Kamati Kuu ya CHADEMA, mkiteua wabunge wa Viti Maalumu kuingia Bungeni, mtakuwa mmefanya kosa kubwa sana

Au unategemea wafuasi wa vyama vya upinzani watakataa kulipa kodi?
Kodi zitalipwa na wote (wapinzani na wasio wapinzani). Lkn kodi zetu ni kiduchu hazitoshelezi mahitaji yetu ya kibajeti.

Ndiyo maana wahisani ni muhimu Sana. Sasa wakigoma kusaidia ni pigo kwa watawala.
 
CCM ya Magulifu ina vituko hajawaigi shinda huyu 2015 masai hii antipa jamaa zao la hewa
 
Kwa msiojua sheria za uchaguzi, tayari majina ya wabunge viti maalum yalikwishapelekwa.

Kwa mujibu wa sheria za Uchaguzi, majina ya viti maalum hupelekwa walau siku 30 kabla ya uchaguzi mkuu. Hivyo majina hayo yapo na jina la kwanza ni Halima Mdee, la pili Esther Bulaya n.k....
 
Ni kweli. Kilichosubiriwa ni idadi ya hao viti maalumu. Inaonekana nafasi hizo kwa chadema zimeongezwa makusudi. Kwasabb hawakustahili idadi kubwa namna hiyo. Ilipaswa kuwa 8 -13
 
vile bunge litakua kijani kitupu kila hoja ndio mzee yajayo yanashangazaa
 
Kwanza nianze kwa kusema, Katika vitu ambavyo CCM kwa sasa wanatamani vitokee, ni kupata wabunge wa upinzani japo wachache ili kuondoa dhana ya Bunge kuitwa Bunge la CCM-Bunge la chama kimoja.

Kwa sababu hiyo,tarajieni kuona wale wale waliowadhulumu haki zenu wakigeuka wema kwenu na kuanza kuonyesha upendo wa kinafiki kwenu na hata wako wataojidai kuwahurumia ila kamwe msiwaamini na wala msiwasikilize.

Hata hill Bunge likianza mtarajie wabunge hawa hawa wa CCM waliofaidika na matokeo haya, wakaanza kutoa kauli za kukumbuka michango ya wapinzani Bungeni ,na hata wanaweza kuja na mapendekezo ya kuwapa mialiko ya kwenda Bungeni kama wageni. Kumbukeni baadhi yao pia nafsi zao zitakuwa zinawasuta na watayatenda haya katika kujaribu kutuliza nafsi zao.

Sio hivyo tu,wanaweza kubadili sheria kuongeza idadi ya wabunge wa kuteuliwa na Raisi, na pia kubadili kanuni/sheria kuongeza wabunge wa vitu maalumu ili nyinyi mpewa nafasi, ila nawambieni kamwe msikubali bali waachieni wao na Bunge lao watimize azima yao na zaidi wakose kisingizio cha kuja kusema wapinzani wanacheleweza/wanakwamisha maendeleo.

Nawaambia angali mapema kabisa kuwa, mkiwa tayari kupeleka wabunge katika Bunge hili,basi pia muwe tayari na masimango kama vile bila huruma ya Raisi au Spika msingekuwa humu ndani, tumewabeba na kauli zingine za aina hiyo pale mtapopishana nao mitazamo ndani ya hilo Bunge.

Pia,iwapo mtapeleka wabunge katika hili Bunge, matapoteza haki na uhalali wa kupinga huu uchaguzi na watatumia uwepo wenu katika hilo Bunge kama hoja ya kujibu tuhuma zozote zinazohusu makandokando ya huu uchaguzi.

Pia,tambueni hata wao wanaelewa mna wafuasi wengi sana katika nchi hii, hivyo ili kutuliza hasira na machungu ya mashabiki wa upinzani na zaidi chuki inayoweza kujenganga,watataka muwepo Bungeni walau kwa uchache na hapa viongozi wa juu wa vyama vya siasa vya upinzani wanaweza kujikuta katika mtihani wa kukubali ubunge wa kuteuliwa na hata kupewa vyeo serikalini.

Kwahiyo,Kamati Kuu ya CHADEMA mkikaa myatafari haya yote na mengine ambayo sijayataja hapa kabla ya kufikiri kukubali kuteua wabunge wa vitu maalumu kuingia katika hili Bunge kwani mtakuwa mmefanya kosa kubwa sana la kisiasa.

