Kamati kuu ya CCM yakutana Mwanza: Yampongeza Rais Magufuli, Walio hama vyama vya Upinzani waongeza Ruzuku ya chama hadi Bil 13

Watanzania wengi walifungwa wakawa wanaishambulia CCM kuwa inanunua wabunge na madiwani wa upinzani pasipo kujua kuwa huo ni mchezo wa kisiasa tena wa kuimarisha uchumi wa chama ongezeko la ruzuku ndani ya chama chochote cha siasa nimoja ya ustawi mkubwa ndani ya chama
Yaan ni zile hesabu za hasi na chana loose and gain

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wazee ni hazina kwa taifa..

Mzee Pinda katoa dira..Watanzania tumuunge mkono.

Kwa hakika watanzania tumebarikiwa sana

Kinachonifurahisha mimi sio sehemu ya watanzania wanafiki.
 

Siasa itikadi na imani, ikiwa biashara hiyo sio siasa bali ni uhuni kama uhuni kama uhuni mwingine.
 
hahahahah, alisharudi kitambooo sisiemu, yani zamani tangia sukari inauzwa kilo Tshs.100/= hadi sasa inauzwa Tshs.2,400/= kwa kilo. hahahahaha
Hivi sukari ni Tshs 2,400/? Hongera magu maana nilisikia ukisema ulipoingia madarakani sukari ilikuwa 5,000/ kwa kilo.
Ila mtu mzima kujaa fix ni noma!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MASANJA KADOGOSA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU MAFANIKIO YA TAASISI HIYO KATIKA MIAKA MINNE YA SERIKALI YA AWAMU YA TANO*

#TRC ilianza kazi rasmi mwezi Machi 2018 na iliundwa kupitia Sheria Na. 10 ya mwaka 2017 ili kuendeleza kazi zilizokuwa zikifanywa na RAHCO na TRL

#TRC imefanikiwa kuanzisha huduma ya usafiri wa treni za mjini (Dar es Salaam) kutoka Posta kwenda Pugu na kutoka Posta kwenda Ubungo

#Kuanzia Julai 2018 TRC imerejesha safari kwa treni za mizigo kutoka Dar es Salaam hadi Kampala nchini Uganda na kusafirisha tani 52,709 za mizigo

#Kuanzia Julai 2019 TRC imerejesha huduma ya treni za mizigo kutoka Dar es Salaam-Tanga-Moshi na kusafirisha tani 4,800 za mizigo

#TRC imeongeza idadi ya abiria kwa treni za mikoani kutoka 411,172 mwaka 2014/15 hadi 578,439 mwaka 2018/19

#Kuanzia 6 Desemba 2019, TRC imerejesha huduma ya usafiri wa abiria kutoka Dar es Salaam kwenda Kilimanjaro

#TRC inatekeleza mradi mkubwa wa ujenzi wa reli ya kisasa "Standard Gauge Railway" awamu ya kwanza kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza yenye kilometa 1,219

#TRC inaboresha reli ya kati kutoka Dar es Salaam hadi Isaka yenye kilometa 970 ambapo mradi huo umetoa zaidi ya ajira 1600

#TRC imeongeza mapato yake kutoka shilingi bilioni 17.4 kwa mwaka 2014/15 hadi bilioni 30 mwaka 2018/19 kwa treni ya mizigo.
 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli amewapongeza Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) kwa kuweza kushinda uchaguzi wa serikali za Mitaa.

Rais Magufuli ambaye ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa ametoa kauli hiyo wakati anafungua Semina ya Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) Inayofanyika Jijini Mwanza .

"Nilianza kwa kuwapongeza kwa kushinda uchaguzi wa serikali za Mitaa na kuwakumbusha kuhusu mageuzi tuliyoyafanya kwenye Chama chetu na mafanikio yaliyopatikana kutokana na mageuzi hayo na mafanikio yaliyopatikana kwa kipindi cha miaka minne ya uongozi wangu" alisema Rais Magufuli

Aliendelea kwa kusema, "Ninyi wajumbe wa NEC ndio vyombo muhimu wa kuleta mabadiliko katika Taifa hili, hayupo mwingine wa kuwasemea na hata patikana kwa sababu serikali hii inaongozwa na Chama cha Mapinduzi".
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…