Kamati Kuu ya CHADEMA, mkiteua wabunge wa Viti Maalumu kuingia Bungeni, mtakuwa mmefanya kosa kubwa sana

Kamati Kuu ya CHADEMA, mkiteua wabunge wa Viti Maalumu kuingia Bungeni, mtakuwa mmefanya kosa kubwa sana

Yaani wafanyiwe kila aina ya uharamia halafu waingie bungeni kwa njia ya asante NEC?.

Huu siyo muda wa kugawana nafasi za kula, kuingia bungeni ni kulegitimise mchakato haramu..
Wasipoenda bungeni wafanye nini?

Toa plan B.
 
Kwanza nianze kwa kusema kuwa, Katika vitu ambavyo CCM kwa sasa wanatamani vitokee, ni kupata wabunge wa upinzani japo wachache ili kuondoa dhana ya Bunge kuitwa Bunge la CCM-Bunge la chama kimoja...
Divide and rule, wanataka wawape ubunge alafu wawashawishi waunge juhudi, huu ni upumbavu tu wa nchi hii
 
Kuna mnyukano huko wa hatari kina Matiko, Mdee, Bulaya, Magelesi and the likes wameunda women wing kushinikiza kamati kuu kuwaruhusu wateuliwe na kushiriki bingeni kama viti maalum, vinginevo wakiwahama wasilalamike.
Matiko and bulaya are too ASSY to be on the sideline....
 
Unatumia nguvu kubwa kuharibu uchaguzi alafu unatoa zawadi eti ya viti 22 ili kumkomoa lissu asiwe raisi, huu ujinga huu Pelekeni lumumba
 
Walioshinda ubunge kama yule dada wa Nkasi aende bungeni, viti maalum nao waende bungeni, na wale wanaoona wameonewa kwenye majimbo yao hawakushindwa kihalali waende mahakamani...
Leo umeongea neo
Chadema wanatakiwa waende bungeni kwa maslahi ya taifa; au wagomee bunge kwa maslahi yao binafsi
 
Wana hasira sana na wamejawa na roho za wivu, visasi kiasi kiasi cha kuwaza suluhu kwao ni mauaji.... na hii inatupa wananchi mwanga wa kuwajua zaidi, tunazidi kuwaona walivyo wachanga kisiasa na kwa maana nyingine hawafai kushika...
Magufuli ndo aliyeanzisha haya mambo ya chuki visas na kutubagua
 
Umakini unahitajika hope wataona hili andiko walifanyie kazi! Bado CHADEMA ni kikwazo kwa CCM ijapokua wameiba kura na kujipa ushindi mezani .
 
Mimi nafahamu idadi ya kura alizopata mgombea uraisi hutumika pia kama mojawapo ya kigezo cha kuamua idadi ya wabunge wa vitu maalumu.
Pole hujui. Idadi ya wabunge at least 5% ndiyo inatumika kupata wabunge wa viti maalum. Kura za mgombea urais zinatumika kupata ruzuku.
 
Wana hasira sana na wamejawa na roho za wivu, visasi kiasi kiasi cha kuwaza suluhu kwao ni mauaji.... na hii inatupa wananchi mwanga wa kuwajua zaidi, tunazidi kuwaona walivyo wachanga kisiasa na kwa maana nyingine hawafai kushika.

Tunahitaji viongozi na chama ambacho kinapokua na mamlaka kitaweka maslahi ya taifa mbele na kujali wananchi wake bila kuhoji tofauti zao za vyama, dini, ukabila. Na hadi sasa chama kinachoweza hayo ni kimoja tuu, nacho ni CCM
Hutaki mpaka leo kukubali mlishinda kwa hila, utakuwa namba moja kwa ubishi duniani.
 
Wasisusie ubunge waende maana wanasimamia katiba na siyo uchaguzi maana wakisusa watapewa wengine na watakuwa wamepoteza nafasi zao kikatiba kwa kuwapa mamluki yaani wawabane wanaosubiri kundondoshewa tonge la mtu mwingine, alafu sasa waache utoto wakutengeneza mikakati ya kitoto waende shule za mikakati ya kushinda dhuruma.

Ila Mimi nimependa aliyeshinda aendelee ili amalizie mipango yakuweka akili za Watanzania sawa hasa vyeti feti waliobaki watimuliwe na mafao yawekwe utaratibu siyo kujizolea mapesa mengi mpaka wanavimbiwa, Kodi ya chinga iongezwe na vitu vingi vitakavyoweka akili ya mapoyo ikae sawa.
 
Waende bungeni kwa mjibu wa katiba na siyo kwamba wamekubali uchaguzi na wakiwa huko wakae kimya yaani ndiyo mzee wakisusa watakuwa wameharibu sana.
 
