Uchaguzi 2020 Kamanda Mambosasa: Mbowe na wenzake kushtakiwa kwa makosa ya ugaidi, walipanga kulipua vituo vya mafuta

Uchaguzi 2020 Kamanda Mambosasa: Mbowe na wenzake kushtakiwa kwa makosa ya ugaidi, walipanga kulipua vituo vya mafuta

Arusha Hali ya Hewa Ni shwari nimetoka Kisongo Hadi Usa River nikarudi Hadi Moshono, Chekereni Hadi Chuo Kikuu Cha Nelson Mandela kwa kutumia Baiskeli bila shida yeyote. Kila mtu anaendelea na kazi zake za kila siku.
 
Maandamano & Sheria Husika

Sheria ya Jeshi la Polisi ya mwaka 1961 na marekebisho yake ya mwaka 1995, ambayo ndiyo huelekeza na kuongoza kuhusu njia na namna ya kuendesha maandamano nchini, inasema:

(1) Mtu yeyote ambaye ana mpango wa kufanya, kukusanya, kuunda au kupanga mkusanyiko au maandamano ya hadhara, kwa muda usiopungua saa 48 kabla ya mkusanyiko au maandamano kwa muda uliopangwa kuanza, atawasilisha kwa maandishi notisi kuhusu kufanyika kwa mkusanyiko au maandamano hayo kwa afisa polisi msimamizi wa eneo hilo akianisha:

(a) Sehemu na muda ambao mkutano utafanyika;
(b) Dhumuni kwa ujumla kuhusu mkutano huo; na
(c) Maelezo mengine kama Waziri atakavyotangaza kwa notisi, mara kwa mara kwenye Gazeti la Serikali.

(2) Pale ambapo mtu amewasilisha taarifa kulingana na kifungu kidogo cha (1), anaweza kuendelea kuitisha, kukusanya, kuunda, au kuandaa mkusanyiko au maandamano hayo kama yalivyopangwa isipokuwa pale atakapopokea amri kutoka kwa afisa polisi msimamizi wa eneo husika ikielekeza kwamba mkusanyiko au maandamano hayo hayatafanyika kama ilivyotaarifiwa.

(3) Afisa polisi ambaye taarifa imewasilishwa kwake kulingana na kifungu kidogo cha (1), hatatoa amri ya kusitisha chini ya kifungu kidogo cha (2) kulingana na taarifa husika, isipokuwa ameridhika kwamba kufanyika kwa mkusanyiko au maandamano hayo kuna uwezekano wa kusababisha kuvunjika kwa amani au kuathiri usalama wa taifa au kudumisha amri kwa umma au kutumika kwa dhumuni lolote lisilokuwa halali.

Hii ndiyo sheria inayoongoza Jeshi la Polisi kwa maana rahisi maandamano ni mpaka pale jeshi la polisi limekubali na kutoa kibali baada ya waandamanaji kuomba kibali hicho.

Vyovyote vile, kuhusu maandamano hayo, jeshi la polisi linapaswa lijiridhishe pasipo shaka kuwa hayahatarishi maisha au kuleta madhara yoyote na hayataingilia haki za watu wengine ambao hawataki kuandamana.

NINI KINACHOWEZA KUTOKEA?

Kinachoweza kutokea baada ya katazo la jeshi la polisi, ni kujitokeza kwa watu wenye nia ya kutaka kuandamana kwa nguvu. Ukifanya hivyo moja kwa moja utakuwa unatenda kosa la UHAINI ambalo ndilo kosa kubwa kuliko yote nchini kwa mujibu wa ibara ya 28 ya Katiba yetu.

Sheria inasema kwamba kama ukifanya yafuatayo utakuwa umefanya uhaini katika Jamhuri ya Muungano:

(a) Kifungu cha 39 (1) cha kanuni za adhabu kinasema kuwa mtu yeyote ambaye yumo ndani ya Jamhuri ya Muungano au popote akajaribu kumuua Rais, atakuwa ametenda uhaini.

(b) Mtu yeyote aliye ndani ya Jamhuri ya Muungano au popote akaanzisha vita dhidi ya Jamhuri ya Muungano atakuwa naye ametenda kosa la uhaini.

(c) Mtu yeyote ambaye yuko ndani ya Jamhuri ya Muungano au popote ambaye atajenga, kusababisha au kuwezesha, kuchochea, kushawishi, kushauri, kuhusu kifo, kumlemaza, kumzuia, au kufungwa kwa Rais atakuwa ametenda uhaini.

