Kamati Kuu ya CHADEMA yawakuta na hatia Kubenea na Komu. Wavuliwa nyadhifa zote chamani na kupewa onyo

Naona unatype huku unabubujikwa na machozi, duwa la kuku halimpati mwewe.

Fikeni bei basi mbona mnaweweseka? Au kauli ya Kubenea inewakata maini? Maana mlikuwa kama mafisi mnadhani mkono wa binadamu ni kweli unaweza kudondoka? Mwe!
 
Kosa linahukumiwa kulingana na mazingira yake si kila kosa hutolewa hukumu ileile usikariri.
Kupanga njama za kumpoteza meya na kumbambikia kesi ya uhujumu uchumi m/kiti we unaona ni kosa dogo?
Hebu linganisha makosa ya zito na makosa ya akina Kubenea uone yapi mazito..
Tatizo hapo ni Komu. Atafukuzwaje naye ni mchaga!? Kubenea ashukuru kuwa na mchaga,kama si hivyo angekuwa kafyeekelewa mbali
 
Naona unatype huku unabubujikwa na machozi, duwa la kuku halimpati mwewe.

Fikeni bei basi mbona mnaweweseka? Au kauli ya Kubenea inewakata maini? Maana mlikuwa kama mafisi mnadhani mkono wa binadamu ni kweli unaweza kudondoka? Mwe!
Nyumbu ni nyumbu tuu..
Hapo wameachwa kwasababu Komu ni mchaga. Hiyo ndio imemponya Kubenea
 
Waambieni Polisi wenu wawakamate wadeal na jinai waliyotenda mnangoja mpaka muambiwe na jiwe?
 

Hiyo clip inapatikana wapi mkuu?
 
Kitendo walichokifanya wabunge wa Chadema , Mh Saed Kubenea na Mh Antony Komu , cha kukiri makosa yao mbele ya Kamati Kuu na kuomba radhi ni cha kupongezwa na kupigiwa mfano , hakika huu ni ujasiri na ukomavu wa kiwango cha juu mno !

Binadamu yeyote aweza kutenda makosa , iwe kwa makusudi ama kwa bahati mbaya , lakini ikitokea akakiri na kuomba radhi mbele ya viongozi wake , mtu huyo si tu wa kusamehewa bali ni wa kupongezwa pia , mtu yeyote mwenye dhamira mbaya hujaa kiburi na dharau kuu , hawezi kukiri wala kuomba radhi

Yaliyopita si ndwele tugange yajayo , Hongera sana Chadema .
 
Mazungumuzo ya faragha kati ya wabunge hao wawili waliyanasa kwa kutumia high communication technology. Ni technology gani hii ambayo wanaitumia kufuatilia faragha za wabunge wao na watu wengine? Jee kitendo cha kuingilia na kufuatilia faragha za mtu kwa sheria zetu si kosa la jinai kweli? Vyombo hivi si ndivyo vinatumiwagwa na majasusi? Walivipata wapi na kwa madhumuni gani? Jee wabunge hao waliofanyiwa ujasusi huo wanaweza kufungua kesi ya jinai dhidi ya chama hiki?

Kubenea na Komu fanyeni maamuzi magumu kabla Pole pole hajafunga mlango.
 
wote tumesikia sued kubenea na anton komu wakikili kuwa walipanga kunteka na kumpoteza meya jacob Bonifaci mbele ya kamati kuu ya chadema

wote tumeumizwa na kulushiana tuhuma nani yuko nyuma ya utekaji hasa wa ndani ya nchi yetu na kushindwa kibaini nani ni nani na wapi pa kuanzia katika jambo zito


wanachadema na wanaccm dini zote na kabila zote wamechukizwa na jambo hili ovu

Jamii ya kimataifa imeshtushwa habari za kuteka zinazo chafua nchi yetu na hasa kuogopesha wawekezaji

kwa kuwa chadema wamewaonya tu hawa watuhumiwa (ushahidi upo kamili) tunaomba mfanye hima kuanza na hawa ili maisha yaendele


wote
 
Jifunze kuandika kishwahili fasaha kwanza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…