Huu uchaguzi wa Chama Kikuu cha upinzani Tanzania , Chadema ndio utakaotoa mwelekeo wa wale Wapambe wanaowaza kuandana ili Katiba ya nchi ifanyiwe marekebisho ili ukomo wa Rais uondolewe.
Kitendo cha Wajumbe wa Chama kinachopigania Demokrasia yenye ukomo wa madaraka ili kuondoa hulka ya Nchi au Chama kuongozwa kwa matakwa ya mtu mmoja kumchagua tena Mbowe kitahalalisha kabisa wale wasanii wanaotaka JPM atawale milele kwa sababu yeye ni kiboko ya mabeberu.
WanaChadema wapemba Demokrasia ya kweli wamshukuru Mbowe kwa kukiongoza Chama kwa miaka 15 kwa mafanikio aliyoyafanya na sasa wampe Muda wa Kupumzika ili chama Kiongozwe na mtu mwingine .
Kwa sasa Mbowe ameunga mkono Juhudi za serikali ya awamu ya Tano kuzuia mikutano ya kisiasa na kuwabana wapinzani kwa kuhudhuria maadhimisho ya siku ya Uhuru.
Mbowe aliungana na Wakoloni kuadhimisha siku ya Uhuru wa CCM huku akijua wazi kuwa Mamilioni ya watanzania wa vyama vya upinzani hawana Uhuru wa kisiasa.
Mamia ya wanasiasa wa Upinzani waliunga mkono Juhudi na kuhudhuria mikutano ya serikali baada ya kutishwa na kulazimishwa lakini Mbowe ameunga mkono kwa hiyari huku akisahau kuwa kwa miaka ninne amewasababishia watanzania kwa maelfu maumivu makali kwa matamko yake ya kususia shughuli zote za serikali hata zile za maendeleo.
Tunataka kuondoa Ukabila na ukanda kama Ule anaoueneza yule wa CCM kwa kusema kuwa kura za Kanda ya ziwa zinatosha kumpata Rais.
Tuondoe wazo kuwa kura za Moshi tu zinatosha kumfanya Mbowe awe mwenyekiti wa kudumu wa Chadema .
Kura yako iwe ni :-
... ... TANZANIA VS UKANDA.
Sent using
Jamii Forums mobile app