(d) Mtu yeyote ambaye yuko ndani ya Jamhuri ya Muungano au popote ambaye atajenga, kusababisha au kuwezesha, kuchochea, kushawishi, kushauri kumwondoa Rais madarakani visivyo halali atakuwa ametenda kosa la uhaini.

(e) Mtu yeyote ambaye yuko ndani ya Jamhuri ya Muungano au popote ambaye atajenga, kusababisha au kuwezesha, kuchochea, kushawishi, kushauri kumwondolea Rais heshima na jina la mkuu wa nchi, amiri jeshi mkuu, au kiongozi mkuu wa serikali atakuwa ametenda kosa la uhaini.

(f) Mtu yeyote ambaye yuko ndani ya Jamhuri ya Muungano au popote ambaye atajenga, kusababisha au kuwezesha, kuchochea, kushawishi, kushauri kupindua serikali iliyo madarakani, kutishia serikali, bunge au mahakama atakuwa ametenda kosa la uhaini.

ADHABU
Kwa mtu yeyote atakayekutwa na hatia ya kutenda kosa la uhaini, adhabu yake ni kifo; na sheria hiyo ya kifo imeelezwa katika kifungu cha sheria namba 39 na 40 cha kanuni za adhabu.

Hivyo, Watanzania kwa umoja wetu tunapaswa kuzijua sheria za nchi yetu ili kuweza kujiepusha kutenda makosa ya jinai dhidi ya nchi yetu.
 
CCM mlivyo Wapumbavu mnafurahia ukandamizaji huu wa haki ya kidemokrasia..!!
 
Hii nchi ni ya kishetani kweli, watu wamejaa uongo na uzindaki tena hawaoni hata aibu wanapoongea, lakini msipowaruhusu watu watoe hisia zao mnatengeneza ugaidi
Wajifunze kwa jirani, Uhuru aliwaachia wakaenda zao uwanjani na kina Miguna, wakajiapisha uraisi, walivyomaliza wakasambaratikia ikulu za majumbani! Kiroho safii!

Everyday is Saturday............... 😎
 
Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam ACP Lazaro Mambosasa amesema wanawashikilia watu kadhaa wakiwemo viongozi watatu wa CHADEMA...

Ushauri wangu kwa Jeshi la Polisi.
1. Kuhakikisha inazikamata familia za hawa wahamasishaji wa haya maandamano ya kidhalimu.

2. Kufanya uchunguzi wa kina juu ya tuhuma za pesa wanazopokea viongozi hawa kusababisha vurugu nchini.

3. Kuangalia upya hivi vyama na kuweka mkakati wa itisha uhaguzi wa huru ndani ya hivi vyama ili wale viongozi wanaongangania madaraka waondoshwe. Wanachama wengi wa vyama vya CHADEMA na ACT hawakubaliani na uhuni wa viongozi wa juu wa vyama hivi.Hivyo serikali kupitia msajili wa vyama aitishe mikutano ili tuweze kupata viongozi wazalendo.

4. Kufuta vyama vyenye mrengo wa Ushoga amabavyo ni kinyume na mila na desturi za watanzania.
 
Mimi nimeshajiandaa na vijana wenzangu kama 70 hivi. Mabali na sisi Coaster kumi na mbili toka maeneo mengine ikiwemo Arusha ziko njiani muda huu.
Wewe Sexless unaandamana kwenye key board tu. Wala huendi road.
Mwenzio Mbowe yuko ndichi saa hii.
 
Mimi nimeshajiandaa na vijana wenzangu kama 70 hivi. Mabali na sisi Coaster kumi na mbili toka maeneo mengine ikiwemo Arusha ziko njiani muda huu.
😂😂😂 Watu 70 + coaster moja inabeba watu kuanzia 35+ so 35*12= 420 then + 70 inakuwa ni watu 490 😳😳😳😳😳
Unadanganya umma 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣 bhana hao watu mko wap
 
Wanaumia kuukosa ubunge ,maandamano yakitokea watu wakawa wengi hasa basi ujue Magufuli hatukumchagua ila nijuavyo mimi Magufuli kapata kura nyingi sana ila kama figisu zilitokea ni ngazi ya Ubunge kama hawakumtaka wengi ndio wanaweza watu wake kuandamana ila sio kwa sababu Lissu kaibiwa hiyo ni Big No ngoja pakuche utashuhudia.
Kulikuwa na multiple voting na ballot pre-ticking za kutosha - kwa kura za Urais na ubunge pia. Fuatilia taarifa za Watazamaji wa kujitegemea
 
Back
Top Bottom