Agenda kuu inapaswa kuwa ni kudai Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi na si kufikiria kuteua wabunge wa vitu maalumu kwenda katika hili Bunge.

Wapinzani,kama kweli mnataka kushika dola,basi lazima muwe tayari ku-sacrifice baadhi ya mambo vinginevyo msahau kuingia Ikulu.

Wasiposikiliza haya si wapinzani
 
Ingawa naelewa unakotokea lakini kwenye hili natofautiana na wewe. Mimi nadhani kuwa kuna umuhimu wa Chadema kuwepo Bungeni kwa sababu zifuatazo:
1. Ingawa tutaliita kuwa ni Bunge la CCM lakini ukweli ni kuwa ni Bunge la taifa la Tanzania lenye wajumbe wengi kutoka CCM. Kwa sababu hiyo kuna haja ya uwepo wa wajumbe wataowatetea wananchi na kusimamia taifa lao.
2. Kuingia kwenye Bunge sio ishara kuwa wamekubali matokeo ya uchaguzi. Wao wanaweza kusema kuwa wanaingia under protest. Watakapoapa hawataapia CCM au NEC bali wataapia Katiba ya taifa lao la Tanzania.
3. Wakiwa Bungeni watakuwa na nafasi nzuri ya kuwatetea na kuwasemea kwa Mamlaka wale wote ambao kwa namna moja ya nyingine wataona kuwa hawajatendewa haki na serikali.
4. Watapata nafasi ya kuwakumbusha wananchi na serikali kuwa kuna wanachama wao, wafuasi wao na watu wengine ambao wako ndani kwa kesi ambazo hazina mashiko. Wataweza tena kuikumbusha serikali kuwa majibu bado yanahitajika kuhusu wale ambao wamepotea katika mazingira potofu.
5. Wakiwemo watampa ujasiri mbunge mwenzao wa Nkasi ambae kuweza kuwasemea watu wake. Ingawa inabidi wamuangalie vizuri kwa sababu kuna uwezekano wa yeye kuhamia upande wa pili.
6. Wakiwa wabunge wa viti maalum wasio na majimbo watapata fursa kuwasimamia wabunge waliotoka katika maeneo yao na kuwakumbusha wananchi kuhusu ahadi zao. Halima anaweza kumuuliza kila siku Askofu kuhusu maendeleo ya chuo cha uvuvi na safari za kwenda Marekani.
7. Wabunge watakuwa huru zaidi kusimamia masuala ya kitaifa bila kuathirika sana na wao kutokuwepo majimboni mwao.
8. Chadema inahitaji pesa za kujiendesha. Ruzuku watakayopata itawasaidia sana katika kupunguza gharama za kujiendesha na kujijenga upya. Hawataweza kufanya hivyo kwa kutegemea ada na michango.

Angalizo kubwa ni katika uteuzi wa wabunge wa viti maalum. Kipaumbele kitolewe kwa wale ambao wameonyesha wazi kuwa wana uwezo ws kujenga hoja na wana msimamo usiotetereka. Watu kama Halima Mdee, Esther Bulaya, Esther Matiko, Pendolino Peneza, Salome Makamba, Jesca Kishoka, Suzan Kiwanga na wengine wa calibre hiyo bila kusahau vijana kama yule waliyempora ushindi na kumpa John Mrema, yule aliyegombea Muheza na watu kama Mama Mollel.
Aidha waendelee kuwajenga wapambanaji vijana waliojitokeza kama yule wa Chato. Watu kama Heche, Lema, Msigwa, Sugu, Profesa Lwaitama, Askofu Mwamakula watumike kukijenga chama na kuendelea kuisimamia serikali wakiwa nje ya Bunge.
Waongeze ushirikiano na vyama kama ACT WAZALENDO na CHAUMMA kuendeleo shinikizo la kutaka Katiba Mpya, Tume huru ya uchaguzi na mabadiliko katika utendaji wa vyombo vya dola. Yote haya yanaweza kufanyika hata wakiwa na wawakilishi ndani ya Bunge.
Wakiamua kususa wajue kuwa Chama Tawala kitaendelea kama walivyofanya Zanzibar na hamna watakachoweza kufanya. Presha kutoka nchi za nje si za kutegemea.

Amandla...
Yaani wafanyiwe kila aina ya uharamia halafu waingie bungeni kwa njia ya asante NEC?.

Huu siyo muda wa kugawana nafasi za kula, kuingia bungeni ni kulegitimise mchakato haramu.

