JamiiForums imemtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Kaster Ngonyani kuhusiana na tukio hilo ambapo amesema "Ndio ni kweli, taarifa za tukio hilo lipo na tayari tumeshaenda eneo la tukio na Mgonjwa sasa hivi yupo Hospitali ya Wilaya ya Mlele eneo Mpigwe Kibaoni
SACP Ngonyani amesema Sativa aliokotwa Usiku wa Kuamkia Juni 27, 2024 Barabarani maeneo ya Pori la Hifadhi ya Taifa ya Katavi (Barabara ya Msimbwe Majimoto inayoelekea Mpanda.
Pia soma:
Sativa225 (Edgar Mwakabela) kijana maarufu kwa kukosoa serikali X apatikana, baada ya kutekwa na watu wasiojulikana
Ameongeza "Mgonjwa ameongea Mwenyewe japo kwa shida amesema alikamatwa na Watu Juni 23 Mbezi kwa Msuguri, kisha akapelekwa Mkoani Arusha katika sehemu ambayo haijui na baadaye kuletwa Katavi ambapo alipigwa na kitu chenye ncha kali ambacho anasema kilitokea mdomoni kisha Wakamtupa kwenye msitu huo na kutoweka
Amesema "Mgonjwa alijikokota kutoka Porini hadi Barabarani ambapo Wasamaria wema walimwona na kumpakia kwenye gari kisha kumpeleka Hospitali. Aliongea kidogo sana kwa sasa haongei. Tunasubiri taarifa ya Daktari kuhusu alichomwa na kitu gani.