Kamanda Lissu, Usisubiri Jibu la IGP Kuhusu Usalama Wako, Aliyekulinda na Shambulio Lile Yupo, Yeye Aweza, na Ataendelea Kukulinda, Welcome Back Home!

Kamanda Lissu, Usisubiri Jibu la IGP Kuhusu Usalama Wako, Aliyekulinda na Shambulio Lile Yupo, Yeye Aweza, na Ataendelea Kukulinda, Welcome Back Home!

Nimependa sana matumizi ya maneno "jeshi letu lenye huruma".

Huwa najiuliza Lissu hata akirejea leo hivi watamfanya nini? concentration ya public itakuwa kwake, halafu wathubutu kumshambulia tena? mtu huyo huyo ashambuliwe mara mbili na wasiojulikana na wasifahamike itawezekana vipi kwenye nchi inayojinasibu ina vyombo vya ulinzi na usalama?!

Wakithubutu kufanya hivyo watazidi kujivua nguo mbele ya dunia yote, na ikiwa Pompeo kashaanza kumtaja muuwaji, na mpaka leo hajawahi kukanusha, sana sana wataanza kumfungulia Lissu kesi zao zisizo na kichwa wala miguu, but sio kumshambulia tena, ili kulinda heshima zao binafsi, za serikali yao, na za taifa, mbele ya jumuia ya kimataifa.

Kwangu kuomba ulinzi wa mwanadamu ni sawa na kumtukuza shetani, imeandikwa amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, yaishi maandiko hata ikibidi kuweka rehani uzima wako ili kumtukuza Mungu wa kweli, na mchawi siku zote mpe mwanao akulelee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mugah di mathew,
Sasa kama kazi ya polisi inajulukana ni kulinda raia na mali zao, je Mh Lissu ni au si raia? kama ni raia, polisi itawandikia wangapi? au yeye tu?

Nadhani hela wanayo ila si ya kuandikia raia kuwajulisha kuwa wanawalinda!! Na zaidi mlinzi wa kweli ni YEYE yule aliemkinga na kile kifo!!
 
Alaaniwe tena aliyepanga na kutekeleza Shambulio la mbunge mahiri wa Wakati wote Mh Tundu Lisu

Alaaniwe yeye na kizazi chake Kwa unyama aloufanya

Pamoja na hayo, Ni vema hata Sisi kuzingatia heshima na Utu wa mtu hasa Kwa maneno yetu ili siku ya siku tuhifadhiane Kwa upendo,

Kashifa za maneno na kejeli kuhusu kazi za watu si nzuri hata kidogo Bali ni kujitafutia uadui usio na tija, binadamu husaidiana Sisi Kwa Sisi,

Maneno magumu na kukejeli Idara ya ulinzi ama mtu binafsi yaliyokuwa yakitumiwa na mwenzetu Lisu, kuwasilisha kile asichokipenda Kwa maasikari polisi nchini, hayakuwa sahihi hata kidogo, ukizingatia kwamba Wao ndio wanaopaswa wamhakikishie ulinzi wake n.k

SASA hembu ona , walewale uliokuwa ukiwatusi na kuwakejeri unawaomba tena wakuhakikishie ulinzi, Duniani hakuna mwenye moyo wa jiwe, sote tunaumia na kuumizwa na Kisha uzalendo na uvumilivu huisha

Hili liwe fundisho si Kwa mtu mmoja tu, Bali mtu yeyote mwenye maneno mbofumbofu, kutukana wengine, kudharau na kukebehe pia kuwaona walio chini yake kuwa ni mafala tu, kwa sababu ya kiburi tu cha uzima ama madaraka, kila mtu akipandacho atavuna Kwa kicho, tuepukeni kujitafutia maadui Kwa lazima na hili linaepukika

Tanzania yangu, Tundu Lisu ni Mtanzania mwenzetu, aweza kuwa anamakosa, lakini hawezi kuhukumiwa milele, Chonde Chonde tunampenda kama wengine, tungependa kuona akiendelea kulisaidia Taifa lake

Mungu akulinde Lisu akupe Amani na maisha ya kushinda, hakika wewe ni shujaaa
 
Pascal Mayalla,
Kulindwa na ni upendeleo tu, just kwa kuwa Mungu yupo haipaswi kutafsirika kwamba tuache kuchukua hatua na kutumia akili zetu.