Nawaomba sana Chadema wasifuate misimamo ya waliosurrender, wakifanya hivyo kwanza hawataweza kuisaidia nchi kupiga hatua katika demokrasia nchini.
Pili CCM itarudia tena na tena kufanya hii michezo ya kupora haki za wananchi kwa sababu inajua wapinzani at the end of the day watakubali tu.

Mapambano sasa hivi yawe ni kudai katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.

Hao wanaopendekeza eti wabunge wa viti maalum waingie bungeni, waende wakafanye nini kama serikali na wabunge wa kuchaguliwa wamepatikana bila ridhaa ya wananchi? , Sasa waende bungeni wakamtetee nani?, katika nini, ili wasikilizwe na nani?

Muachieni Magufuli bunge lake, Mkiingia huko mtaudissapoint umma kwa kiwango ambacho hakijawahi kutokea.

Msiwasikilize influencers wa CCM waliotumwa humu mirandaoni kujaribu kushape opinion zenu ili mkubali kuhalalisha haramu.

Najua mnahitaji ruzuku na michango ya wabunge ya kila mwezi ili muendeshe Chama. Nawaombeni ndugu zangu kuweni na subira sana, hizo ruzuku zinaweza kutumika kama fimbo ya kuwachapia ili nchi iendelee kuwa katika kongwa za udhalimu wa udikteta. Tafuteni namna ya kusurvive ikiwemo kupitia michango ya wanachama.

Kumbueni Chadema, mkibwaga manyanga chini, nchi hii inaingia katika giza nene la udikteta tusiojua hatima yake.

Chadema msituangushe, tuliwapigia kura, msitusaliti, Waacheni wafu wazike wafu wao!
 
Kupeleka wabunge wa viti maalum bungeni maana yake ni KUTAMBUA MATOKEO YA UCHAGUZI MKUU uliofanyika kwa njia za HARAMU, iwapo Chadema itajaribu kufanya huo UPUUZI basi tutawachukulia kama GENGE tu la wasaka tonge na wachumia tumbo.

Tafadhali sana, msimamo wa awali wa kutotambua kufanyika kwa uchaguzi mkuu na matokeo yake na uendelee kuheshimika.
 
Kwa msiojua sheria za uchaguzi, tayari majina ya wabunge viti maalum yalikwishapelekwa.

Kwa mujibu wa sheria za Uchaguzi, majina ya viti maalum hupelekwa walau siku 30 kabla ya uchaguzi mkuu. Hivyo majina hayo yapo na jina la kwanza ni Halima Mdee, la pili Esther Bulaya n.k....
Kama yalipelekwa mapema hakuna shida, muhimu kwasasa ni KUTOJITOKEZA HUKO BUNGENI ili kunogesha mchakato mzima wa KUHARAMISHA hicho kinachoitwa uchaguzi mkuu.
 
Kwanza nianze kwa kusema, Katika vitu ambavyo CCM kwa sasa wanatamani vitokee, ni kupata wabunge wa upinzani japo wachache ili kuondoa dhana ya Bunge kuitwa Bunge la CCM-Bunge la chama kimoja.

Kwa sababu hiyo,tarajieni kuona wale wale waliowadhulumu haki zenu wakigeuka wema kwenu na kuanza kuonyesha upendo wa kinafiki kwenu na hata wako wataojidai kuwahurumia ila kamwe msiwaamini na wala msiwasikilize.

Hata hill Bunge likianza mtarajie wabunge hawa hawa wa CCM waliofaidika na matokeo haya, wakaanza kutoa kauli za kukumbuka michango ya wapinzani Bungeni ,na hata wanaweza kuja na mapendekezo ya kuwapa mialiko ya kwenda Bungeni kama wageni. Kumbukeni baadhi yao pia nafsi zao zitakuwa zinawasuta na watayatenda haya katika kujaribu kutuliza nafsi zao.

Sio hivyo tu,wanaweza kubadili sheria kuongeza idadi ya wabunge wa kuteuliwa na Raisi, na pia kubadili kanuni/sheria kuongeza wabunge wa vitu maalumu ili nyinyi mpewa nafasi, ila nawambieni kamwe msikubali bali waachieni wao na Bunge lao watimize azima yao na zaidi wakose kisingizio cha kuja kusema wapinzani wanacheleweza/wanakwamisha maendeleo.

