Uchaguzi 2020 Kamanda Mambosasa: Mbowe na wenzake kushtakiwa kwa makosa ya ugaidi, walipanga kulipua vituo vya mafuta

Uchaguzi 2020 Kamanda Mambosasa: Mbowe na wenzake kushtakiwa kwa makosa ya ugaidi, walipanga kulipua vituo vya mafuta

Mambosasa yupo live ITV usiku huu akisema amewakamata Mbowe, Lema na Jacob kwa kuhamasisha maandamano.

Hii haitarudisha nyuma morali wa waandamanaji...
kizazi hiki hakuna mwenye jeuri ya kuandamana zaidi ya kutoa povu mtandaoni
 
Arusha Hali ya Hewa Ni shwari nimetoka Kisongo Hadi Usa River nikarudi Hadi Moshono, Chekereni Hadi Chuo Kikuu Cha Nelson Mandela kwa kutumia Baiskeli bila shida yeyote. Kila mtu anaendelea na kazi zake za kila siku.
Tupo tunaandamana kwenye keyboard
 
Yule mlemavu hayupo! Nadhani kwa sababu ya kundi maalum...
Punguza chuki kauli mbovu kama hizi sio nzuri. Kwani hata yeye hakupenda. Hujafa hujaumbika lolote linaweza kukutokea wewe au familia yako.
 
Saa tano asubuhi , Mwanza ni shwari kabisa, nipo hapa nakula michembe, makande na maziwa mgando! Yaani Mbowe akose ruzuku mimi niandamane?
 
Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam ACP Lazaro Mambosasa amesema wanawashikilia watu kadhaa wakiwemo viongozi watatu wa CHADEMA.

Viongozi wa CHADEMA wanaowashikilia ni pamoja na Freeman Mbowe ambaye ni mwenyekiti wa CHADEMA taifa, Godbless Lema na Boniface Jacob.

Amesema wanawashikilia viongozi hao kwa kuwa wanahatarisha usalama wa Raia na mali zao kwa kuwa Novemba 2 walipanga kuwatumia vijana kuchoma moto miundominu na vituo vya mafuta.

Aidha kwa usiku huu wanaendelea kuwatafuta watu ambao wanawashawishi vijana kushiriki maandamano ambayo Polisi wamesema ni ya Vurugu na si amani kwa kuwa wanaoshawishiwa ni vijana wavuta bangi.

Amesema hayo katika kipindi mubashara kilichorushwa na ITV.

PIA SOMA
= > Uchaguzi 2020 - Dar es Salaam: Watu watatu zaidi wakamatwa kuzuia maandamano
Wawapeleke zoo ili wananchi tupate kuwaona.
 
Maandamano ya amani ni haki ya kikatiba.
Ama nakosea?
 
Polisi wame-panic. Itakula kwao. Wanaoandamana siyo Mbowe, Lema, Lissu, Zitto, Maalim, Bony wala Mazrui. Ni Kaumu ya wananchi walioibiwa kura zao. Ni hii ngoma imesukwa vizuri. Kwamba ni maandamano yasiyokuwa na kikomo.

Ni maandamano ya amani hadi kieleweke. Ki msingi, kuwaweka viongozi ndani ndio kukoleza maandamano yenye fujo. Burasa isipotumika, tusubiri yatakayofuata. Tumekwisha kusoma statements za UK, US, Canada na kwingineko.
Hizo ni kauli za kukataa kuwajibika. Walioibiwa kura sio wananchi , ni wagombea. Mimi kazi yangu ni kupiga kura, kumpa mgombea. Yeye ana wajibu wa kuilinda na kuhakikisha inamnufaisha kwa kuongezea na za wengine. Ni sawa na wewe kupewa pesa na mtu then ukakabwa na kuibiwa. Itakuwa si aliyekupa pesa aliyeibiwa ni wewe. Ulipwe mshahara na boss wako then uibiwe, uje useme boss kaibiwa ili akulipe tena au akakutete sababu ya uzembe wako?
 
Hizo ni kauli za kukataa kuwajibika. Walioibiwa kura sio wananchi , ni wagombea. Mimi kazi yangu ni kupiga kura, kumpa mgombea. Yeye ana wajibu wa kuilinda na kuhakikisha inamnufaisha kwa kuongezea na za wengine. Ni sasa wewe kuoewa pesa na mtu then ukakabwa na kuibiwa. Itakuwa si huyo mtu aliyeibiwa ni wewe. Ulipwe mshahara na boss wako then uibiwe, uje useme boss kaibiwa ili akulipe tena au akakutete sababu ya uzembe wako?
Na utakuwa mpumbavu wa kiwango cha lami kwenda kuandamana wakati ulitimiza wajibu wako.

Mawakala wenu mnawachagua kisha kura zikiibwa wananchi waandamane! Kwanini wasianze mawakala na viongozi wa VYAMA vilivyoibiwa kura!?

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Wajifunze kwa jirani, Uhuru aliwaachia wakaenda zao uwanjani na kina Miguna, wakajiapisha uraisi, walivyomaliza wakasambaratikia ikulu za majumbani! Kiroho safii!

Everyday is Saturday............... 😎
Sasa hivi wote wako kwenye Ikulu zao na Mafesti ledi wao.. wanapambana na bajeti tuu 🙂

Hahaha! Huu Mchango wa mwaka!

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Ya Amani na yenye kibali.
Unapoanza kupanga kuchoma vituo vya mafuta ...yote hayo yanakoma

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Kupanga kuchoma vituo ni maneno ya kutunga au tuseme ni ule mwendelezo wa kesi bambikizi.
Tulifikiri kuwa Tanzania ingejirudi na kuacha kubambikiza watu kesi ila sasa jawabu la mambo haya ni kwamba Serikali imejipanga kutumia mabavu maradufu ya yaliyoyatumia huko nyuma ili kulinda maovu yake.

Hebu fikiria polisi anasema et kuna mtu katuambia wamepanga kuchoma vituo. Sasa kumbe hizi ni habari za kuambiwa?
Na ikiwa ni mtu kama Gwajima amewaambia ukweli wa ushuhuda wake una uhalali kiasi gani?
 
Back
Top Bottom