Kamati Kuu ya CHADEMA, mkiteua wabunge wa Viti Maalumu kuingia Bungeni, mtakuwa mmefanya kosa kubwa sana

Kamati Kuu ya CHADEMA, mkiteua wabunge wa Viti Maalumu kuingia Bungeni, mtakuwa mmefanya kosa kubwa sana

Acha mambo ya kususa ww
Ela ya kuendesha chama utatoa ww?

Keleleele nyingiiiiii mbona hatujakuona barabarani?

Chama kinataka ela ili kujiendesha, Sasa kama hakuna wabunge wa viti maalum do u think Wanapata wapi ela?

Sasa kama Chama kinadhulumiwa chaguzi, hizo hela za kuendeshea hicho chama zina faida gani? - Yaani kiwepowepo tu bila uhakika wa kushika dola hata kama kikishinda?
 
Kususa ni bad idea na wakisusa watasahaulika kabisa kwa nature ya jpm yeye hajali na wataeneza propaganda kuwa hawataki maendeleo ukichangia na vichwa vya watanzania vilivo vichwa panzi
Kutosahaulika kuna faida gani kama kinatengenezewa mazingira ya kamwe hakiwezi kupewa dola hata kama kikishinda?
 
WANAWAKE CHADEMA WAKOMALIA VITI MAALUM UBUNGE: WASEMA WAKO TAYARI KUVULIWA UANACHAMA WAKIWA BUNGENI

- Ni katika kikao kinachoendelea muda huu bahari beach Hotel

- Wanaume wawataka wanawake wa Viti Maalum kukataa Ubunge huo..
Huo ni Udikteta.
 
Kutosahaulika kuna faida gani kama kinatengenezewa mazingira ya kamwe hakiwezi kupewa dola hata kama kikishinda?
Kususa sio solution nzuri hata kidogo mbona enzi za dr slaa walikuwa few na impact's yake ilionekana, ccm si yakususiwa hapo wakija na propaganda mfu na akili hizi za watanzania wapinzani kuja kuaminiwa itachukua mda mrefu. Waache ujinga wa kususa waende bungeni waje na new strategy.
 
Chadema, kujiimarisha na kujiporomosha vyote viko mikononi mwenu.
Kweli mkuu:
Waligomea uchaguzi wa serikali za mitaa, ikala kwao.
Wamegalagazwa kwenye uchaguzi mkuu, kwa hasara yao
Wagomee kuingia bungeni na kwenye halmashauri za miji, unadhani nani atanufaika?
Chadema wataishia kuwa kama kagenge au ka kijiwe ka mtaani tu.
 
Kwanza nianze kwa kusema kuwa, Katika vitu ambavyo CCM kwa sasa wanatamani vitokee, ni kupata wabunge wa upinzani japo wachache ili kuondoa dhana ya Bunge kuitwa Bunge la CCM-Bunge la chama kimoja...
chadema na upinzani kwa ujumla najua mtatupiwa mifupa mingi sana kama ndoana ya kuwatuliza ili mambo yatulie na ili tuendelee kutawaliwa kikatili na kidikteta. yan nasubiri siku nikiona mmeanza kukubabali kudaka mifupo hiyo migumu isiyo na nyama siku hiyo hiyo nachanachana kadi ya chadema na nachukua likadi la kijani japo sijawahigi kushika likadi hilo tangu nizaliwe hadi sasa nina miaka hamsini keshi.

huu ndo wakati wa upinzani wa kweli Tanzania kujitofautisha na upinzani njaa. chadema na ict mkiloba stepu tu mmekwisha. jiwe anawasubiri kwa hamu muingie laini. ni heri nguruwe wa porini anayejitafutia lakin anao uhuru wa kujilinda na kujitetea dhidi ya adui kuliko nguruwe anayefugwa kwa kupewa kila kitu lakin asiye na uhuru wa kujilinda wala kujitetea bwana wake aamuapo kumchinja....chagueni wenyewe chadema na ict...nasubiri na kadi mkononi...mkikosea tu naichanachana na sintokaa nirudi upinzani tena asilani...huu utakuwa ni utopolo sasa maamaye
 
Kususa sio solution nzuri hata kidogo mbona enzi za dr slaa walikuwa few na impact's yake ilionekana, ccm si yakususiwa hapo wakija na propaganda mfu na akili hizi za watanzania wapinzani kuja kuaminiwa itachukua mda mrefu. Waache ujinga wa kususa waende bungeni waje na new strategy.

