa?

Yesu angekuwepo basi dhambi zinazoongozwa kutendwa na wafia dini za ulawiti, uuwaji, ubakaji na ushirikina makanisan haya zisingekuwepo.

Yesu angewafia wanadamu basi isingekuwa na haja ya kutueleza sana maana kila mtu angeshajua bila kuforciwa na dini.

Yesu hatorudi, mtakesha mkisubiri hatorudi maana hajawai kuwepo na hatowai kuwepo.

Jina la Yesu liloundwa na wazungu wa kirumi kisiri kwa kumaanisha SUN/SON ama mwana wa shetan/nyota ya asubuh ambaye ni aina ya Pepo lenye muundo wa kondoo dume, pepo hilo lina nguvu kubwa ya kutenda mazingaombwe kwa wanaoliita kupitia makafala ya damu(damu ya yesu), pia kutaja majina yake ya asili ama kificho pepo hilo linaweza kutenda maajabu.

Pepo hilo ndio aina ya yale sign of 666 ambayo ndio hayo yatatumika kuwaingia watu kama chapa ya akili kwa kuwapotosha na kuwafunga kiakili na kiroho wasiweze kutambua Muumba wa kweli ni yupi, na badala yake kuwafanya watu waamini maajenti wa hili pepo ambao ndio hao wachungaji wenu na dinu zote za ulimwengu zote ziko chini ya hiki kiumbe kushirikiana na mapepo wengine(666) ambao kama watakuingia basi sahau kuhusu Kupona ktk Hukumu, maana utakuwa mmoja wa waabudu sanamu.

Dini zote ni uongo, dini zote zinamuabudu kiumbe mmoja kupitia mikanganyiko ya kuwafanya watu wasijue kweli kwa kufarakana na kutofautiana ktk mafundisho yao.

Muumba wa kweli hana haja ya sisi kuwa na dini na hajawai kumtuma huyo yesu aje awafie wanadamu, dhambi kutoka kwake ni wew kuomba mthamah na kuacha FULL STOP.

Wewe ni kibogoyo wa akili na fikra! Nadhani kila atakayethubutu kukujibu hapa atakushushia mawe badala ya kukupongeza hizo pumba ulizomwaga hapa!
 
Ndio maana wayahudi wanasema Yesu bado hajaja.

Maana wanadamu tuiahidiwa Yesu Kristo atazaliwa na atakufa msalabani. Kifo chake kitakuwa alama ya ukombozi kwa Mwanadamu kutoka ktk utumwa wa dhambi.

Mbona sasa maovu, maasi na dhambi ndio kwanza zinazidi kuongezeka. Au aliyekuja na kufa sio Yesu Halisi
Yesu alikuja na AKAISHI kwa ajili yetu ili maisha yake yakawe funzo kwetu.

Yeyote atakayekubali hilo na kuamua kuiga na kufuata kuishi kama alivyoelekeza yeye mwenyewe Kristu basi atakuwa amekombolewa na utumwa wa dhambi.

Kosa lilianza tulioohusianisha mambo ya kafara za mizimu, na kufanya kama mungu 'alihitaji' kafara tu ili siai tupone. La si hivyo! Siku zote Mungu hupendezwa na maisha bora aliyojitoa mtu kuyaishi kwa ajili ya rafiki zake. Umeelewaelewa kaka?
 
Baada ya gharika ya kipindi cha Nuhu na dhahma ya Sodoma na Gomora, kuna tukio lingine lilikuwa linaandaliwa kwaajili waasi. Yesu akaja kuwafundisha watu namna ya kumjua Mungu ili waongoke na kujilinda ili hasira za Mungu zisije kuwaka juu yao.

Kupitia Yesu watu wengi wameokoka. Wamepatikana watu 10 kwenye 50. Naye, Mungu anauacha mji salama kwa ajili yao.

"Mpaka sasa hakuna maovu binafamu amefanya kuzidi maovu waliofanya watu walioishi katika miji ya Sodoma na Ghomora" Ustadh Khamis.
 
Kama hutamuamini Yesu usitegemee kutotenda dhambi na kuokoka [emoji116]

YOHANA 3:16

[16]Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
 
Back
Top Bottom