Kamati Kuu ya CHADEMA, mkiteua wabunge wa Viti Maalumu kuingia Bungeni, mtakuwa mmefanya kosa kubwa sana

Kamati Kuu ya CHADEMA, mkiteua wabunge wa Viti Maalumu kuingia Bungeni, mtakuwa mmefanya kosa kubwa sana

Uchaguzi ulikuwa huru na haki,

Chadema waendelee kususa kama wakitaka.

Wananchi wameielewa CCM.

Taifa halitawasubiri sisi tunasonga mbele.
 
Wakafanye shughuli nyingine wawaachie bunge lao la kijani ,wakatuletee maendeleo jimboni kama wanavyojitutumua
 
Mie nilishapendekeza kwamba CCM na Magufuli need to learn their lesson. Wapinzani wasijishughulishe kabisa na hili BUnge, hata wale wapinzani walioshinda ubunge nilipendekeza wajiuzulu..

Watakosa ruzuku na uwndeshaji wa chama utakuwa mgumu sana hasa kwa sababu hawana source nyingine ya fedha!
 
Walioshinda ubunge kama yule dada wa Nkasi aende bungeni (japo namtilia shaka nyendo zake), viti maalum nao waende bungeni, na wale wanaoona wameonewa kwenye majimbo yao hawakushindwa kihalali waende mahakamani...
Option ya mahakamani waachane nayo, credibility ya mahakama kwa sasa ipo chini sana.
 
Zanzibar kimeeleweka kitu gani?

Zenji tayari nia ya maridhiano tayari inanukia na emissaries tayari wako kazini na jahazi liko katika kung'oa nanga.

Tatizo ni huu uvuguvugu wetu na kudhani tunaweza kupata kote bila ya kupoteza.

Hatukupaswa kukubali kuenguliwa mgombea yeyote wala kusimamishwa kampeni. Mwanzo wa madai halisi ya tume huru ilikuwa hapo.

Tusingekubali popote uchaguzi kuanza bila kuwepo na mawakala wetu wala uchaguzi kuendelea popote bila wao.

Kote tusingekubali kuondoka vituoni kabla ya matangazo yote hapo hapo kutangazwa.

Lugha sahihi za kikomavu zenye kuambatana na vitendo stahiki ndiyo pekee wahuni hawa huelewa.

Angalia ilitusaidia nini kukubaliana na uhuni wao wowote tokea kwenye kukubali uchaguzi bila tume huru hadi kwenye kutangazwa matokeo?
 
Majina tayari yapo tume kabla ya uchaguzi ya vyama vyote na Kuna wabunge wanawekwa majina yao hata Kama wanagombea uchaguzi mkuu hivyo NEC watakuwa washachagua na barua washapewa tatizo wengi ni mashabiki tu hata sheria hawafatilii zinasemaje nasema Tena hao wabunge waende bungeni kuna mengi ya kujua hasa sheria zitakazopitishwa pia wakumbuke ya Zanzibar nini kilitokea, Kuna watu wanahitaji kujua Nini kinafanyika bungeni na wapate taarifa za kina maana Chadema na ACT Wana wanachama wengi wanaohitaji kujua vitu vitakavyopitishwa bungeni na wakienda huku wakigomea uchaguzi mwingine utakaofanyika bila tume mpya na hapo pia watakuwa wamebana nafasi za wanaotaka kupokea tonge lilisusiwa.
 
Utakuwa ni Upumbavu wa kiwango cha kimataifa na mtapoteza Wafuasi na Wanachama wenu
 
Kuna mnyukano huko wa hatari kina Matiko, Mdee, Bulaya, Magelesi and the likes wameunda women wing kushinikiza kamati kuu kuwaruhusu wateuliwe na kushiriki bingeni kama viti maalum, vinginevo wakiwahama wasilalamike.
Hiyo Women wing Bora ihame Tu,kuingia Bungeni baada ya dhulma na unyanyasaji waliofanyiwa ni ujinga wa hali ya juu, Dunia itawashanga
 
Kwanza nianze kwa kusema kuwa, Katika vitu ambavyo CCM kwa sasa wanatamani vitokee, ni kupata wabunge wa upinzani japo wachache ili kuondoa dhana ya Bunge kuitwa Bunge la CCM-Bunge la chama kimoja..
Kiongozi hapa hakuna la kuongeza zaidi ya kupongeza kwa ulichokiweka hapa. Wachukue ushauri huu kinyume cha hapo Watanzania tutakatishwa tamaa. Libaki bunge la kijani tu ili tuone maendeleo.
 
Kuna mnyukano huko wa hatari kina Matiko, Mdee, Bulaya, Magelesi and the likes wameunda women wing kushinikiza kamati kuu kuwaruhusu wateuliwe na kushiriki bingeni kama viti maalum, vinginevo wakiwahama wasilalamike.
Wahame tu. Upinzani kuanza upya inaweza kuwa na afya zaidi kuliko kuwa na hao wenye uroho wa posho za ubunge uliotokana na uchaguzi ulioacha majeraha kwa Watanzania wengi.
 
Zenji tayari nia ya maridhiano tayari inanukia na emissaries tayari wako kazini na jahazi liko katika kung'oa nanga.

Tatizo ni huu uvuguvugu wetu na kudhani tunaweza kupata kote bila ya kupoteza...
Njia ya maridhiano kwangu naiona danganya toto tu, kila siku ataendelea kupewa namba mbili hata kama alistahili kuwa namba moja.
 
Mie nilishapendekeza kwamba CCM na Magufuli need to learn their lesson. Wapinzani wasijishughulishe kabisa na hili BUnge, hata wale wapinzani walioshinda ubunge nilipendekeza wajiuzulu...
Hivi CHADEMA na upinzani kwa ujumla wanazipata hoja nzito kama hizi? Kinyume na hapa wataonekana wapo kwaajili ya maslahi na kuwavunja mioyo Watanzania.
 
Walioshinda ubunge kama yule dada wa Nkasi aende bungeni (japo namtilia shaka nyendo zake), viti maalum nao waende bungeni, na wale wanaoona wameonewa kwenye majimbo yao hawakushindwa kihalali waende mahakamani...
Afadhali ibaki CCM kuliko siasa zinazoendeshwa bila mizani sawa kwa maslahi ya chama kimoja. Endeleeni na bunge la chama kimoja bila wale wapinga maendeleo ili tuone mkituletea Watanzania maendeleo kwa kasi.
 
Back
Top Bottom