Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Kamanda Muliro nafahamu unasoma hapa jukwaani.
Inawezekana mmejiundia ama kujijengea kasumba kwamba wanasiasa wanafurahia kazi yenu ya kutumia nguvu bila mizania. Mmekuwa mkiwakandamiza na kuwadharau sana wananchi wanapoonewa na askari wa chini yenu.
Mmejipa majukumu ya kisiasa kinyume na Katiba. Mnatoa matamko bila mizania ya matokeo yake.
Mimi kama raia ninatoa ushauri kwenu kwamba, makachero mliowamwaga mitaani kuwasaka wakosoaji na wapinzani wanaochipukia hawawezi kufagia wote. Wanachokipata sasa ni kukosa ushirikiano na hiyo kupelekea taarifa nyingi kupikwa ili malkia aendelee kuamini kuwa mna uwezo wa KUWAZIMA wananchi wanaolilia haki zao.
Tamko ulilolitoa ni budi ikalirejea kwa uzingativu wa alignment kwa Katiba, Sheria na kanuni rasmi. Afisa ama mtumishi wa umma anayekiuka utaratibu anapotekeleza majukumu yake anakuwa ametenda makosa ambayo yanagharimu Haki, Utu na kuichafua serikali.
Askari anapomvamia na kumkwapua raia anayetuhumiwa bila kuzingatia taratibu za ukamataji salama ni wazi anatenda kosa. Wananchi wengi wametekwa haujaleta majibu ya uchunguzi. Ametekwa Ali Kibao kwa mitutu mizito mchana kweupe na kwenda kuuawa mpaka leo hakuna ripoti ya uchunguzi wala waliokamatwa.
Hivyo unavyowatishia wananchi ili waendelee kuwa kondoo wanapotekwa nyara na vyombo vya dola ni wazi kwamba mmeshakolea na kujiamini kwamba matendo ya kigaidi wanayofanyiwa raia ni sawa tu.
Mkuu Muliro, tumia ulimi na ufahamu wako kwa tija na siyo kututishia kwani chuki dhidi yenu imeshaenea vya kutosha. Asiwepo wa kuwasha utambi