Mkuu kongole. Mimi nimefahamu kwamba watu waachiwe watoe maoni, yaangaliwe, na yafanyiwe kazi. Hakuna tatizo ktk hilo. Tatizo ni pale unapoenda zaidi na kuhamasisha watu waichukie serikali, kufanya uchochezi na zaidi kuhamasisha kuondoa uongozi ulioko madarakani kwa nguvu (kufanya mapinduzi).
Mkuu haya ya kufanya uchochezi na kuhamasisha watu kufanya Mapinduzi yanatoka wapi?
Kumekuwa na mawazo kuwa kwenye suala hili tumegawanyika. Haijulikani ni nani wapi salama.
"Kwamba imekuwa ni udini, uzanzibari na utanganyika?"
1. Hivi ndugu zetu kina Mwaipopo au Assad na wa namna hiyo hawaioni hoja ya kisheria hapa?
2. Hivi ndugu zetu wazanzibari kina
Zawadini au Fatma karume kulikoni kufumba macho leo dhidi ya kamata kamata hIzi na hata kuona kuna uhaini hapa? Si kuwa kumbe panakuwapo damu iliyo nzito kuliko maji hapa?
3. Kulikoni suala hili kuwa ni Zanzibar dhidi ya Tanganyika? Kulikoni kuwa ni suala la bandari za bara lakini si Zanzibar?
Kwamba Zanzibar hawalioni hilo na kuwa mlipo sasa mnatushangaa mno tunapopaza sauti kuuonyesha kutokuridhishwa kwetu?
Haya ya kupakaziana uhani si ni yale yale yakiwasibu Maalim, CUF, masheikh wa uamsho nk sote tukiyapigia kelele tokea enzi za Mkapa?
Ndugu zetu katika mapambano, nini kimebadilika au kinewasibu leo?
Ni kwa vile kuna mzanzibari, mwanamke au mwislamu madarakani anayeyafanya yale yale leo?
Kwamba nyie leo mmeuona huu ni uhaini?
Bwana
Zawadini nikiamini wewe kama mmoja wa wale wajumbe nguli aliye muadilifu katika mapambano tokea pande za huko, nini kimekupata ndugu yangu?
"Nini kimewapata ndugu zetu? Kulikoni kigugumizi hiki?"
Kwa hakika leo nakuona kama walivyonishangaza Prof. Assad na Fatma Karume.
"Umeniacha njia panda."