Mtoto wa nzi
JF-Expert Member
- Jun 6, 2012
- 10,017
- 18,537
Mifugo ya mara itakuwa inakunya sana ..mzigo wa kilo 25 SI mchezoHao mifugo wameanza kunya leo?
Hao mifugo wanafuga wakazi wa Mara TU?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mifugo ya mara itakuwa inakunya sana ..mzigo wa kilo 25 SI mchezoHao mifugo wameanza kunya leo?
Hao mifugo wanafuga wakazi wa Mara TU?
Haya yote ndiyo gharama ya kuruhusu vibaka katawala nchi.The worst is yet to come.Ngombe hawa hawa wa mara mmoja anakunya kinyesi cha kg 25 na mkojo lita 21..???
Hivi wanaficha nini kwa manufaa ya nani?..hivi hiyo mifugo imeanza kufungwa mwaka huu maeneo hayo..mbona hayakuwahi kutokea hayo.?
Nadiriki kusema hii ni moja ya kamati za michongo...hivi wanadhani watanzania wasasa ni vilaza sana kwamba hawajui kuhoji au ku reason.
Eti mwenyekiti wa kamati ni professor..daah hii nchi kuna mambo yanakera sana..
Hivi hamna huruma na wananchi kansa kila uchwao zinaongezeka kanda ya ziwa..magonjwa ya ajabu ajabu..sasa hadi samaki wanakufa..ila mnaleta ngonjera.
#MaendeleoHayanaChama
Now we talking buddy...Ila ukifanya leachinga kwa kutumia Sodium Cyanide as the main lixiviant katika PH ndogo basi moja ya by products itakua HCN (Hydrogen cyanide gas) ambayo tofauti na ulivoelezea kwamba CN- hupoteza nguvu kwenye hewa,...Cyanide ikiwa kwenye form ya gaseous(HCN) ni more toxic kuliko unavodhani.
Kingine nachokubaliana na wewe watu wengi wana comment kwa mihemko tu,kabla tailings (Uchafu) unaotoka kwenye CIP tanks haujapelekwa kwenye bwawa la kutunzia mabaki ya tope lisilo na dhahabu (Tailing Storage Facility {TSF}) bas kiwango cha cyanide kilichobaki kwenye tope hilo huakikiwa ili kukidhi WAD cyanide ambayo kitaalamu concentration inatakiwa iwe below 50 ppm ikiwa zaidi ya hapo bas hufanyika dilution kupunguza makali ya cyanide kufikia hio 50 ppm ili tope lipate idhaa ya kuingia TSF
Hao samaki wangechunguzwa kwenye miili yao halafu wagundue ni kipi kilichokuwa accumulated. Hii ingetoa mwanga wa kuanzia.
Huwa najisikia vibaya nikiona profesa anakuwa hivi.
Wapo sahihi kutuona kuwa sisi ni wajinga kwa sababu tungekuwa werevu tusingeruhusu vibaka kushika dola.Hawa wapumbavu wanatugeuza sisi wajinga
nwnl.blog
Shida ya mbolea isingekuwapo TanzaniaTumefuga ng'ombe ... Sijawahi ona ng'ombe anajisaidia kinyesi kilo 20-25 kwa siku. Hamna waache kutuona sisi wapuuzi
Halafu mkojo lita 21? Kweli? Kwa nini wanafikiria sisi ni wajinga kiasi hiki?
So ikitokea ng'ombe hajanya au kukojoa kwa siku anakuwa na ongezeko la kilo zipatazo 30-40? Inawezekana kweli?
Jamani msitutukane kiasi hiki. Mtuheshimu kidogo. Huyo ng'ombe wa kutoa kinyesi cha kg 25 kwa siku. Hivi wale ambao tumefuga ng'ombe wa maziwa lets say 10. Kwa siku wana produce kinyesi kilo 250? Kwa siku 10 ni Tani 2.5? Kwa mwezi tani 7.5 ? Kwa mwaka ni zaidi ya Tani 87 ya kinyesi kwa ng'ombe 10. Kweli?
Profesa pleaaseeee....nakuomba propesa usitufanyie hivyo. Nasi tumeenda enda shule kidogo.
Yaliyotokea 2020..sio hata ya kuongea kwa ufupi hatuna viongozi wanaotokana na wanachi.Ina maana hamuwaamini viongozi mliowachagua wenyewe...?
Musoma. Kamati maalum ya kitaifa iliyoundwa na serikali kuchunguza mabadiliko ya maji ndani ya mto Mara, imetoa taarifa ya chanzo cha mabadiliko katika mto huo yaliyosababisha maji kuwa meusi na kutoa harufu, huku samaki wakifa ambapo chanzo kimeelezwa kuwa ni shughuli za binadamu pamoja na nguvu za asili.
