Kamati: Kinyesi na Mikojo ya Mifugo ndiyo chanzo cha kufa samaki mto Mara, sio sumu ya maji ya Migodini

Kamati: Kinyesi na Mikojo ya Mifugo ndiyo chanzo cha kufa samaki mto Mara, sio sumu ya maji ya Migodini

Nchi nzima inajua kwamba ile report ni ya mchongo na kufanyana wajinga, kwa mwendo huu sasa samaki wa ziwa victoria ni hatari kuwala maana cows washasingiziwa na mabeberu yako huru kumwaga sumu zao mtoni maana profesa keshatoa majibu ya utafiti wake na tume yake isiyoeleweka

Pamoja na mapungufu ya the late Jpm kwenye hili uhakika ni kwamba angesimama na raia
Utafiti unapingwa kwa utafiti, ni vyema uwepo utafiti mbadala ili kupinga sio maneno tu.
 
nakuhakikishia kwenye hili angesimama na walaji samaki na afya za wana mara na huyo Jaffo angekuwa keshatimuliwa zamani

Ungeweza kuweka utetezi wako bila kutaka kutuonyesha Magufuli alikuwa bora kwa hivyo. Ripoti ya uongo ya Ossoro ilikuwa chini yake, na hawa wameiga kupika ripoti.
 
Hii nchi ina vituko sana, wanafanya yote Haya sababu wanajua hatuna cha kufanya zaidi ya kulalamika mitandaoni tu.!
 
Utafiti unapingwa kwa utafiti, ni vyema uwepo utafiti mbadala ili kupinga sio maneno tu.
utafiiti kwamba kinyesi cha cows kinaua samaki? jamani mbona tunalazimisha kufanyana wajinga? haya maprofesa ya nchi hii nayo sifuri kabisa
 
Ungeweza kuweka utetezi wako bila kutaka kutuonyesha Magufuli alikuwa bora kwa hivyo. Ripoti ya uongo ya Ossoro ilikuwa chini yake, na hawa wameiga kupika ripoti.
sijawahi kuwa shabiki wake report ya mchongo ya kipindi kile ilikuwa kulazimisha mabeberu yatoe hela ndefu ila ya safari hii ni kutoa green lights ya wana mara kuendelea kuugua cancer na wala samaki wa mto mara na ziwa victoria..asingekaa kimya huku mabeberu yakimwaga sumu mtoni
 
Ndiyo madhara ya kuwatunuku vyeo vikubwa wapumbavu. Hii ripoti ndiyo zile Lisu husema ni professorial rubbish. Yaani professor anatuambia kuwa:

1 - Hao ng'ombe hawanyi na kukojoa sehemu nyingine yo yote isipokuwa wanafanya hivyo wakifika mtoni tu kama fungo na humo wanakunya kilo zote 25 na mikojo lita 21?

2 - Na kwamba mto mara hautiririshi maji kuondoa hicho kinyesi?
 
Mmhh,ila kuhusu kinyesi jamani mmh...nitakuwa Sasa siamini tafiti yoyote yule ya msomi wa kitanzania,walakini na maswali ya kujiuliza ni mengi mnoo,Yani hadi unakosa hata hamu...hizi tafiti inabidi zijibu maswali mengi sana.
 
sijawahi kuwa shabiki wake report ya mchongo ya kipindi kile ilikuwa kulazimisha mabeberu yatoe hela ndefu ila ya safari hii ni kutoa green lights ya wana mara kuendelea kuugua cancer na wala samaki wa mto mara na ziwa victoria..asingekaa kimya huku mabeberu yakimwaga sumu mtoni

Huu ni mwendelezo wa ripoti za kupika. Kama ripoti za kupika zinatoa hela, basi ile $192b waliyosema tunawadai Barrick tungelipwa. Tukatae ripoti yoyote ya kupika, na sio kufurahia ripoti ya kupika ili kujipatia fedha, ambayo wala hatukuzipata zaidi ya kuonekana majuha. Nasema iseme ripoti hii ya kupika, lakini usimtaje mtu muongo ili kumpa kick asiyostahili.
 
Wataalamu wa humu watusaidie,kuhusu kinyesi na mikojo ya hao wanyama tajwa ni kweli ndio inaleta shida hizo?...wataalamu!
 
Musoma. Kamati maalum ya kitaifa iliyoundwa na serikali kuchunguza mabadiliko ya maji ndani ya mto Mara, imetoa taarifa ya chanzo cha mabadiliko katika mto huo yaliyosababisha maji kuwa meusi na kutoa harufu, huku samaki wakifa ambapo chanzo kimeelezwa kuwa ni shughuli za binadamu pamoja na nguvu za asili....
Dr Joseph Musukuma Yeye ni mfugaji Ana maoni gani kuhusu majibu ya hii Kamati?
 
Back
Top Bottom