TANZIA Kamanda wa Polisi ACP Jonathan Shana afariki Dunia

TANZIA Kamanda wa Polisi ACP Jonathan Shana afariki Dunia

Huu ndio mwisho wa bin-Adam yeyote. Ndivyo ilivyoandikwa. Tuwe wema kwa binadamu wenzetu wakati bado tunapumua. Tutende haki ili tuwe wenye haki mbele ya Muumba wetu. Poleni wafiwa!
 
Hivi huyu sio ndo yule aliyesema
If A=B and B=C
Then A=C?

Km ni yy ni habari njema sn Mungu anamakusidi nae hasa kipindi hiki
 
Yote maisha...mtu huwezi kuwa sahihi kila jambo,na huwezi kumfurahisha kila mtu.yesu mwenyewe hakupendwa na watu wote.hata aliposulubiwa msalabani wapo waliofurahi.that' s life,wote tutakufa tu muda ukifika.R.I.P
 
Ni huzuni & majonzi

Ameumaliza mwendo

Kazi ya Mungu Haina makosa

RIP Kamanda Shana

=====

TANZIA: KAMANDA JONATHAN SHANA AFARIKI DUNIA

Aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Jonathan Shana amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu

Alifahamika zaidi katika kujihusisha na shughuli za Vyama akiwa na sare za kipolisi. Aidha, aliwahi kufananisha Chama Tawala, Serikali na Dola kwa Kanuni za Kihesabu

Kamanda Shana aliwahi kuwa RCO Mikoa Mbalimbali Nchini ikiwemoRPC-Mikoa ya Pwani, Mwanza na Arusha pia aliwahi kuwa Mkuu wa Upelelezi Simiyu.

ACP Jonathan Shana amefariki akiwa Afisa Mnadhimu katika Chuo cha Polisi (CCP) Moshi



Pia soma >>> RPC Shana anavyotikisha Arusha, awadaka Majangili hatari, AK 45, Meno ya Tembo

Watu 9 waliohusika kutungua chopa na kumuua rubani wakamatwa
Kweli duniani tunapita,
We are not here forever!!!
 
Back
Top Bottom