Mungu aliweka akili kubwa ndani ya vichwa vyetu ili tuweze kujimudu kwa mambo Mengi badala ya kumtegemea kwa kila kitu.

Kwa hivyo basi, nakushauri, ksma wewe ni Mkristo wa kweli uache mara moja kumjaribu Mungu wako.
 
Ila huyu Lissu anawahangaisha sana watu mawazo yao. Vipi inakuwaje anaowatuhumu ndio wamlinde? Ningelishangaa sana kama IGP angeijibu hiyo barua ya kumpa ulinzi. Ushauri wangu, kama anataka ulinzi, atembee na Red Brigades hata kumi. Au hawaamini? Maana kuna conspiracy theory inayodai Red Brigades ndio walio stage ile kitu!
 
Binafsi nimewahi kuwa shuhuda wa hali kama hiyo.
Ndugu yangu alitekwa na baada ya siku akarejea akiwa mgonjwa akatibiwa kwa uangalizi wa polisi ktk eneo hilo lkn hawakumuoji nasi bila kuchelewa tukapambania rufaa ili aende hospital nyingine na kubwa ili atibiwe pia apate mapumziko.

Baada ya wiki kadhaa akarejea lkn wakati huo sisi na yeye akiwa kwenye hofu nzito ya kufuatiliwa na kukimbizwa, tukaamua mm mwenyewe kupeleka barua kwa RPC wa eneo hilo kuomba ulinzi.

Barua haikuwahi kujibiwa pia ulinzi hatukuwahi kuuona. Hali hiyo iliendelea mpka tulipoamua kula sahani moja na serikali kwa adabu.

Mnaweza kutegemea kama hayo kwa kuwa mmarekani kashasema nani ni chokochoko.

Lisu mwenyewe anajua hawezi kuzuriwa tena.
Anatafuta attention ya umma kama ulinzi
Lisu rudi hapa ni kwenu na kwako.
 
Huwezi kumjaribu MUNGU maadam wabaya wako bado wapo na wanaendelea kutawala bakia huko. Hata alipozaliwa YESU enzi za utawala dharimu wazazi kwa kuongozwa na ROHO wa MUNGU walikimbilia MISRI.

Kuna wimbo ulipigwa na Balsidia wema hawana maisha. Hukatiliwa mbali na waovu tafuta kazi subiri MUNGU awatengeneze kwanza na auweke wazi uovu wao.

Nakushauri usimsikilize huyo P ni mshirika ama mwenzao ktk kutengeneza mitego.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usimdanganye ! Arudi wamdungue tena ? Kumbuka hata yule Lazaro aliyefufuliwa na Yesu Kristo alikufa tena. Zaidi sana hata Mtoto Yesu Kristo alikaa uhamishoni Misri mpaka yule Herode aliyetaka kumuua alipofariki. Abaki huko huko kama anamudu gharama za maisha ya huko.
Ungemsoma vzr pasco mayala ungeelewa nini alicho andika.tafuta hiden meaning ya bandiko lake utatabasam tu!
 
Ushauri wa Pasco hauna bases yoyote ila nikujikosha kwa wanaoitamani damu ya Mh. Lissu. Mungu ndiye mlinzi wetu wote, lakini pia imeandikwa usimjaribu Mungu wako. Maana yake ni Kwamba bado mazingira ya kile kilichompata hayajabadirika na Kiganja cha chuma bado chaweza kuwa kinamsubiri. Naungana na wanaoshauri aendelee Kuishi huko ughaibuni hadi pale tufani hii utakapotulia. Your Beloved Tanzanian Love You and are not ready to miss you. Blessed.
Soma between lines utaelewa alichoa andika pasco
 
Mwandishi hebu tumia akili kufikiri mara mbili kabla ya kuandika..kwa serikali hii ya kutunisha misuli usifikiri lissu akirudi ataachwa hivi hivi na kwakua ana kesi zilizokua zinaendelea basi atakmatwa mapema tu pale Airport na huko wanaweza kumpa hata sumu ikamuua pole pole

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna lolote hapa zaidi ya unafiq.
Ni kama ule wa nyuzi za kaFLAG.
Lissu usirudi
images (3).jpeg
 
Back
Top Bottom