Kamati: Kinyesi na Mikojo ya Mifugo ndiyo chanzo cha kufa samaki mto Mara, sio sumu ya maji ya Migodini

Kamati: Kinyesi na Mikojo ya Mifugo ndiyo chanzo cha kufa samaki mto Mara, sio sumu ya maji ya Migodini

Ngombe hawa hawa wa mara mmoja anakunya kinyesi cha kg 25 na mkojo lita 21..???

Hivi wanaficha nini kwa manufaa ya nani?..hivi hiyo mifugo imeanza kufungwa mwaka huu maeneo hayo..mbona hayakuwahi kutokea hayo.?

Nadiriki kusema hii ni moja ya kamati za michongo...hivi wanadhani watanzania wasasa ni vilaza sana kwamba hawajui kuhoji au ku reason.

Eti mwenyekiti wa kamati ni professor..daah hii nchi kuna mambo yanakera sana..

Hivi hamna huruma na wananchi kansa kila uchwao zinaongezeka kanda ya ziwa..magonjwa ya ajabu ajabu..sasa hadi samaki wanakufa..ila mnaleta ngonjera.

#MaendeleoHayanaChama
Haya yote ndiyo gharama ya kuruhusu vibaka katawala nchi.The worst is yet to come.
 
Now we talking buddy...Ila ukifanya leachinga kwa kutumia Sodium Cyanide as the main lixiviant katika PH ndogo basi moja ya by products itakua HCN (Hydrogen cyanide gas) ambayo tofauti na ulivoelezea kwamba CN- hupoteza nguvu kwenye hewa,...Cyanide ikiwa kwenye form ya gaseous(HCN) ni more toxic kuliko unavodhani.

Kingine nachokubaliana na wewe watu wengi wana comment kwa mihemko tu,kabla tailings (Uchafu) unaotoka kwenye CIP tanks haujapelekwa kwenye bwawa la kutunzia mabaki ya tope lisilo na dhahabu (Tailing Storage Facility {TSF}) bas kiwango cha cyanide kilichobaki kwenye tope hilo huakikiwa ili kukidhi WAD cyanide ambayo kitaalamu concentration inatakiwa iwe below 50 ppm ikiwa zaidi ya hapo bas hufanyika dilution kupunguza makali ya cyanide kufikia hio 50 ppm ili tope lipate idhaa ya kuingia TSF
 
Hadi hali hii kufikia hivyo, manaake ni kwamba; kuna uzembe wa maafisa maliasili, mifugo, afya na hata waziri husika wa mazingira!

Inamaanisha, kabla ya samaki kukosa hewa na hatmaye kufa, wananchi walitumia maji yenye kinyesi na mkojo wa wanyama?

Hapa bado kuna viongozi wanapaswa kuwajibishwa, japo wanajaribu kuwatupia mzigo wananchi! Ni jitihada gani zilishafanyika kuwasaidia hali hiyo isijitokeze na kuleta madhara kwa viumbe hai waishio ndani na nje y

a mto?
I wish Magu angekuwepo🤔🙌
 
Kazi ipo
IMG-20220320-WA0009.jpg
 
Ina maana hamuwaamini viongozi mliowachagua wenyewe...?
 
Tumefuga ng'ombe ... Sijawahi ona ng'ombe anajisaidia kinyesi kilo 20-25 kwa siku. Hamna waache kutuona sisi wapuuzi

Halafu mkojo lita 21? Kweli? Kwa nini wanafikiria sisi ni wajinga kiasi hiki?

So ikitokea ng'ombe hajanya au kukojoa kwa siku anakuwa na ongezeko la kilo zipatazo 30-40? Inawezekana kweli?

Jamani msitutukane kiasi hiki. Mtuheshimu kidogo. Huyo ng'ombe wa kutoa kinyesi cha kg 25 kwa siku. Hivi wale ambao tumefuga ng'ombe wa maziwa lets say 10. Kwa siku wana produce kinyesi kilo 250? Kwa siku 10 ni Tani 2.5? Kwa mwezi tani 7.5 ? Kwa mwaka ni zaidi ya Tani 87 ya kinyesi kwa ng'ombe 10. Kweli?

Profesa pleaaseeee....nakuomba propesa usitufanyie hivyo. Nasi tumeenda enda shule kidogo.
Shida ya mbolea isingekuwapo Tanzania
 
Mimi huwa nawaita hawa viongozi wa Tanzania kuwa ni vibaka lakini cha ajabu hapa jukwaani watu huwa wananishangaa na kunilaumu.

Ni vyema sasa watu waanze kujishangaa wenyewe na kujilaumu wenyewe kwa kujidanganya kuwa nchi ina viongozi.
 
Musoma. Kamati maalum ya kitaifa iliyoundwa na serikali kuchunguza mabadiliko ya maji ndani ya mto Mara, imetoa taarifa ya chanzo cha mabadiliko katika mto huo yaliyosababisha maji kuwa meusi na kutoa harufu, huku samaki wakifa ambapo chanzo kimeelezwa kuwa ni shughuli za binadamu pamoja na nguvu za asili.

Akitoa matokeo ya uchunguzi leo Jumamosi Machi 19, 2022 mjini Musoma, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Profesa Samuel Manyele amesema kuwa hali hiyo imetokana na kuwepo kwa kiwango kikubwa cha kinyesi cha mifugo mtoni pamoja na uozo wa mimea ndani ya mto hasa mimea vamizi kama vile magugu maji na matete.