Enzi za Dr Slaa, Wapinzani walikuwa wanatafuta ridhaa ya umma, na akina Slaa waliingia bungeni kihalali.

Sasa safari hii wapinzani wameshapata ridhaa ya umma ila wanatendewa uharamia kupitia vyombo na nyenzo za dola. Sasa katika hali hiyo waende bungeni ili kutaka ridhaa ya nani?
 
chadema na upinzani kwa ujumla najua mtatupiwa mifupa mingi sana kama ndoana ya kuwatuliza ili mambo yatulie na ili tuendelee kutawaliwa kikatili na kidikteta. yan nasubiri siku nikiona mmeanza kukubabali kudaka mifupo hiyo migumu isiyo na nyama siku hiyo hiyo nachanachana kadi ya chadema na nachukua likadi la kijani japo sijawahigi kushika likadi hilo tangu nizaliwe hadi sasa nina miaka hamsini keshi..
Watafuatwa mmoja mmoja inbox nakurushiwa mabulungutu watulie

CCM wanataka hela ya wahisani, Upinzani unaweza kuharibu hilo iwapo utaendelea kusisitiza uharamia uliofanyika kwenye uchaguzi huu.

Kwa hiyo watajaribu kuwanunua wale watu influential wa kambi ya upinzani, The worst case ni mbaya zaidi kwa wale watakaogoma kuchukua hela na teuzi
 
Enzi za Dr Slaa, Wapinzani walikuwa wanatafuta ridhaa ya umma, na akina Slaa waliingia bungeni kihalali.

Sasa safari hii wapinzani wameshapata ridhaa ya umma ila wanatendewa uharamia kupitia vyombo na nyenzo za dola. Sasa katika hali hiyo waende bungeni ili kutaka ridhaa ya nani?
Kwani kina Mbowe waliopenda bungeni walishinda kwa NEC hii hii ya ccm au kwa NEC ya kwa trump?

Kwanini sasa hivi wao waliposhindwa ndio wazuie wengi kwenda bungeni wakati Toka enzi hzo uharamia wa kura ulikuwepo.

Halafu viti maalumu ni kwa ajili ya wanawake na ipo kwenye katiba na serikali ni signatories kuhusu Mambo ya gender equality why sasa wameshindwa wanaume wote wazuie hao viti maalumu?

So lengo la CDM ni interest zao na sio masilahi ya nchi na kuheshimu wanawake?
Na kwanini wasuse hzo nafasi za wanawake CDM kususa wanajipoteza mazima hao wanawake wakiwa huko bungeni lazima wataonyesha utofauti wa ccm na CDM, so kususa watajiharibia big time, huko bungeni chuya na mchele utajulikana tu
 
chadema na upinzani kwa ujumla najua mtatupiwa mifupa mingi sana kama ndoana ya kuwatuliza ili mambo yatulie na ili tuendelee kutawaliwa kikatili na kidikteta. yan nasubiri siku nikiona mmeanza kukubabali kudaka mifupo hiyo migumu isiyo na nyama siku hiyo hiyo nachanachana kadi ya chadema na nachukua likadi la kijani japo sijawahigi kushika likadi hilo tangu nizaliwe hadi sasa nina miaka hamsini keshi...
Unawadanganya viongozi wako na unawaingiza chaka kabisa.Mwaka huu kulikuwa na wagombea urais 13 ccm inao uwezo wa kupata wabunge wa upinzani bila hata chadema na ACT kuwemo.Zanzibar Seif alususa lakini serikali haikusimama na ilikubalika kimataifa.
 
Kwa wale wanaosema wasiingie bungeni wangetoa ushauri wa nini wafanye wakiwa nje ya bunge. Waeleze chama kitajiendesha vipi wakiwa nje ya bunge. Waeleze chama kitawapiganiaje waliotiwa ndani kwa kukitetea chama. Lissu ndio huyo anahamia Ubelgiji ambako bila shaka ataendeleza juhudi zake za uharakati.

