Ni huzuni & majonzi
Ameumaliza mwendo
Kazi ya Mungu Haina makosa
RIP Kamanda Shana
=====
TANZIA: KAMANDA JONATHAN SHANA AFARIKI DUNIA
Aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Jonathan Shana amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu
Alifahamika zaidi katika kujihusisha na shughuli za Vyama akiwa na sare za kipolisi. Aidha, aliwahi kufananisha Chama Tawala, Serikali na Dola kwa Kanuni za Kihesabu
Kamanda Shana aliwahi kuwa RCO Mikoa Mbalimbali Nchini ikiwemoRPC-Mikoa ya Pwani, Mwanza na Arusha pia aliwahi kuwa Mkuu wa Upelelezi Simiyu.
ACP Jonathan Shana amefariki akiwa Afisa Mnadhimu katika Chuo cha Polisi (CCP) Moshi
Pia soma >>>
RPC Shana anavyotikisha Arusha, awadaka Majangili hatari, AK 45, Meno ya Tembo
Watu 9 waliohusika kutungua chopa na kumuua rubani wakamatwa