Kamati Kuu ya CHADEMA iliyoongozwa na Tundu Lissu, yateua Wakurugenzi wapya

Nimecheka kwa nguvu kwa hili dua la kuku. Hizi story za cdm itakufa ni za kipindi sana, kabla hata hujavunja ungo, naona umejiunga mwaka juzi basi unadhani umeleta dua jipya.
 
Garubindi kachukua nafasi ya rugemeleza nshala kwani keshatenguliwa?
Rugemaliza Nshala ndio yule mwanasheria aliyekuwa anagombea uwenyekiti wa Tanganyika Law Society?
Na kama ndio huyo Lissu alimpigia kampeni mtu mwingine, by nature nadhani Lissu hakutaka misimamo mingine.
 
Nashukuru kwamba Wachaga awamu hii wamewekwa pembeni.
Ingekuwa bado mfalme Mboya yuko madarakani viongozi wote wangekuwa: Mushi, Kweka, Mallya, Uroki, Uronu nk.
 
Kwa sasa chadema imekuwa kama taasisi tu na sio chama cha upinzani.. sioni hamsha hamsha utadhani hawapo teyar kwa uchaguzi na ni mwaka huu 2025.
Amsha amsha inaletwa na wanachama na wafuasi siyo viongozi kama unavyofikiria! Vyombo vya habari ni huru?????
 
Masonga naona katemwa.
 
Mungu ibariki CHADEMA
 
Uteuzi wa uongozi
Mwezi wa Ramadhani
Hivi vinaweka mbali na waislam
 
Uteuzi wa uongozi
Mwezi wa Ramadhani
Hivi vinaweka mbali na waislam
Unasema kweli?

"Mwezi wa Ramadhani" hapapaswi kuwepo na uteuzi wa viongozi wa kisiasa?

Nadhani CHADEMA kuwa "mbali na waislam", itakuwepo sababu nyingine zaidi ya uteuzi huu.
 
Yaani kwa safu hz muislamu anayejitambua lazima akiogope hiki chama.
Hapo bado hatujajua chrome cha Padri Kitime, Padri Slaa and the likes.
Napata shida sana kujibu mawazo ya namna hii kwa Tanzania yetu hii.
Nashukuru tu kwamba hao unaowaita "...anayejitambua" (bila shaka wewe ukiwa ni mfano wao) siyo wawakilishi wa waTanzania waislamu. Mtatafuta kila njia za kuwagawa waTanzania katika makundi kama haya kwa faida zenu, lakini hamtafanikiwa.
 


Viongozi wetu nawasihi sana, wekeni msisitizo kwenye uwajibikaji makini kwa maslai ya Watanzania wote, Taifa letu limebakiza tumaini moja tu ambalo ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)

Watanzania wote tunawaombea Mungu awalinde na muweze kutuongoza na kulifikisha Taifa letu kwenye kilele cha Mafanikio
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…