Akitoa matokeo ya uchunguzi leo Jumamosi Machi 19, 2022 mjini Musoma, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Profesa Samuel Manyele amesema kuwa hali hiyo imetokana na kuwepo kwa kiwango kikubwa cha kinyesi cha mifugo mtoni pamoja na uozo wa mimea ndani ya mto hasa mimea vamizi kama vile magugu maji na matete.
Amesema kuwa hali hiyo ilisababisha kupungua kwa kiasi kikubwa kiwango cha oksijeni ndani ya mto na hivyo maji kubadilika rangi na kuwa na harufu mbaya huku samaki wakikosa chakula na hivyo kusababisha vifo vyao.
Hata hivyo, amekanusha picha zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zilizokuwa zikionyesha samaki wakiwa wamekufa kwa wingi, akisema sio kutoka mkoani Mara.
Amesema kuwa kwa mujibu wa uchunguzi waliofanyana walibaini kuwa mabadiliko hayo ni matokeo ya mvua kubwa iliyonyesha ghafla kwa muda mfupi katika kipindi cha mwezi huu hivyo kutibua uchafu uliokuwa umejikusanya chini ya mto kwa muda mrefu.
"Mvua zingeendelea kunyesha hali hii ingeisha kwani uchafu ungetiririshwa lakini kwa vile mvua zimenyesha na kukatika ghafla ina maana uchafu ule unatoka taratibu na hii hali inaweza kudumu kwa zaidi ya miezi mitatu hadi minne endapo mvua hazitanyesha hapa katikakati," amesema.
Profesa Manyele amesema kuwa mto huo umeathiriwa kuanzia katika kijiji cha Marasibora wilayani Rorya na kijiji cha Wegero wilayani Butiama huku akisema kuwa mgodi wa dhahabu wa Barrick North Mara hauhusiki na uchafuzi huo.
"Mgodi upo mbali sana na maeneo yaliyoathirika na hata kama uchafu unaozalishwa mgodini pale ungezidishwa mara ishirini na kumwagwa mtoni maji yasingebadilika rangi wala kuwa katika hali iivyo sasa na maji ya mto kelekea kule mgodini ni masafi na hayana shida yoyote," amesema.
Amesema kuwa wamebaini uwepo wa kinyesi cha ng'ombe zaidi ya tani 1.8 milioni pamoja na mkojo wa ng'ombe lita 1.5 bilioni uchafu uliotokana na kuwepo kwa ng'ombe zaidi ya laki 3 waliokuwepo katika eneo oevu la mto Mara kwa kipindi cha miezi minane mwaka jana wakati wa kiangazi.
"Ng'ombe mmoja ana toa kilo 25 za kinyesi kwa siku moja na mkojo lita 21 kwa siku kwahiyo ukizidisha kwa idadi hiyo ya ng'ombe mara miezi minane utapata kiwango hicho na hapo bado hatujaweka kinyesi na mkojo wa kondoo, mbuzi na punda," amesema.
Akizungumza baada ya kupokea taarifa hiyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Suleiman Jafo ametoa muda wa siku mbili kwa kamati hiyo kuandaa taarifa kamili yenye mpango kazi juu ya nini kifanyike na muhusika ni nani kisha taarifa hiyo ikabidhiwe kwake kwaajili ya utekelezaji.
"Hii taarifa imenipa faraja baada ya uchunguzi kubaini kuwa hakuna kemikali mtoni maana kama kungekuwa na kemikali hii ingekuwa ni habari mbaya sana lakini taarifa hii inaonyesha kuwa tuna kazi kubwa sana ya kufanya ili mto uweze kuendelea kuwepo na tusipochukua hatua za haraka mto unaweza kupotea," amesema Jafo.
Chanzo: Mwananchi
Pia soma;
1).Vifo vya Samaki Mto Mara: Kamati ya Dharura yaundwa kuchunguza Samaki wanaodaiwa kufa kwa Sumu
2). Madai ya sumu Mto Mara kutoka migodini, wananchi wazuiwa kutumia maji, kula samaki, uvuvi, Serikali yatoa tamko
View attachment 2157025
😁😁😁Angekuwepo angesema kwani mie ndio nimewatuma mkanye mjaze vyoo 😃😃 yule mzee fuse zilikata
Kwamba kwa siku nne ngombe anakunya gunia zima!?[emoji856]Ng'mbe mmoja kinyesi 25kg kwa siku + 21 Lita za mkojo???????????? Sijawahi kufuga lakini hapa....Ngumu kumeza
Naomba kuuliza ni kwa nini basi pale NM kwenye tailings dam wameweka carpet kwa chini ili maji ya processing plant yanaenda hapo kwanza? Na mto Mara uko karibu sana na huo mgodi na maafisa wa mgodi huo huenda mto Mara kufanya water sampling. Why then would they do that....?Kwa fikra zako unadhani ni mwekezaji gani kwa namna gani yawezekana akawa amechafua mto Mara?