Kwa uchu wa madaraka,kuna viongozi mule wanatamani hata wachukue nafasi za viti maalum walivyo wapuuzi. Waacheni waliochaguliwa pamoja na viti maalum waende mjengoni, kwani lazima kila siku kina Mbowe na genge lake?
 
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imekitaarifu CHADEMA kupeleka majina 22 ya viti maalumu.

Inasemekana uongozi mkuu wa CHADEMA umeketi leo kujadili kuhusu hili swala. Kikubwa ni wapeleke majina au wasusie.

Maamuzi yoyote yatakaofanywa yatakiathiri chama kwa namna moja ama nyengine. Wakikubali kupeleka majina watahalalisha uchaguzi ambao wameukataa. Pia watapoteza uaminifu kwa watanzania na wanachama wao. Tukumbuke kuna wananchi wengi wameumizwa kwenye uchaguzi huu kukitetea chama. Kuna watu wamepigwa na polisi, wengine wamepigwa mabomu. Kuna ambao wamebambikiwa kesi na hata waliopigwa risasi na kuuliwa.

Unadhani kuna waTanzania watakielewa chama wakipeleka majina ya wabunge ambapo itakua ni sawa na kuipa serikali utetezi kwenye jumuiya za kimtaifa?

Mi ni mtumishi wa balozi ya nchi moja ya magharibi, na niwahakikishieni kuwa kuna msukumo mkubwa kuitaka serikali itende haki katika uchaguzi huu. Hamshangai kwanini kuna ukimya na hakuna sherehe kama ilivyozoeleka? Ubalozi wangu unatafakari kwa kina sana kupunguza misaada nchini na kubadilsiha programu zao zielekezwe kwenye uteteaji wa demokrasia na haki.

Ubaya ni kuwa serikali ipo vibaya sana kifedha. Kwanza uchaguzi huu wote umelipiwa na fedha za ndani, alafu pia kuna pesa chama tawala ilikua inachota hazina kukisaidia chama. Magufuli anajua itakua ngumu kuendesha nchi bila misaada ya wafadhili, tena na hivi anavyopenda miradi mikubwa.

Sasa wanategemea kuwapa CHADEMA hao wabunge 22 ili wapate "defense" na "justification" ya uchaguzi huu. Tena kuna sources nyengine zinasema Ndugai na Magufuli wanapanga kuwateua hao wabunge kwenye kamati mbali mbali za bunge ili kuonyesha kuwa bunge lina wapinzani.

Kwenye upande mwengine wa shillingi, CHADEMA kinahitaji mapato. Kinahitaji hizo ruzuku lakini itakuja at a cost.

Huko Zanzibar pia, ACT-Wazalendo wanafikiria kuhusu serikali ya umoja wa kitaifa utakaomfanya Maalim Seif awe Makam wa Kwanza wa Rais. Tuone itaishiaje.
 
Kwanza nianze kwa kusema kuwa, Katika vitu ambavyo CCM kwa sasa wanatamani vitokee, ni kupata wabunge wa upinzani japo wachache ili kuondoa dhana ya Bunge kuitwa Bunge la CCM-Bunge la chama kimoja..
Hahaha jomba unawadanganya wenzako unataka kuwaingiza Chaka...kwanza unachekesha sijui unatia huruma. Kwa sababu kwanza umeonyesha dharau kwa watanzania kwa maneno yako Ni Kama vile hizo kura wamejipa wenyewe..nikwambie tu kwanza kura sisi wananchi ndio tumewapa kwa sababu tumeona wapo serious na maendeleo ya nchi hii..sio maendeleo ya kinafiki mnayotaka kufanya..hakuna lolote mmekalia makelele tu na mayowe..wananchi tuliamua kwa neema ya Mungu tuwapige chini wote kwa sababu hatuoni faida yenu.

Ni Bora waje wapya nao wajipambanue tuwapime..mliopo Sasa nendeni mkatafute kazi nyingine..wananchi tumeamua Kwa hiyo ukome kudharau wananchi kwa maamuzi yao waliyoyayafanya jomba..Kama huna sera Bora ukaziba mdomo...unless uje utuambie ulikuwa una mkataba na watu kadhaa wawapigie kura..

Don't underrate Tanzanians..Wana maamuzi ambayo dunia nzima wanajua..hawapelekwi pelekwi na mifumo yenu ya kuendeshwa na mabeberu...NOOOOO...unaweza ukaona wanakuchekea Lakini moyoni ukija wanakuchinja..rejea maandiko yangu kadhaa...kwaheri nenda kajipange Sasa hivi hakuna siasa Tena..tuonane 2030 kwa sababu najua 2025 hamna chenu..tunategemea by 2025 Tanzania itakuwa Kama ulaya..no difference...tukutane hapa 2025 tuelezane yatakayojiri...
 
Back
Top Bottom