Kamati Kuu ya CHADEMA, mkiteua wabunge wa Viti Maalumu kuingia Bungeni, mtakuwa mmefanya kosa kubwa sana

Au unategemea wafuasi wa vyama vya upinzani watakataa kulipa kodi?
Kodi zitalipwa na wote (wapinzani na wasio wapinzani). Lkn kodi zetu ni kiduchu hazitoshelezi mahitaji yetu ya kibajeti.

Ndiyo maana wahisani ni muhimu Sana. Sasa wakigoma kusaidia ni pigo kwa watawala.
 
CCM ya Magulifu ina vituko hajawaigi shinda huyu 2015 masai hii antipa jamaa zao la hewa
 
Kwa msiojua sheria za uchaguzi, tayari majina ya wabunge viti maalum yalikwishapelekwa.

Kwa mujibu wa sheria za Uchaguzi, majina ya viti maalum hupelekwa walau siku 30 kabla ya uchaguzi mkuu. Hivyo majina hayo yapo na jina la kwanza ni Halima Mdee, la pili Esther Bulaya n.k....
 
Ni kweli. Kilichosubiriwa ni idadi ya hao viti maalumu. Inaonekana nafasi hizo kwa chadema zimeongezwa makusudi. Kwasabb hawakustahili idadi kubwa namna hiyo. Ilipaswa kuwa 8 -13
 
vile bunge litakua kijani kitupu kila hoja ndio mzee yajayo yanashangazaa
 

Wasiposikiliza haya si wapinzani
 
Yaani wafanyiwe kila aina ya uharamia halafu waingie bungeni kwa njia ya asante NEC?.

Huu siyo muda wa kugawana nafasi za kula, kuingia bungeni ni kulegitimise mchakato haramu.

Nawaomba sana Chadema wasifuate misimamo ya waliosurrender, wakifanya hivyo kwanza hawataweza kuisaidia nchi kupiga hatua katika demokrasia nchini.
Pili CCM itarudia tena na tena kufanya hii michezo ya kupora haki za wananchi kwa sababu inajua wapinzani at the end of the day watakubali tu.

Mapambano sasa hivi yawe ni kudai katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.

Hao wanaopendekeza eti wabunge wa viti maalum waingie bungeni, waende wakafanye nini kama serikali na wabunge wa kuchaguliwa wamepatikana bila ridhaa ya wananchi? , Sasa waende bungeni wakamtetee nani?, katika nini, ili wasikilizwe na nani?

Muachieni Magufuli bunge lake, Mkiingia huko mtaudissapoint umma kwa kiwango ambacho hakijawahi kutokea.

Msiwasikilize influencers wa CCM waliotumwa humu mirandaoni kujaribu kushape opinion zenu ili mkubali kuhalalisha haramu.

Najua mnahitaji ruzuku na michango ya wabunge ya kila mwezi ili muendeshe Chama. Nawaombeni ndugu zangu kuweni na subira sana, hizo ruzuku zinaweza kutumika kama fimbo ya kuwachapia ili nchi iendelee kuwa katika kongwa za udhalimu wa udikteta. Tafuteni namna ya kusurvive ikiwemo kupitia michango ya wanachama.

Kumbueni Chadema, mkibwaga manyanga chini, nchi hii inaingia katika giza nene la udikteta tusiojua hatima yake.

Chadema msituangushe, tuliwapigia kura, msitusaliti, Waacheni wafu wazike wafu wao!
 
Kupeleka wabunge wa viti maalum bungeni maana yake ni KUTAMBUA MATOKEO YA UCHAGUZI MKUU uliofanyika kwa njia za HARAMU, iwapo Chadema itajaribu kufanya huo UPUUZI basi tutawachukulia kama GENGE tu la wasaka tonge na wachumia tumbo.

Tafadhali sana, msimamo wa awali wa kutotambua kufanyika kwa uchaguzi mkuu na matokeo yake na uendelee kuheshimika.
 
Kama yalipelekwa mapema hakuna shida, muhimu kwasasa ni KUTOJITOKEZA HUKO BUNGENI ili kunogesha mchakato mzima wa KUHARAMISHA hicho kinachoitwa uchaguzi mkuu.
 
Hiyo Tume itakua ni Tume ya mashoga. Unakitakaje Chama kilichopinga uchaguzi na matokeo, kikuoe majuna ya wanachama wake wanaopendekezwa kwa viti maalum?
Mnawapuuza malalamiko yao lakini mnatafuta ushirikiano wao.
 

Acha mambo ya kususa ww
Ela ya kuendesha chama utatoa ww?

Keleleele nyingiiiiii mbona hatujakuona barabarani?

Chama kinataka ela ili kujiendesha, Sasa kama hakuna wabunge wa viti maalum do u think Wanapata wapi ela?
 
HAUKUA UCHAGUZI, HAKUNA UBUNGE wala VITI MAALUM.

Brand ya CHADEMA lazima iheshimiwe na kila Mwana CHADEMA, anaetaka kula damu ya VYEO aende CCM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…