Kutegemea kuwa nchi za magharibi zitaiwekea serikali vikwazo na kushinikiza mabadiliko wakati nyie wenyewe mmejifungia ndani ni ndoto za alinacha.

Hao wakina dada wanaotaka kuingia bungeni ni wapiganaji na mpaka sasa hivi wajitolea sana kwenye harakati za kutetea maslahi ya wananchi. Hawa wakiwa bungeni wana ujasiri wa kuikosoa serikali pale inapokosea na hivyo kuwafungua macho raia wasio na uelewa.

Wasipokuwepo, serikali itajifanyia inavyotaka wakijua hamna wa kuwaonyesha raia athari za maamuzi yao. Msijidanganye kuwa mtaweza kuwaelimisha kwa kupitia social media.
Mkiwakataza ndio mwanzo wa kuwa insignificant.

Amandla...
 
Kwani kina Mbowe waliopenda bungeni walishinda kwa NEC hii hii ya ccm au kwa NEC ya kwa trump? Kwanini sasa hivi wao waliposhindwa ndio wazuie wengi kwenda bungeni wakati Toka enzi hzo uharamia wa kura ulikuwepo...
Hii NEC ya safari hii imekosa hata chembe ya aibu, ilichokifanya ni ubakaji kabisa wa chaguo la wananchi katika ngazi zote
 
Kwa wale wanaosema wasiingie bungeni wangetoa ushauri wa nini wafanye wakiwa nje ya bunge. Waeleze chama kitajiendesha vipi wakiwa nje ya bunge. Waeleze chama kitawapiganiaje waliotiwa ndani kwa kukitetea chama...
Chama siyo Saccos. Kujali ruzuku badala ya kutetea principles ni kugeuka kuwa chama "ruzuku". Chama cha namna hiyo bora kife kije kingine kinachopigania chaguzi za wananchi ziheshimiwe na tupate mifumo ya kuwezesha hilo. Unfortunately hilo haliwezi kuwezekana kupitia bunge hili la CCM.

Chama kiendelee kutoa elimu ya uraia kwa wananchi kuhusu umuhimu wa tume huru ya uchaguzi na katiba mpya, Wananchi wao wenyewe watajua cha kufanya come the day isiyo na siku wala jina.
Lakini CCM wakuibie Ngamia kisha wakupe sungura na wewe unapokea tu huo ni ujuha na wananchi wataidharau Chadema zaidi.

Yaani wakuvurugie uchaguzi wa wabunge na rais, kisha wakupe viti maalum halafu useme eti ukipiga kelele bungeni kutetea wananchi watajali, let me tell you one thing They care nothing kuhusu kelelekelele hizi za eti maslahi ya wananchi, wangekuwa wanaheshimu maslahi ya wananchi wasingewadharau wananchi kwa kuwaharibia uchaguzi wao!
 
Sasa kama Chama kinadhulumiwa chaguzi, hizo hela za kuendeshea hicho chama zina faida gani? - Yaani kiwepowepo tu bila uhakika wa kushika dola hata kama kikishinda?

Sasa solution ndio kususa?
Inatakiwa kupambana, kuingiza watu bungen at least watu wajue tofauti ya wao na wale
 
Sasa solution ndio kususa?
Inatakiwa kupambana, kuingiza watu bungen at least watu wajue tofauti ya wao na wale
Uingize watu bungeni kuhalalisha haramu?

Watu tayari wameshajua tofauti kati yao na CCM ndiyo maana watu wako na upinzani ila CCM wamefanya uharamia wa kutisha kwenye uchaguzi huu.

Sasa kwa nini ushiriki vikao vya wachawi ama wewe ni mtu safi?
 
Kamati Kuu Ya CHADEMA Ipo Kwenye Kikao. Mjadala Mkubwa Ni Viti Maalumu. Je Wakubali Au Wakatae?

Unadhani Wakubali Kwa Msingi Kwamba Fisi Hasusiwi Bucha? Au Wakatae Kwa Msingi Kwamba Hawakubaliani Na Mchakato Mzima Wa Uchaguzi Na Matokeo Yake? Nini Maoni Yako?

Jadili kwa maslahi mapana ya Taifa, amani, haki na ustawi wa Demokrasia ya kweli nchini
 
Back
Top Bottom