Hapana naamini ni Mr DJ huyo wa Chadema ndio mtuhumiwa wa ugaidiBashite ndiye bosi wa kundi la wasiojulikana hivyo walienda Arusha kumuonyeha kuwa kazi uliyotutuma hii hapa naye akatoa maelekezo wamuue kisha wakamtupe katavi aliwe na wanyama kupoteza ushahidi.
Hivi Wanasiasa wana roho na mioyo ya kawaida kweli! Yaani kirahisi tu unafikia hatua ya kujeruhi au kuyaondoa kabisa maisha ya binadamu mwenzako, kisa tu hutaki kukosolewa!!JamiiForums imemtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Kaster Ngonyani kuhusiana na tukio hilo ambapo amesema "Ndio ni kweli, taarifa za tukio hilo lipo na tayari tumeshaenda eneo la tukio na Mgonjwa sasa hivi yupo Hospitali ya Wilaya ya Mlele eneo Mpigwe Kibaoni
SACP Ngonyani amesema Sativa aliokotwa Usiku wa Kuamkia Juni 27, 2024 Barabarani maeneo ya Pori la Hifadhi ya Taifa ya Katavi (Barabara ya Msimbwe Majimoto inayoelekea Mpanda.
Pia soma: Sativa225 (Edgar Mwakabela) kijana maarufu kwa kukosoa serikali X apatikana, baada ya kutekwa na watu wasiojulikana
Ameongeza "Mgonjwa ameongea Mwenyewe japo kwa shida amesema alikamatwa na Watu Juni 23 Mbezi kwa Msuguri, kisha akapelekwa Mkoani Arusha katika sehemu ambayo haijui na baadaye kuletwa Katavi ambapo alipigwa na kitu chenye ncha kali ambacho anasema kilitokea mdomoni kisha Wakamtupa kwenye msitu huo na kutoweka
Amesema "Mgonjwa alijikokota kutoka Porini hadi Barabarani ambapo Wasamaria wema walimwona na kumpakia kwenye gari kisha kumpeleka Hospitali. Aliongea kidogo sana kwa sasa haongei. Tunasubiri taarifa ya Daktari kuhusu alichomwa na kitu gani.
Aisee na mimi ngoja tu nirudi kwenye jukwaa langu la michezo. Huku ngoja nimwachie Lucas Mwashambwa ili aendelee kulitetemesha jukwaa na wanaiasa wenzake kutoka CHADEMA.Bora tuendelee kubishana juu ya Simba na Yanga, huko kwingine muda wowote parapanda inaweza lia juu yetu.
Na yeye auwawe tuMtekaji huyu hapa
Hili jamaa linanuitaga Ummy Mwalimu Odo ake🤣Mtekaji huyu hapa
itakuwa risasi, cha kushukuru Mungu si ukute risasi haijagusa hata mfupa wala mshipa, Mungu mkubwa. hata kama mtu amekukosoa vibaya na kwa uwongo, ndio ufanye hivi jamani? ubinadamu upo wapi? hii dunia juu mbinguni huko kuna mbabe wa kila mtu, God is watching, msijiona wababe sana, yupo Mungu mbinguni.Hicho kitu chenye ncha kali kilichotokea mdomoni,kiliingilia eneo gani la mwili wake mpaka kikatokea mdomoni?
Ndo nimejiuliza hapoo tyuuuh.Hicho kitu chenye ncha kali kilichotokea mdomoni,kiliingilia eneo gani la mwili wake mpaka kikatokea mdomoni?
Anaitwa nani? Afu hafananii na tabia ya wasiojulikana.Mtekaji huyu hapa
Tangu Mello ateuliwe kwenye kamati ya ulinzi wa nn sijui hakuna tena uhakika wa uhuru humu.Huko X wakosoaji wengi wako hatarini, humu kwenyewe watu wawe makini hamko safe km mnavyofikiria.
"Chezea ndevu usichezee dola "
Alisema nani huu ushauri?
Kwa upande mwingine Sativa alikuwa ni mtu wa mitusi mikubwa ya nguoni. Tujifunze tuAnaitwa nani? Afu hafananii na tabia ya wasiojulikana.
Soma miitusi ya Sativa hapa:Aulizwe mwenyekiti wa uvccm kagera Faris Buruhan.
Sativa alikuwa anatukana utadhani hakuzaliwa na mwanamkeHuu ni upumbavu, unakwenda kumteka, kumuumiza mtu mdogo kama huyu ambaye hana madhara yoyote zaidi ya kubwabwaja Tu mitandaoni.
Haya ni matumizi mabaya ya Dola.