econonist
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 20,189
- 29,663
Leo kwenye Kongamano la TLS kuhusu utekaji na kupotea Kwa raia, Kamanda Muliro amejichanganya kwa kuelezea kuhusu suala la Sativa.
1. Kwanza, amekiri kwamba Sativa kabla ya kuhojiwa alikiri kuwa anamjua aliyemteka.
2. Pili, Kamanda Muliro amedai ya kwamba baada ya kauli ya Sativa , alitokea mtu anayejiita whistleblower kwenye mtandao wa x zamani Twitter na kuelezea kuwa aliyemteka Sativa alikuwa ni mtu Fulani.
3. Tatu, Kamanda Muliro kadai ya kwamba walipomhoji Sativa alikiri kwamba akitekwa na washkaji Fulani hivi.
4. Nne, Kamanda Muliro amedai kuwa baada ya mahojiano ameshangaa kusikia stori tofauti ya Sativa kwamba alitekwa na Mafwele.
5. Tano, kamanda Muliro amedai kwamba suala la Sativa linafanyiwa upelelezi na kwamba Kuna wanasheria na wataalamu wanalifuatilia Hilo jambo kwa kina.
6. Mwisho, Kamanda Muliro kadai ya kwamba wao ndio walimuokoa Sativa, Jambo ambalo ukumbi mzima ulipinga kwa mshangao.
Swali linakuja Kamanda Muliro anadai kwamba walimuokoa Sativa, je walimuokoa kutoka wapi na dhidi ya nani. Je nani aliwapa taarifa ya kwenda kumuokoa? Kama waliweza kwenda kumuokoa wanashindwaje kumkamata muhusika. Kwakweli hapa ndipo tatizo lipo. Halafu Cha kusikitisha jeshi la polisi wapo kwenye uchunguzi wa kina huku mtuhumiwa mkuu ndio ZCO wa Dar es Salaam. Huo ni upelelezi au komedi. Ilitakiwa Mafwele apelekwe likizo ya muda kupisha upelelezi na si vingine.
Pia Kamanda Muliro kadai ya kwamba Sativa alidai ya kwamba katekwa na Washkaji na sio mafwele. Sasa ni kwanini jeshi la polisi linatumia nguvu nyingi kudai hajatekwa na Mafwele baadala ya kuwakamata hao washkaji waliotajwa?. Kama jeshi la polisi linaamini alitekwa na washkaji, ni kwanini inakuwa ngumu kuwakamata Hawa washkaji?. Kama washkaji wa mtaani ni ngumu kuwakamata je polisi wataweza kumkamata nani?.
Mwisho, Napenda kumshauri Kamanda Muliro awe Neutral asioneshe upande wake. Leo ni kama alijipanga kuja kupambana na sio kuleta suluhisho au kuleta mpango wa Jeshi la polisi DSM kupambana na utekaji. Pia ni muhimu kukiri mapungufu kwenye jeshi la polisi hasa kwenye utekaji.