Nawaambia angali mapema kabisa kuwa, mkiwa tayari kupeleka wabunge katika Bunge hili,basi pia muwe tayari na masimango kama vile bila huruma ya Raisi au Spika msingekuwa humu ndani, tumewabeba na kauli zingine za aina hiyo pale mtapopishana nao mitazamo ndani ya hilo Bunge.

Pia,iwapo mtapeleka wabunge katika hili Bunge, matapoteza haki na uhalali wa kupinga huu uchaguzi na watatumia uwepo wenu katika hilo Bunge kama hoja ya kujibu tuhuma zozote zinazohusu makandokando ya huu uchaguzi.

Pia,tambueni hata wao wanaelewa mna wafuasi wengi sana katika nchi hii, hivyo ili kutuliza hasira na machungu ya mashabiki wa upinzani na zaidi chuki inayoweza kujenganga,watataka muwepo Bungeni walau kwa uchache na hapa viongozi wa juu wa vyama vya siasa vya upinzani wanaweza kujikuta katika mtihani wa kukubali ubunge wa kuteuliwa na hata kupewa vyeo serikalini.

Kwahiyo,Kamati Kuu ya CHADEMA mkikaa myatafari haya yote na mengine ambayo sijayataja hapa kabla ya kufikiri kukubali kuteua wabunge wa vitu maalumu kuingia katika hili Bunge kwani mtakuwa mmefanya kosa kubwa sana la kisiasa.

Agenda kuu inapaswa kuwa ni kudai Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi na si kufikiria kuteua wabunge wa vitu maalumu kwenda katika hili Bunge.

Wapinzani,kama kweli mnataka kushika dola,basi lazima muwe tayari ku-sacrifice baadhi ya mambo vinginevyo msahau kuingia Ikulu.
Hiyo Tume itakua ni Tume ya mashoga. Unakitakaje Chama kilichopinga uchaguzi na matokeo, kikuoe majuna ya wanachama wake wanaopendekezwa kwa viti maalum?
Mnawapuuza malalamiko yao lakini mnatafuta ushirikiano wao.
 
Yaani wafanyiwe kila aina ya uharamia halafu waingie bungeni kwa njia ya asante NEC?.

Huu siyo muda wa kugawana nafasi za kula, kuingia bungeni ni kulegitimise mchakato haramu.

Nawaomba sana Chadema wasifuate misimamo ya waliosurrender, wakifanya hivyo kwanza hawataweza kuisaidia nchi kupiga hatua katika demokrasia nchini.
Pili CCM itarudia tena na tena kufanya hii michezo ya kupora haki za wananchi kwa sababu inajua wapinzani at the end of the day watakubali tu.

Mapambano sasa hivi yawe ni kudai katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.

Hao wanaopendekeza eti wabunge wa viti maalum waingie bungeni, waende wakafanye nini kama serikali na wabunge wa kuchaguliwa wamepatikana bila ridhaa ya wananchi? , Sasa waende bungeni wakamtetee nani?, katika nini, ili wasikilizwe na nani?

Muachieni Magufuli bunge lake, Mkiingia huko mtaudissapoint umma kwa kiwango ambacho hakijawahi kutokea.

Msiwasikilize influencers wa CCM waliotumwa humu mirandaoni kujaribu kushape opinion zenu ili mkubali kuhalalisha haramu.

Najua mnahitaji ruzuku na michango ya wabunge ya kila mwezi ili muendeshe Chama. Nawaombeni ndugu zangu kuweni na subira sana, hizo ruzuku zinaweza kutumika kama fimbo ya kuwachapia ili nchi iendelee kuwa katika kongwa za udhalimu wa udikteta. Tafuteni namna ya kusurvive ikiwemo kupitia michango ya wanachama.

Kumbueni Chadema, mkibwaga manyanga chini, nchi hii inaingia katika giza nene la udikteta tusiojua hatima yake.

Chadema msituangushe, tuliwapigia kura, msitusaliti, Waacheni wafu wazike wafu wao!

Acha mambo ya kususa ww
Ela ya kuendesha chama utatoa ww?

Keleleele nyingiiiiii mbona hatujakuona barabarani?

Chama kinataka ela ili kujiendesha, Sasa kama hakuna wabunge wa viti maalum do u think Wanapata wapi ela?
 
HAUKUA UCHAGUZI, HAKUNA UBUNGE wala VITI MAALUM.

Brand ya CHADEMA lazima iheshimiwe na kila Mwana CHADEMA, anaetaka kula damu ya VYEO aende CCM.
 
Back
Top Bottom