Kuendekeza uvunjaji wa sheria, kanuni na taratibu tulijiwekea kama nchi ni hatari sana kwa mustakabali wa Taifa letu. Nchi yoyote hujiita Taifa kwa sababu ya sheria na kanuni mbali mbali. Ni sheria hizo huweka umma katika utulivu( public order). Bila public order, hata mwenye nguvu hushindwa kutawala.
Mimi nashauri tusiendekeze sana uvunjaji wa taratibu zinazoleta order yoyote iwe ya kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni au kijamii.
Wanasiasa wetu waache kufikiria haki ya sasa tu. Nchi ipo hata kesho na kesho kutwa.
Figisu za kisiasa zaweza kufanyika bila uvunjaji wa national order and arrangements.