MASANJA KADOGOSA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU MAFANIKIO YA TAASISI HIYO KATIKA MIAKA MINNE YA SERIKALI YA AWAMU YA TANO*
#TRC ilianza kazi rasmi mwezi Machi 2018 na iliundwa kupitia Sheria Na. 10 ya mwaka 2017 ili kuendeleza kazi zilizokuwa zikifanywa na RAHCO na TRL
#TRC imefanikiwa kuanzisha huduma ya usafiri wa treni za mjini (Dar es Salaam) kutoka Posta kwenda Pugu na kutoka Posta kwenda Ubungo
#Kuanzia Julai 2018 TRC imerejesha safari kwa treni za mizigo kutoka Dar es Salaam hadi Kampala nchini Uganda na kusafirisha tani 52,709 za mizigo
#Kuanzia Julai 2019 TRC imerejesha huduma ya treni za mizigo kutoka Dar es Salaam-Tanga-Moshi na kusafirisha tani 4,800 za mizigo
#TRC imeongeza idadi ya abiria kwa treni za mikoani kutoka 411,172 mwaka 2014/15 hadi 578,439 mwaka 2018/19
#Kuanzia 6 Desemba 2019, TRC imerejesha huduma ya usafiri wa abiria kutoka Dar es Salaam kwenda Kilimanjaro
#TRC inatekeleza mradi mkubwa wa ujenzi wa reli ya kisasa "Standard Gauge Railway" awamu ya kwanza kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza yenye kilometa 1,219
#TRC inaboresha reli ya kati kutoka Dar es Salaam hadi Isaka yenye kilometa 970 ambapo mradi huo umetoa zaidi ya ajira 1600
#TRC imeongeza mapato yake kutoka shilingi bilioni 17.4 kwa mwaka 2014/15 hadi bilioni 30 mwaka 2018/19 kwa treni ya mizigo.