Hawashindwi ila katika hili la sasa mbona watu wameonekana na kusikika,
Kama hawashindwi si ndiyo haya waswahili huita akutukanaye hakuchagulii tusi ndugu? Lini watataka kumbambikizia nani nini huo ni uchaguzi wao.
Mkuu hapa swala sio kuridhika au kutoridhika, kuziheshimu au kutokuziheshimu bali swala ni kwamba sheria zipo na hivyo ni lazima kufuatwa. Kuzivunja kunapelekea kuchukuliwa hatua.
Hata mkoloni sheria alikuwa nazo. Ndiyo maana kutwa kucha tunapogania katiba mpya Ili kuwa na sheria za haki Enye kukubaliwa Kwa haki na sote.
Sheria mbaya hukataliwa. Sheria hazitoku Kwa mwenyezi Mungu. Miito ya kuziangusha serikali Kwa mujibu wa Katiba haliwezi kuwa haramu.
Hawa ndo wanatakiwa kutoa tafsiri ziwe sahihi au zisiwe sahihi na nini cha kufanya pale mtu asiporidhika zimewekwa, ni wajibu wetu kuzifuata.
Hawa ndugu wanashikiliwa kinyume cha sheria. Hakuna shaka kuwa unajua mtu akikamatwa ndani ya masaa 24 inabidi awe kafikishwa mahakamani. Kumbe wewe nani kutofuata yeye sheria unakuona wewe ni sawa?
Hawa ulotutaja tuko unprncipled kwa maoni yako. Unao uhuru wa mawazo huenda ukweli utajulikana kwamba walioko unprincipled
Asante Kwa kutambua ni Kwanini ninalazimika kuwaita unprincipled na kwamba si from nowhere!
Huenda haya unayodai ya unafiki ni kwasababu ya kutofanya yale unayoyataka wewe. Ni ajabu!! Hivi wewe hali (status) yako ni ipi? Jee wewe ni kiherehere, kitimbakwiri au nani hasa?
Mimi ninasimama na ndugu huyu ambao ndiyo ulio ukweli mchungu:
Si swala la mkuki kwa ngurue, Uzanzibari, udini wala njaa. Pia si swala la kuona vionjo vya kuiondoa serikali bali swala ni kutamka hadharani swala la kuiondoa serkakali.
Kwa hiyo kwako wewe haipo tofauti ya kutamka mapinduzi na kupanga mapinduzi? Kwamba kumbe hawa wanashtakiwa Kwa kutamka mapinduzi Wala si kupanga mapinduzi?
Ni kichekesho na ni akili za kitoto kudhani kwamba kuiondoa serikali kinyume cha sheria ni halali. Huku ni kuishiwa na hoja, kushindwa na kukosa hekima. Haifanani kwako kuyadai haya. Nakusihi fikiri kwanza kabla hukuanza kuandika.
Uhalali wa serikali ni upi? Seif alipokuwa hamtambui SheIn hadharani, uliwahi kudokeza popote au kumuasa kuwa ulikuwa ni uhaini? Au ilikufikirisha kwanini hakukamatwa kwa uhaini?
Hili nalo ni kukosa na kuishiwa na hoja. Hivi unamfananisha Amini na mama Samia? Huku ni kukosa uelewa na kutokufikiri. Tafakari.
Amini na wote wafanyao yoyote kinyume na matakwa ya umma hawawezi kujinasibu kuwa ni tofauti. Wote ni wahalifu kama wowote.
"Zingatia kibaka ni kibaka TU hata kama yuko kwenye V8."
Kwamba wewe unayo tofauti ya tafsiri ya neno kibaka?
Uhalali wa serikali unakoma unapojinyakulia haki za raia na uka geuka kuwa wabakaji. Jiridhishe kuhusiana na kadhia ya bandari za bara kukabidhiwa dp world lakini Siyo za Zenji. Hiyo ikiwa bila ya ridhaa ya wabara.
Kwamba ni hoja yako tutulie tuli mbakaji amalize starehe zake Kwa amani? Kwamba hiyo ndiyo hoja yako Bora kabisa kwenye hili?
Kwamba unakwazija kuona tunasimama kuupinga ubakwaji huu? Bado tusijiulize nini kimekupata wewe au wenzetu tokea Zanzibari huko?
Kwa mwenendo huu na utaratbu huu ni kweli Wazanzibari, kama mimi, siko tayari kuwa mshirika katika hili
"Hapa ndipo hatutaacha kukumbushana ya Martin Luther."
Hii ni Leo na hata milele!
Mkuu kama ni udini basi wewe brazaj unaongoza na haya maandiko yako yanathibitisha hayo. Hivi la kuwa rais ni mwenzetu linkuja sasa? Mlikuwa wapi wakati watu waliponyanyaswa nanyi mukakaa kimya kwa kuwa wao ni Wazanzibari?
Nikukumbushe tena mrejee brazaj tangia 26 Nov 2016 alipotia timu. Kulikoni kutaka kumnyooshea kidole ndugu huyu kabla ya siku hiyo pasipo na kufahamu kabla ya hapo alikuwa wapi na hata kama alikuwa Bado kuzaliwa?
Nakukumbusha tu akina Juma Duni walishitakiwa kwa uhaini sikumsikia brazaj akipaza sauti hadi pale mahakama lipoamua hakuwezi kufanyika Zanzibar kwa kuwa sio nchi? Ulikuwa wapi wakati masheikh waliposhiliwa kwa miaka zaidi ya tisa? Huo haukuwa udini, haukuwa ubaguzi, haukuwa umajimbo? Iweje leo liwe jambo kwasababu tu wanaoshikiliwa ni wale wenye imani moja nawe, ni wale wenye asili moja nawe?
Ninakukumbusha Tena kuyarejea maandiko ya brazaj tokea 26 Nov 2016 kuhusu haki. Bila
kusahau kuihusu Zanzibar, Maalim Seif na wote uliowataja wakiwamo masheikh wa uamsho. Ya nini kuandika mate?
Nipende kukutaarifu brazaj hakuwahi kukaa kimya au kuacha kukerwa na ubaguzi wowote na hata kama mbaguzi huyo alitaka kuwa zawadini ambaye mapema nikimtambua kama mshirika mwaminifu wa siku zote kabla ya maandiko yako haya.
Lini nimewahi kuwa na simile na wabaguzi tokea kokote watokako hata kama ingekuwa mbinguni? Kama wao kama wewe sitakufumbia macho kwenye hili!
Kwenye hili nitakuwa mchoyo wa fadhila kutokuwafahamisha kuwa: "mme boogie!"
Mimi Zawadini nitaendelea kuunga mkono juhudi za kupata haki kwa kutumia njia za kistaarabu na kamwe staunga mkono wabaguzi wa aina yoyote. Hatuna budi siku zote jembe tuliite jembe
Hayupo anayetaka Shari. Hata hivyo waliotambua amani kutopatikana ila kwa ncha ya upanga hawakukosea.
Kwamba tunataka haki? Kwamba iwe kwa vipi? Hayo hayawezi kuwa Kwa utashi au uchaguzi wa maadui zetu.
Huo ndiyo ulio ukweli mchungu kwa huyu ndugu yenu na hasa kama mwampenda.
Atatawala si kwa matakwa yake, bali Kwa mujibu wa Katiba!