Uchaguzi 2020 Kamanda Sirro: Vyama kulinda kura ni kosa la jinai

Hamna mtu anaemjua huyo shoga mwenzako.
 
Asipende kuhoroka ovyo, atuambie ni kifungu kipi cha sheria kinasimamia maneno yake?
Vinginevyo ni porojo tu, tumeshasema SASA BASI
 
Raia Wanaweza kufanya tukio lisilozulika, hawatakiwi kulinda kura.
Kuna sheria inayowakataza?
Ebu tuelimishane kwa wanaojua sheria.
Mimi najua kama jambo sheria haijakataza kulifanya, ukifanya huwezi kuhesabiwa umetenda kosa mpaka hapo sheria ya kulikataza itakapotungwa.
 
Raia Wanaweza kufanya tukio lisilozulika, hawatakiwi kulinda kura.

Huoni umuhimu wa washindani kujiridhisha wenyewe kushinda au kushindwa kwenye kinyang'anyiro chochote?

Haiyumkiniki utakuwa mnufaika katika hali fyongo iliyopo.
 
Raia Wanaweza kufanya tukio lisilozulika, hawatakiwi kulinda kura.

Ni hivi, kuanzia kamanda Sirro mpaka waliochini yake hatuwaamini. Yeye alinde kwakuwa ni wajibu wake kisheria, lakini sio kwamba analinda kwakuwa anaaminika. Kama Magufuli mwenyewe hatumuamini ndio itakuwa kamanda Sirro?
 
Tupe utaratibu unaoruhusu vyama kulinda kura.

Inawezekana hata kusiwe na hata haja ya mtu yeyote kulinda kura kama utaratibu ukiwa wa wazi na wa haki kama ule waliotumia wajumbe kwa watia nia wa lile chama kubwa CCM.

Kinachozozaniwa si ulinzi bali haki.

Wewe huoni hivyo mkuu?
 
Polisi ni sehemu ya wagombea watalinda vipi kura ?
 
Sidhani kama wanahitaji imani ya upinzani huu koko.

Kulindwa kwa kura au kubakia salama kwa kura kunakugugusa negatively mkuu?

Kwa hakika kama wewe ni mnufaika vipi utake utaratibu mwingine unaoweza kukuumbua?



Ndiyo mafisi mnataka kujimilikisha kazi ya kulinda mabucha?
 
Maradaka ya kulevya yanasababisha binadamu kujitoa ufahamu
 
"Ukishindwa kutumia dola kubaki madarakani wewe ni mzembe"by Mao Setung Bashiru Ally.
 
Hii haina tofauti na Fisi kujipa haki pekee za ki leseni (exclusive rights) kulinda mabucha.

Hata aibu kidogo hamna!
 
Unazungumzia utaratibu wenye lengo gani? Utaratibu unaolenga kuiba kura? Sasa wenye utaratibu unaolenga kuzuia wizi wa kura si wanapaswa kuwa na utaratibu wao pia? Kwa nini wazuiwe?

Polisi hawana maslahi wala moral authority ya kulinda kura za wagonbea wa Upinzani? Wasipoteze muda wa watanzania.
 
Kura ni Mali ya Umma,kuzilinda ilitakiwa iwe Ulinzi Shirikishi vinginevyo IGP Sirro atuambie kama kulinda mali ya umma imegeuzwa kuwa jinai?Hofu yake nini?Tulitarajia kura za mwaka huu zihesabiwe hadharani kwa uwazi kwa kila wakala katika kituo cha kura kuhesabu wenyewe kura za wanaowawakilisha pale pale,angalizo la IGP linadhihirisha kuwa matarajio ya Haki kutendeka yanafifia.
Vipi suala la Mawakala kunyimwa vitambulisho na kutokupewa fomu ya matokeo?Je,kwa uzoefu wake anataka kutuaminisha vyanzo vya uvunjifu wa Amani ndiyo hivyo pekee alivyotutajia?Mbona hatujasikia jinai ya kughushi barua za utambulisho wa wagombea kutoka vyama vya upinzani,kuvamiwa na kunyang'anywa fomu za ugombea,kukataliwa kupokelewa fomu na wasimamizi au ofisi kufungwa?Hatusikii hawa wasimamizi wa aina ya yule wa Kinondoni/Kibamba wanastahili adhabu gani?Hiyo nayo ni jinai kwa tafsiri ya IGP?
 
Mwambie Sirro aache kujidhalilisha. Kama vile ambavyo hakuna sheria inayosema polisi ndio watalinda kura basi mwaka huu wananchi tutalinda kura zetu zote.

Na hii ndo hoja kuu kwa mwaka huu. Wananchi tutalinda kura zetu!!! Full stop
Zikiwemo pia za Mh.Magufuli,tunalinda zote ili matokeo halali tu yatangazwe,pasije kutokea wasimamizi wakalinda mishahara na magari waliyopewa kwa kumtangaza asiyeshinda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…