Kamanda Muliro akemea kushambuliwa kwa watumishi wa TRA waliodhaniwa kuwa watekaji

Kamanda Muliro akemea kushambuliwa kwa watumishi wa TRA waliodhaniwa kuwa watekaji

Nahisi hawa wanaopiga watendaji wa serikali wakitekeleza majukumu ni wale walienda Burundi na sasa wamerejea nchini
Wakuu,

Kuhusu sakata la kupigwa kwa viongozi wa TRA waliodhaniwa kuwa ni watekaji, Jumanne Muliro ambaye ni Mkuu wa Polisi Dar Es Salaam amesema:

"Nakemea vikali tabia hiyo na tabia hiyo haivumiliki na wasimamizi wa sheria wataendelea kutimiza majukumu yao wahalifu wataendelea kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria"

Soma pia:
Ufafanuzi kuhusu shambulio la gari la watumishi wa TRA eneo la Tegeta, Dar es Salaam

View attachment 3170230
 
Kamanda amechelewa, angeanza na kukemea matukio ya utekaji tusingefika huku.
Wachangamke kabla hawajachelewa zaidi. Wananchi wakikosa imani hali itakuwa mbaya zaidi kwa serikali kutimiza majukumu yake.

Nchi inatawalika kisheria kunapokuwa na usimamizi wa hizo sheria. Vyombo vyavusimamizi vikishindwa kusimamia, na wananchi wakajua vomeshindwa wanajisimamia wenyewe.

Kulikuwa na haja gani kukimbizana na mtu mtaani wakati wana namba za usajili wa gari? Si wangeenda tu kumpigia simu kupitia taarifa zake
 
Hajawai kukemea watekaji Wala kulaani hayo matukio. Na akemei sababu hayawagusi wao. Sasa wananchi wameona iwe nyama kwa nyama inawagusa wanakemea Sasa. Na hii ni bado ipo siku mtaenda sehemu ya matukio kubeba mizoga yenu ndiyo mtaelewa kuwa dhambi mlizozipanda wenyewe Sasa ni wakati wa mavuno. Kamanda akumbuke ikifikia hivi hata Mungu amewachoka kwa damu mnazozimwaga.
 
Wakuu,

Kuhusu sakata la kupigwa kwa viongozi wa TRA waliodhaniwa kuwa ni watekaji, Jumanne Muliro ambaye ni Mkuu wa Polisi Dar Es Salaam amesema:

"Nakemea vikali tabia hiyo na tabia hiyo haivumiliki na wasimamizi wa sheria wataendelea kutimiza majukumu yao wahalifu wataendelea kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria"

Soma pia:
Ufafanuzi kuhusu shambulio la gari la watumishi wa TRA eneo la Tegeta, Dar es Salaam

View attachment 3170230
Jeshi la polisi na matamko ya kisiasa
 
Vipi kuhusu watekaji wengine? Haoni kwa hatua wananchi waliyochukua wamepoteza imani na jeshi lake
Kwa maana fupi watakao chukuliwa sheria ni wale pekee waliojichukulia sheria mkononi wafanyiwa uchunguzi. Lkn watekaji tusubili tume iundwe ya uchunguz kwa mzee kibao mpaka sasa hakuna majibu ila hao walio bonda gar masaa 12 hayapiti itakuwa tayar
 
Back
Top Bottom