Amesema kuwa hali hiyo ilisababisha kupungua kwa kiasi kikubwa kiwango cha oksijeni ndani ya mto na hivyo maji kubadilika rangi na kuwa na harufu mbaya huku samaki wakikosa chakula na hivyo kusababisha vifo vyao.

Hata hivyo, amekanusha picha zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zilizokuwa zikionyesha samaki wakiwa wamekufa kwa wingi, akisema sio kutoka mkoani Mara.

Amesema kuwa kwa mujibu wa uchunguzi waliofanyana walibaini kuwa mabadiliko hayo ni matokeo ya mvua kubwa iliyonyesha ghafla kwa muda mfupi katika kipindi cha mwezi huu hivyo kutibua uchafu uliokuwa umejikusanya chini ya mto kwa muda mrefu.

"Mvua zingeendelea kunyesha hali hii ingeisha kwani uchafu ungetiririshwa lakini kwa vile mvua zimenyesha na kukatika ghafla ina maana uchafu ule unatoka taratibu na hii hali inaweza kudumu kwa zaidi ya miezi mitatu hadi minne endapo mvua hazitanyesha hapa katikakati," amesema.

Profesa Manyele amesema kuwa mto huo umeathiriwa kuanzia katika kijiji cha Marasibora wilayani Rorya na kijiji cha Wegero wilayani Butiama huku akisema kuwa mgodi wa dhahabu wa Barrick North Mara hauhusiki na uchafuzi huo.

"Mgodi upo mbali sana na maeneo yaliyoathirika na hata kama uchafu unaozalishwa mgodini pale ungezidishwa mara ishirini na kumwagwa mtoni maji yasingebadilika rangi wala kuwa katika hali iivyo sasa na maji ya mto kelekea kule mgodini ni masafi na hayana shida yoyote," amesema.

Amesema kuwa wamebaini uwepo wa kinyesi cha ng'ombe zaidi ya tani 1.8 milioni pamoja na mkojo wa ng'ombe lita 1.5 bilioni uchafu uliotokana na kuwepo kwa ng'ombe zaidi ya laki 3 waliokuwepo katika eneo oevu la mto Mara kwa kipindi cha miezi minane mwaka jana wakati wa kiangazi.

"Ng'ombe mmoja ana toa kilo 25 za kinyesi kwa siku moja na mkojo lita 21 kwa siku kwahiyo ukizidisha kwa idadi hiyo ya ng'ombe mara miezi minane utapata kiwango hicho na hapo bado hatujaweka kinyesi na mkojo wa kondoo, mbuzi na punda," amesema.

Akizungumza baada ya kupokea taarifa hiyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Suleiman Jafo ametoa muda wa siku mbili kwa kamati hiyo kuandaa taarifa kamili yenye mpango kazi juu ya nini kifanyike na muhusika ni nani kisha taarifa hiyo ikabidhiwe kwake kwaajili ya utekelezaji.

"Hii taarifa imenipa faraja baada ya uchunguzi kubaini kuwa hakuna kemikali mtoni maana kama kungekuwa na kemikali hii ingekuwa ni habari mbaya sana lakini taarifa hii inaonyesha kuwa tuna kazi kubwa sana ya kufanya ili mto uweze kuendelea kuwepo na tusipochukua hatua za haraka mto unaweza kupotea," amesema Jafo.

Chanzo: Mwananchi

Pia soma;

1).Vifo vya Samaki Mto Mara: Kamati ya Dharura yaundwa kuchunguza Samaki wanaodaiwa kufa kwa Sumu

2). Madai ya sumu Mto Mara kutoka migodini, wananchi wazuiwa kutumia maji, kula samaki, uvuvi, Serikali yatoa tamko
View attachment 2157025

Kamati: inatambua kuwa Mkoa wa Mara, wananchi leo wameshughudia sangara wakiwa wameelea ziwa victoria wakiwa wamekufa?​

Je kamati inaelewa kuwa mkoa wa mars unatumia maji ya ziwa victoria kwa matumizi ya binadamu na leo hii hakuna maji ya kunywa mkoa wa mara?​

Kamati inatambua leo dagaa hawapstikani tena kwa sabsbu ya dagaa kufa? Waziri Jafo jiuzulu​

 
Huu ni uongo.. Kinyesi cha Ng'ombe kuua samaki..

Hapa kamati wametudanganya...
 
Serikali hii haijali kivile maisha ya Watanzania. Muhimu kwao ni kubaki madarakani, kujitajirisha kwa namna yoyote ile.

Kudanganya mchana kweupe kwao sio issue tena.

Maji yamekuwa meusi,yanatoa harufu samaki wengi wamekufa na wanyama wengine kwa muda fulani (specific time). Unasingizia ngo'mbe.

Soko la nje hata la ndani la samaki (sato, sangara, dagaa nk) linaweza kutoweka tukiendekeza uongo na kutojali ecosystem. Magonjwa mengi ya ajabu kama ya kansa yataongezeka.

Tulete wachunguzi wa kimataifa, watuambie ukweli.
 
Profesa fulani kutoka Tanzania😁😁😁
 
Kwa fikra zako unadhani ni mwekezaji gani kwa namna gani yawezekana akawa amechafua mto Mara?
Naomba kuuliza ni kwa nini basi pale NM kwenye tailings dam wameweka carpet kwa chini ili maji ya processing plant yanaenda hapo kwanza? Na mto Mara uko karibu sana na huo mgodi na maafisa wa mgodi huo huenda mto Mara kufanya water sampling. Why then would they do that....?
 
Back
Top Bottom