Kamati: Kinyesi na Mikojo ya Mifugo ndiyo chanzo cha kufa samaki mto Mara, sio sumu ya maji ya Migodini

Kamati: Kinyesi na Mikojo ya Mifugo ndiyo chanzo cha kufa samaki mto Mara, sio sumu ya maji ya Migodini

Manyere.jpg
 
Mi naona mheshimiwa Jafo angeunda kamati nyingine na mwenyekiti wa kamati iyo awe King Msukuma,majibu yatakayotoka ndio nitayaamini
 
Mi naona mheshimiwa Jafo angeunda kamati nyingine na mwenyekiti wa kamati iyo awe King Msukuma,majibu yatakayotoka ndio nitayaamini
Hakuwa hata na sababu ya kuunda Tume. Ni uzembe wa maamuzi ktk uongozi. NEMC ni chombo chenye dhamana ya kazi hizo chini ya ofisi yake. Badala yake yeye anaunda Tume chini ya mtu ambaye hata hatujui utaalamu wake. Labda alitaka hadithi kama hizo.
 
Prof. Samuel Manyele wa Tume ya vinyesi vya Ng'ombe Mto Mara.

Unafahamu ulipigwa changa la macho kwa kutokuishirikisha Tume ya madini kwenye tume yako?

Unaijua ukubwa wa leseni ya uchimbaji ya Barrick North Mara?

Nikujulishe tu kuwa leseni hiyo inapakana na Mto mara kwa kilometa moja na eneo hilo hilo ndipo ilipo bwawa la kuweka maji machafu yenye sumu kutokea mgodini.

Ninakushauri tume ya madini ikushauri ili uweze kuokoa maisha ya mto mara.

Kwenda kukaa mto Kirumi na kupima umbali kwenda mgodini kupitia Tarime umedanganywa.

Ukitaka pima umbali kutoka mgodini kupitia barabara ya kwenda serengeti kupitia mungumu ndipo utapata ukweli kuwa kutoka mto mara kwenda kwenye enoe lilipo bwawa la maji ya sumu ni pua na mdomo.
 
Ng'mbe mmoja kinyesi 25kg kwa siku + 21 Lita za mkojo???????????? Sijawahi kufuga lakini hapa....Ngumu kumeza
Umebishia buree, ungekuwa umewahi kufuga ng'ombe usingeona ajabu jambo hilo...kwanza kabisa ng'ombe huwa hashibi...

Tafiti zimeonesha kuwa ng'ombe 'hunya' 'mavi' kilogram 24 hadi 42 (kulingana na aina ya ng'ombe

Screenshot_20220324-100211_Chrome.jpg
 
Umebishia buree, ungekuwa umewahi kufuga ng'ombe usingeona ajabu jambo hilo...kwanza kabisa ng'ombe huwa hashibi...

Tafiti zimeonesha kuwa ng'ombe 'hunya' 'mavi' kilogram 24 hadi 42 (kulingana na aina ya ng'ombe

View attachment 2162541
Hivi kuku wa kienyeji na broiler wanakula na kunya kiwango kimoja? Ndio kama ngombe wa Canada na wa Mara. It's simply 'garbage in garbage out'.
 
Katika report ya prof Manyere mkemia mbobezi amesema moja ya vyanzo vya vifo vya samaki ni uwepo wa vimelea vya mafuta. Ni vyema sasa tuchunguze hayo mafuta ni aina gani
 
Bado kidogo, hata hayo mafuta ni sehemu ndogo sana ya uchunguzi, let keep dot.
 
yalikuwa mafuta ya petrol yatokanayo na maozea ya mimea..Kumbukeni hata mimea ukiisaga inatoa mafuta yanaweza endesha gari.Hivyo tukae mkao wa kula
 
yalikuwa mafuta ya petrol yatokanayo na maozea ya mimea..Kumbukeni hata mimea ukiisaga inatoa mafuta yanaweza endesha gari.Hivyo tukae mkao wa kula
Kwahiyo huo mchirizi wa mafuta umeanzia mto mara hadI hoima?
 
Back
Top Bottom