Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (Chadema) inatarajiwa kukutana jijini Dar es Salaam kujadili masuala mbalimbali ya kisiasa, ikiwemo vurugu zilizotokea Oktoba 29, 2025 katika baadhi ya maeneo nchini.
Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, John Heche amebainisha hayo leo Jumanne, Oktoba 11, 2025, muda mfupi baada ya kuripoti katika kituo cha polisi jijini Dar es Salaam na kusisitiza kuwa maandalizi ya kikao hicho yataanza mara moja na kwamba sekretarieti ya chama imeagizwa kuanza maandalizi.
"Chama chetu kimeamua kuitisha kikao cha Kamati Kuu haraka iwezekanavyo. Tutajadili kwa kina nini kimetokea na hatua gani tuchukue kwa upande wetu," amesema Heche.
Heche, ambaye pamoja na viongozi wengine wa Chadema walikuwa wakishikiliwa na polisi kabla ya kuachiwa kwa dhamana, ametoa pole kwa Watanzania, akisisitiza kuwa hawakufanya makubaliano yoyote ya kisiasa kuhusu kuachiwa kwao.
"Tunataka umma ujue, tumeachiwa bila masharti. Hakuna makubaliano yoyote, kwani tunaamini hatuna kosa," ameongeza Heche.